Uchaguzi 2020 Itokee Lissu akashinda Urais, akakupa nafasi ya kutoa pendekezo, ni kitu gani alichofanya Magufuli utamwomba akiondoe mara moja?

Uchaguzi 2020 Itokee Lissu akashinda Urais, akakupa nafasi ya kutoa pendekezo, ni kitu gani alichofanya Magufuli utamwomba akiondoe mara moja?

Wengi nasikia tu mnasema ooh Magufuli hajafanya lolote, ooh katupiga sana nk. Lakini pale ninapouliza baadhi ya watu kwamba ni kitu gani ambacho amefanya Magufuli ambacho unaona hakifai, wengi wanashindwa kutoa jibu la haraka.

Sasa leo ningependa kuwauliza katika mtandao wa JF, kwamba ikitokea Tundu Lissu anashinda kiti cha uraisi, na akakuambia toa pendekezo ni kitu gani ambacho Magufuli alikifanya nikiondoe au kukikomesha mara moja, utapendekeza nini?
Faraja jipya LA Salenda,Kigongo-Busisi,Burigi Chato National Park,Uwanja wa michezo Chato,Wakurugenzi wa Halmashauri,ma DC,RC ambao makada wa CCM, kikokotoo kipya mafao ya wafanyakazi,kurudisha fao LA kujitoa,kurejesha watumishi waliofukuzwa kazi kinyume cha sheria/kuwalipa stahili zao na fidia ya usumbufu,kuwalipa waliobomolewa nyumbani/makazi,asilimia ya mikopo ya elimu ya juu/kufuta mikopo,kuwafidia wavuvi,wafugaji waliofilisiwa/kuporwa nyav na mifugo yao na Kuendeleza Mchakato wa Katiba Mpya ya Tanzania.
Mzee Baba ameivuruga Tanzania iliyojengwa na Waasisi kama Mwl.Nyerere,Karume na Mara is waliofuatia.Tumjatae huyu Mzee,ni Diktete hasa.

Eti nilteeni Gwajimaaaa,wanawake weupe na Wabunge/Madiwani anaowapenda yeye.Unajiuliza,hawa tunaoenda kuwachagua ni wawakilishi wa Wananchi,Rais au Serikali?
 
Wengi nasikia tu mnasema ooh Magufuli hajafanya lolote, ooh katupiga sana nk. Lakini pale ninapouliza baadhi ya watu kwamba ni kitu gani ambacho amefanya Magufuli ambacho unaona hakifai, wengi wanashindwa kutoa jibu la haraka.

Sasa leo ningependa kuwauliza katika mtandao wa JF, kwamba ikitokea Tundu Lissu anashinda kiti cha uraisi, na akakuambia toa pendekezo ni kitu gani ambacho Magufuli alikifanya nikiondoe au kukikomesha mara moja, utapendekeza nini?
Magenge ya WASIOJULIKANA, huyu bwana utawala wake umekua wa HOFU na mashaka makubwa. Watu hatuna amani na wala uhakika wa kuiona kesho yetu.
 
Wengi nasikia tu mnasema ooh Magufuli hajafanya lolote, ooh katupiga sana nk. Lakini pale ninapouliza baadhi ya watu kwamba ni kitu gani ambacho amefanya Magufuli ambacho unaona hakifai, wengi wanashindwa kutoa jibu la haraka.

Sasa leo ningependa kuwauliza katika mtandao wa JF, kwamba ikitokea Tundu Lissu anashinda kiti cha uraisi, na akakuambia toa pendekezo ni kitu gani ambacho Magufuli alikifanya nikiondoe au kukikomesha mara moja, utapendekeza nini?
mradi wa bwawa la umeme austopishe kwanza, amflisi magufuli na kumfunga HAPO MOYO WANGU UTAKUWA N.A. MATUMAINI TENA
 
Chuki Mbaya sana
Na Bahati hiyo Hatoipata Ataishia kutumika tu kama Kaptula
Shekhe, safari hii hakuna bao la mkono. Tutapiga kura na KUZILINDA, hizo kura zenu fake mtaziingizia kwenye kituo gani cha kupigia kura?
 
Hongera sana Tundu Antiphas Lissu,

Nakuona Tarehe 28/10/2020 ukienda kupiga kura kituoni, Naona watanzania wengi wakienda kukupigia kura siku hii.

Naona vituo vya kupigia kura vikiwa vimejaa, wananchi wakiwa na furaha wakisema Ni yeye.

