ITIFAKI: Ni nani Mkubwa kati ya Waziri Mkuu na Spika wa Bunge?

1. Rais wa JMT
2. Makamu wa Rais
3. Rais wa Zanzibar
4. Waziri Mkuu
 
Bado ninataka kujua katika kuondoka kwenye shuhuli au matukio yakiserikali mfano kuzima mwenge,sherehe za uhuru nk je ninani anaanza katiya waziri mkuu na spika?
Hapo ndio itajulikana nani mkubwa
Mkuu Mbona unajipa Stress Mwenyewe..
Sasa Matukio Ya kiserkali unataka Uone spika wa bunge??
SERIKALI (Excutive) Ni muhimili kama Mihimili mingine Mitatu ambayo ni Mahakama na Bunge ..

Sasa Unataka shughuli za Wachaga umuone Msumuma Akiongoza Shughuli Hizo??

Mfano Kuna Koo tatu..
Unataka Kiongozi wa Ukoo Mwingine aongoze ukoo mwingine??

  • Serikali (Excutive) lina Viongozi wake na nimewataja Mkuu Nimesema ni Rais, Makamu ,Waziri mkuu Na wengine wanafuata..
  • Bunge (Pa..) linaViongozi wake na Kiongozi mkuu ni Spika
  • MAHAKAMA lina viongozi wake na Kiongozi mkuu ni Jaji Mkuu
Sasa unataka Kwenye shughuli za Kiserikali Kiongozi wa Bunge aongoze kiprotokali..

Kama Shughuli itakuwa ya Bunge Bhasi Spika huwa wa kwanza na wanafuata viongozi wa Serkali..

kama shughuli ni Ya Serikali bhasi Wanaanza Serkali halafu wanafuata viongozi wa Bunge halafu viongozi wa Mahakama..

Kama sherehe ni Ya kimahakama Bhasi wanaanza Jaji mkuu, Then Serkali then wBunge..

Sijui umenielewa??
Ila kwa mujibu wa Sherehe ulizotaja ni za Kiserkali so Obvious Jibu umepata
 
Kuongeza, spika na bunge lake waweza kumuondoa Rais madarakani.
Hata hivyo, katika fikra za wabunge kuomba badala ya kuitaka serikali kufanya au kutimiza wajibu wake kwa wananchi, changamoto ni kubwa.
Na Pia wanaweza kutokuwa na Imani na Waziri Mkuu na wakamtoa Kwenye Kiti chake wakaweka wanaemkubali wao..

So Spika anaweza kumuondoa Waziri Mkuu ila Waziri Mkuu hawezi kumuondoa spika..

Ziko tofaiti nyingi sana
 
Hadi page ya nne sijaona aliyenukuu Katiba kuhusu hiyo protokali ya uongozi. Basi sawa ngoja nimalizie kuvuna mahindi
 
Hadi page ya nne sijaona aliyenukuu Katiba kuhusu hiyo protokali ya uongozi. Basi sawa ngoja nimalizie kuvuna mahindi
Si tumesema kuwa hii KATIBA HAIFAI, itupwe jalalani. Sasa tutanukuu wapi?
Wacha twende hivi hivi mpaka katiba mpya ipatikane. Hata katika uchaguzi 2024 na 2025 tutakwenda na mabadiliko ya sheria mpya, katiba tupa kule!!
 
Kwa Mujibu wa Katiba Serkali Ya JMT
Waziri Mkuu Ni msaidizi wa Rais wa JMT wakati makamu wa Rais na Rais Hawapo Wakati Rais wa Zanzibar sio..


Kwa Mujibu wa Katiba Waziri Mkuu ni Kiongozi wa Shughuli zote JMT wakati Rais wa Zanzibar Ni kiongozi wa Shughuli za Zanzibar peke yake.



Kubwa Kuliko Kwa Mujibu wa Katiba Rais wa Zanzibar Ni Mjumbe kwenye Baraza La mawaziri..
Kwa Protokali Ameanza kutajwa Rais, Akafata Makamu wa Rais akafata Waziri Mkuu na akaja Rais wa zanzibar na baadaye mawaziri wote..

Kingine Katika Mikutano ya Baraza la Mawziri Huongozwa na Rais na kama Rais hayupo Bhasi makamu Wa Rais na kama Makamu wa Rais Hayupo Bhasi huomgozwa na WAZIRI MKUU..
Na sio Rais wa zanzibar ambaye yeye Huongozwa kikao hicho...




Sasa Mkuu Nakusubiri uniambie Rais wa zanzibar ni mkubwa kwa sheria ipi
 
Hoja huo ukubwa unatokana na Nini!??

Mihimili ipo mitatu

1. Bunge

2. Mahakama

3. Utawala.

Sasa kati ya hiyo mihimili mitatu Waziri Mkuu anaongoza upi??
Ukuu wa kiongozi unategemea aina ya shughuli inayofanyika:

Bungeni ni Spika; Mahakamani ni Jaji Mkuu; na kwenye mikusanyiko ya wananchi ni Waziri Mkuu.

Kwa hiyo Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kwa mtiririko huo ndiyo wakuu katika shughuli za wananchi/kiserikali. Spika na Jaji Mkuu ni waalikwa tu na wakipendelewa wanaweza kupewa nafasi ya kusalimu wananchi.
 
Waziri Mkuu ni kiongozi Mkuu katika muhimili wa Serikali lakini Spika ni kiongozi Mkuu katika Bunge.Ukubwa wao unatofautiana na katika utendaji na uwajibikaji wao kwenye majukumu yao ya kila siku.
 
Huu mjadala ndiyo unaonesha kuwa ni kwa nini ni vigumu kuiondoa CCM madarakani.
 

Mkuu mna ugomvi?
Kama shughuli inaihusu serikali lazima itifaki ya kiserikali ifuatwe...
1.Rais
2.Makamu wa Rais
3. Waziri Mkuu
Hao 3 ndiyo maboss wa huo mhimili.
Ikitokea namba 1 na 2 hawapo nchini anayekalia kiti ni PM kwa katiba yetu ya sasa.
Zamani ilikuwa Spika kisha Jaji mkuu. Leo hiyo haipo kwa kuwa ni mihimili isiyo ya serikali, ni sahihi kabisa.

Sasa Boss wa wote hapo ni nani?
Bila shaka yoyote ni Rais.
M
 
"Nakubaliana na wewe
Muhimili uliojichimbia chini zaidi ni serikali"
By Magufuli John
 
Nimekuelewa kidogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…