Itashangaza Dunia kama Waziri wa Afya na Naibu wake hawatafukuzwa kazi ya uwaziri

Itashangaza Dunia kama Waziri wa Afya na Naibu wake hawatafukuzwa kazi ya uwaziri

Mollel ni Dentist, hawezi kujua masuala ya pneumonia. Mwenzake ni MD Russia, hana shule. Sijui wanaosoma Udaktari Urusi huwa wanasoma vitu gani.
 
Wakati wa vita unapaswa kuwa kitu kimoja.vita ya uchumi kubwa kikosa umoja,tunatoa nafasi maadui kuwa winda viongozi wetu, ile biashara yao vaccine iendee. Biashara ya glove,ilidona,sanitizer ikadoda, barakoa ikadoda,dawa ikadoda.sasa ni biashara ya chanjo mungu walinde viongozi wetu

Mkuu sidhani hiyo vita tunaweza kuishinda kwa kufanya mambo ambayo hatuwezi kuithibitishia dunia yanazuia au kuponya huu ugonjwa wa Corona. Kumbuka hili gonjwa ni la kidunia na effort zinazofanyika sasa hivi ni kuhakikisha kila Taifa linafanya taratibu ambazo zinakubalika kimataifa bila kuliacha Taifa lolote nyuma kwani likiachwa tu litakuja kuwa kitovu cha maambukizi. Na hakuna Taifa limebuni chanjo ikakataliwa baada ya kuthibitika kisayansi.
 
Wana Jf kwa jinsi tulivyo katika kipindi kigumu ambacho kimezua hofu kwa kila mtu ni wazi kuwa Waziri wa afya na naibu wake hawastahili kuwepo kwenye hii nafasi mpaka sasa.

Mwaka jana bila kupepesa macho Dk Faustine Ndugulile alieleza ukweli umma wa Watanzania kuwa kujifukisha hakuwezi kuua wadudu wa Covid 19, hii ni sababu hawa virus wakiingia kwa binadamu huingia moja kwa moja kwenye mfumo wa kupumua( mapafu) hivyo hata ukijifukiza ni ngumu kuwaua huko ndani ya mapafu.

Mwaka huu baada ya dalili kuwa hili janga limerudi Tanzania kwa namna nyingine,maana inadaiwa sasa hivi kirusi cha korona kimejibadili. Tumeshuhudia madaktari wawili ambao wanasimamia wizara ya afya wakisisitiza watu kujifukiza. Je hawa watu kwa nini hawakutoa ushauri wa kitaalamu unaozingatia taaluma yao kama Faustine Ndugulile?

Leo hii toka watoe demostrantion namna ya kujifukiza hali inaonekana kuwa mbaya. Maana vifo vya vigogo mpaka makabwela vinazidi kupamba moto. Na tatizo ni hilo la kukosa uwezo wa kupumua.

Karne ya ishirini na moja kuongozwa na wasomi ambao hawezi kusimamia taaluma yao na kumshauri rais namna ya kukabiliana na magonjwa kisayansi ni aibu kubwa. Mawaziri hawa wawili wasisubiri vifo vya watanzania iwe sababu ya wao kujiuzulu.
Napendekeza utimuliwe ccm , sera ya chama ni nyungu wewe unataka kuleta mambo ya mabeberu hapa ?
 
Mollel ni Dentist, hawezi kujua masuala ya pneumonia. Mwenzake ni MD Russia, hana shule. Sijui wanaosoma Udaktari Urusi huwa wanasoma vitu gani.
lengo kuu la kusoma Russia ni masuala ya maofisa kipenyo , huo udaktari ulikuwa ni zuga tu
 
Hivi nyungu inasaidia? Kama haisaidii waziri wa Afya na wizara yake wawe held accountable for misleading the nation, then waweke proper guidelines za kufuata kama nchi nyingine.
Huyu Mungu atamfukuza wala tusisumbuke ni swala la muda
 
Hivi we dogo una general knoweledge ya kubishana na mimi juu ya suala lolote? Au unatafuta umaarufu?
Eeenh, ninakukandamiza sana!

Badala ya kujiona unakandamizwa, chukua fursa kujifunza na achana kabisa na ulaghai.

Huwa sina simile na wanafiki hata kidogo.
 
Back
Top Bottom