Uchaguzi 2020 Itokee Lissu akashinda Urais, akakupa nafasi ya kutoa pendekezo, ni kitu gani alichofanya Magufuli utamwomba akiondoe mara moja?

yeye anapofunga wenzie kwa uhujumu uchumi kwa hila anaona raha. Wako wapi kina Saanane,Mawazo na Azory. ana muda nao? Kwanza hata hapo nimemuone huruma anatakiwa afungwe maisha au life sentence
Endelea Kuota
 
Sheria Kandamizi za kidikteta zifutwe, watuhumiwa wote wapewe Dhamana na iwe ni marufuku kumweka ndani mtu kwanza miaka kisha ndo uanze kutafuta ushahidi miaka.
Ushahidi haujakamilika mtu asiwekwe ndani.
 
1.Vitambulisho vya mjasiriamali
2.Ushuru wa mazao
3.Vyama vya ushirika
Hiyo namba moja, inaonesha wazi kwamba wewe sio "machinga" au mjasiriamali.
Na kama ndio basi umeanza baada ya hivi vitambulisho kuanza kutolewa. Tulionza zamani bado tunakumbuka adha za migambo ya jiji.
 
Uwazi kwenye uendeshaji wa serikali tuone trend ya Kodi zetu zinavyotumika tena walipa kodi ndo tuamue vipi ni vipaumbele vya kuanzia na sio mtu na mtoto wa dada zake ndo waamuzi wa matumizi ya Kodi zetu
 
Huyu haiwezi kutokea akawa rais wa jmt mpaka anakufa, so kujadili eti kuna siku lissu atakuwa rais wa Tanzania ni sawa na kula ugali kwa picha ya samaki.
 
Ningetoa wazo ila tatizo ni Future Impossible Tense.

October 28th kura za kishindo ni kwa JPM.

JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Mahakama ya mafisadi
Umeme wa Gesi na Bomba lake tubaki na mastigila
Chato airport ihamishiwe Geita Mkoani
Mbuga ya Chato ifutwe badala yake itengenezwe zoo Kubwa yenye kila mnyama ili tuje tutalii.
Waalimu waajiliwe kama siku zote Kabla ya 2015 na wakina wamezidi kozi hizo zisitishwe kwa Muda
Bunge live
Tusiongeze ndege Kabla ya kujua hizi zimefikia wapi.
Watanzania na viongozi waende nje ya nchi wapate changamoto Mpya kila kwa utaratibu lakn sio vibali.
Maendeleo kwa wote wapinzani na CCM
 
Hauna hoja
 
1. Tume ya kijaji ya maridhiano,wasiojulikana,mauaji ya kisiasa.
2. Kurejesha mali zote zilizoporwa na CCM majengo na viwanja vya michezo.
3. Wabunge na Madiwani wote waliopitishwa bila kuchaguliwa uchaguzi ufanywe upya.
4. Wakurugenzi wote waliovuruga uchaguzi was hutaki we mara moja.
5. Fedha za vitambulisho vya wanachinga zirejeshwe kwakuwa ni utapeli.
6. Fao la kujitoa kurejeshwa mara moja.
7. Katiba ya Warioba ni muhimu ikamaliziwa mara moja.
8. Futa Ukuu wa Mkoa,Wilaya na ofisi zao mara moja.
9. Futa sheria ya kikanga
 
Wasiojulikana kwanza. Hawa wametukalia vibaya kama nchi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…