Naona zoezi la kupiga kura likiwa limekamilika na maeneo mengi Tanzania wananchi wakiwa mita 200 kusubiri matokeo. Wengi wakiwa hawajali kama kuna mvua au jua wanachotaka ni kupata matokeo yao.

Naona maeneo mbalimbali ya Tanzania wananchi wakianza kushangilia kuwa unaongoza kwa kura nyingi dhidi ya Mpinzani wako Magufuli na naona watanzania wengi wakiwa na furaha huku wakipigwa na butwaa kwani hawaamini yanayotokea.

Naona kiongozi mkuu wa kikosi cha walinzi wa viongozi alifika nyumbani kwako na kukutaarifu kuwa Idara nyeti ya Taifa imeamua kukuwekea ulinzi na nyumba yako ikiwekewa ulinzi na kikosi maalumu cha kulinda viongozi. Hii ni kwa sababu idara imeona ni vyema na vizuri kukutambua rasmi kama amiri jeshi mkuu mtarajiwa.

Mwisho Naona vuguvugu la ushindi wako linawashinda Tume ya Uchaguzi maana Tanzania nzima ni furaha na maandamano ya watu kushangilia kuanguka kwa Magufuli na hatimaye Tume ya Taifa ya Uchaguzi inakutangaza kama mshindi wa kiti cha Uraisi.

Mungu naomba fanikisha na simamia hili kwa Jina la Yesu Kristo. Amen.
 
MImi binafsi kuna mambo ambayo sikubaliani kabisa na Raisi Magufuli, na mengi yamejikita katika style yake ya uongozi ya one man show ya yeye kuwa mihimili yote mitatu ya uongozii, ukiukwaji wa utawala wa sheria nchini, uvunjaji katiba wa makusudi, upendeleo na undugu katika nafasi za uongozi, ukiukwaji haki za binadamu na chuki dhidi ya upinzani na yeyote ambae anamkosoa au kutokubaliana nae hata ndani ya chama chake CCM. Lakini sijaona watu wakiongelea sana mambo haya. Nilitarajia haya ndio yatakuwa mambo Makuu ambayo yatawafanya watu watake kumchagua Lissu kumbadili Magufuli.

Sasa kama watu hawaoni haya mambo kuwa ni tatizo basi Raisi Magufuli sio tatizo kiasi hicho hapa Tanzania. KUmchagua Lissu ili aondoe Chato nadhani ni extreme sana. Suala la pato la kujitoa lina mantiki. Zaidi ya hapo sijaona bado mambo ya msingi.
 
Huyo Lissu si alikuja JF last week akasema tuandike maswali atajibu? Kilichomshinda nn hadi Leo kaingia mitini. Ajibu kwanza maswali yetu
Tatizo ni kwamba atawapa moderators kazi kubwa sana. KUmbuka wauliza maswali wasingekuwa watu wa Chadema, ambao kwao ameshakubalika. Sanasana angepokea idadi sawa ya kejeli, matusi na maswali ya kipuuzi kutoka watu ambao wanashabikia upande wa pili. Kwa hiyo unapaswa kuelewa hili.

Hata Magufuli akija humu JF aulizwe maswali, unategeea atapata comments nyingi za aina gani?
 
Umewauliza swali gumu sana Vibendera
Na ngojea uone kama kuna mwenye jambo la Maana toafuti na Ukibendera wao tu
Yaani Magufuli Ashindwe na Lisu kabisa Hizo ni Ndoto za Kichaa
Ngoja niitunze post hii hadi 29/10 maana ile poll station ya uhakika itakuwa imesha toa matokeo ya uhakika kusubiri Confirmation ya NEC tuu
 
1. Wasiojulikana wajulikane.
2. TBC irudi kuwa chombo cha Taifa sio chama.
3. Arudishe Uhuru Haki na Maendeleo ya Watu.
4. Afute vitambulisho hewa vya Magufuli.
5. Alete Mjadala wa Katiba mpya
 
Naona Lisu kaishiwa sasa anatafuta alishwe maneno ya kuongea kwenye kampeni za lala salama baada ya kugundua kuwa mikutano yote aliyofanya hajawagusa wananchi na kitu cha kueleweka

LISU ni mgombea pekee wa uraisi ambaye anamaliza ngwe yake bila kunadi sera za CHAMA CHAKE
Sera ya Viwanda iliishia wapi?

Katiba mpya huko ccm wana habari nayo?
 
Back
Top Bottom