ITIFAKI: Ni nani Mkubwa kati ya Waziri Mkuu na Spika wa Bunge?

So Spika anao uwezo wa Kumuamrisha Waziri Mkuu awapo Bungeni na kumuwajibisha Pia panapo Stahili..

Ila Waziri Mkuu hana Uwezo wa Kumuwajibisha Spika kwa namna yoyote ile..
Kosa la nyie wasomi sasa!

Mnazungumzia INAVYOPASWA KUWA kama ndiyo ILIVYO SASA.

Achana na nadharia mkuu, ingia field, tueleweshe kutokana na unachokiona field, uhalisia.

Kuhusu mihimili, kwa sisi 1990 kushuka chini, tulisoma uraia tangu darasa la 3, tumefundishwa hiyo nadharia.

Swali dogo, MWENEZI na WAZIRI MKUU, imekaaje? Kama uliyasikia yaliyotokea, basi ujue INAVYOPASWA KUWA na ILIVYO ni mbingu na ardhi hapa TZ.

Ndo maana kama nchi tunafeli. Jinsi ilivyo huko field;
  • Demokrasia
  • Haki za binadamu
  • Weledi
  • Siasa safi
  • Haki, Amani na Utulivu

Vyote hivyo havifanyi kazi kwa watu walioko huko.
 
Safi.

Umeutanua mjadala.

Zilongwa mbali, zitendwa mbali...🙏🙏
 
Mwenezi anafanya Kazi kwa Kutumia Katiba ya Chama na Anavaa Kofia ya Katibu Mkuu wa Chama..

Chama Tawala ndo Husimamia Serkali iliyopo madarakani kwa Mujibu wa Katiba..

kwahyo Kama waziri Mkuu atakuwa Ni mwanachama wa chama chake bhasi Dhahiri ataweza kuamrishwa au kukumbushwa kutimiza Ilani ya Chama chake..

Viongozi wakuu wa CCM kwa mujibu wa Ibara ya 112 ya Katiba ya CCM


Kwa kuwa Mwenezi anafanya kazi chini ya KM



So Mimi naona Kulingana na katiba zao Yuko sawa
 
Hapa mnakosea sana...

Waziri Mkuu anatajwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania, Katibu Mwenezi ni wa chama cha Siasa.

Sema CCM wanapenda kufanya mazingaombwe kuonesha kuwa chama chao ni kikubwa kuliko serikali.
 
Anyway, kuna mtu aliuliza akaambiwa, kuna mhimili "umejichimbia zaidi".
 
Umemaliza Kila kitu mkuu, Kwa kuongezea tu, Rais ndio serikali na anapaswa kuwa bungeni, kutokana na kuwa na kazi nyingi, anawakilishwa bungeni na Waziri mkuu, hivyo waziri mkuu ni mwakilishi wa Rais Bungeni hivyo anakuwa ni mkubwa kuliko spika wa Bunge. Rais ana wasaidizi wanne ambao yupo karibu nao muda wote, haiwezi kupita siku hawajawasiliana ambao ni Makamu wa Rais, Waziri mkuu, Katibu mkuu kiongozi na Katibu mkuu ikulu
 
Nafikiri ila sina uhakika ndani ya Bunge mkubwa ni Spika,Serikalini Waziri mkuu ni mkubwa kuliko spika
 
Ukijua inaongeza kipato chako kwa asilimia ngapi?, wake up guy
 
Kwa Tz waziri mkuu ndio serikali yenyewe, spika ni kusimamia tu serikali. Hapo ni nani mkubwa?
 
Bado ninataka kujua katika kuondoka kwenye shuhuli au matukio yakiserikali mfano kuzima mwenge,sherehe za uhuru nk je ninani anaanza katiya waziri mkuu na spika?
Hapo ndio itajulikana nani mkubwa
 
Hapa mnakosea sana...

Waziri Mkuu anatajwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano Tanzania, Katibu Mwenezi ni wa chama cha Siasa.

Sema CCM wanapenda kufanya mazingaombwe kuonesha kuwa chama chao ni kikubwa kuliko serikali.
Mkuu CCM ni Chama kinachotawala..
Unajua kwanini waziri Mkuu lazma atokane na Chama chenye Wabunge wengi??


Na ndo maana Katiba Yetu inafahamu kuhusu Mipaka ya Serkali na Chama.. na Imejitoa Kwamba kama Chama Tawala kikiamua haiwezi kuhusika..

Soma katika ya Tanzania 151(2) Kifungu C

Na hapa sasa Ndo hutumika Ilani na Katiba ya Chama cha Mapinduzi


Na kwa Mujibu wa Katiba ya JMT Ibara ya 151 Ibara Ndogo ya 2C Hapo ndo Huja sasa Ile katiba Pendwa ya CCM INASEMAJE KUHUSU viongozi
 
Kuongeza, spika na bunge lake waweza kumuondoa Rais madarakani.
Hata hivyo, katika fikra za wabunge kuomba badala ya kuitaka serikali kufanya au kutimiza wajibu wake kwa wananchi, changamoto ni kubwa.
 
Spika wa bunge ndio mkubwa. Waziri mkuu anahojiwa na spika wa bunge bungeni na anatupa majibu hata kama hataki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…