Itoshe kusema Simba na Yanga ni wadini hasa?

Hao walioposti ramadhan kwenye vilabu vyao wanafanya hivyo kuwapendezesha wachezaji wao na mashabiki zao wa imani hiyo. Sasa wakianza kupeperusha ile bendera ya rangirangi msilalamike pokeeni kama mlivyopokea salamu za ramadhan
 
Maybe Ramadhani imepigiwa promo zaidi na waumini wake kuliko kwaresma.
Sasa achana na yanga na Simba mimi nafatilia EPL,Laliga kipindi kwaresma inaanza hawakupost chochote ila Leo na jana Klabu zote Man U,city,Madrid n.k wotee wamepost Ramadan kareem JE NA WAO NI WADINI??
 
Ni kweli kuna Udini mkubwa, angalia wameanza kuwarubuni vijana wadogo wa kikristo wabadili dini au kuwasilimisha kilaghai
 
Hebu lete mchoro kama huo,unaohusu kwaresma.Halafu si mnasema mwafanya ibada kiroho sio kimwili,sasa vipi upewe pongezi za kimwili?.Waislamu wanafanya ibada kiroho na kimwili,ndio ukaona wanapewa pongezi kimwili na kiroho.
kumbe ndiyo maana kitimoto imeshuka bei?
 
Very true hizi club mi nasema ni za makabila ya pwani na waislam wabara na wakristo wanajipendekeza
 
[emoji419][emoji419]
 
Mumempoteza mtoa mada kwa mifano hai ya vilabu vya nje vile vimepost ramadhan kareem...haya mtoa mada SALAMU ZA YESU WA TONGARENI .....AMINAAA
 
Hivi sasa kumetokea Wakristo niseme wa hovyo sana,hawazingatii maandiko wao ni kila kitu kutaka kufananishwa na vitu vya ajabu ajabu.

Wewe mleta mada huyo unayemwamini (kama kweli unamuamini na kumfuata alishakupa hints namna gani ufanye ktk maisha yako ya imani hapa duniani ila leo unategemea utangaziwe na wacheza mpira yale yanayokuhusu ktk kuishi kile Mungu amekutaka utende ili akuoshe dhambi zako,wewe hujiulizi hata kwanini vyombo vya habari vya Kanisa huwa havitoi update yoyote kuhusu Kwaresma,ni kwa sababu kufunga ni jambo personal la mtu siyo jamii kuanza kuringiana.

Kasome nakuwekea nukuu fupi Mathayo 6
16 Tena mfungapo, msiwe kama wanafiki wenye uso wa kukunjamana; maana hujiumbua nyuso zao, ili waonekane na watu kuwa wanafunga. Amin, nawaambia, wamekwisha kupata thawabu yao.

17 Bali wewe ufungapo, jipake mafuta kichwani, unawe uso;

18 ili usionekane na watu kuwa unafunga, ila na Baba yako aliye sirini; na Baba yako aonaye sirini atakujazi.


Hili neno likawaongoze wote waliojaliwa kuiona Kwaresma na kuiishi,na siyo ushinde njaa yapo mengi ya kufanya duniani na Tanzania kwa sasa wapo watu wengi wenye matatizo maradhi umaskini pita huko saidia hata kwa kuwashauri fanya kitu jamii ifarijike ikujue kweli wewe ni Mkristo na unamfuata Kristo matendo yako yawe njia ya wao nao kutamani kumfuata.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…