ITV siyo sahihi kutoa sauti ya Hotuba ya Tundu Lissu katika Mkutano wa ACT-Wazalendo

ITV siyo sahihi kutoa sauti ya Hotuba ya Tundu Lissu katika Mkutano wa ACT-Wazalendo

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Nimefuatilia mkutano wa ACT Live unaorushwa na ITV.

Tundu Lissu kapewa nafasi ya kuongea, kaongea kirefu, kisha akaanza kuzungumzia hali ya nchi ndani ya miaka mitano iliyopita, na nia na sababu ya kuiondoa CCM madarakani. ITV wakamzimia sauti.

Sasa najiuliza kama ITV inafanya kazi kwa maslahi ya CCM si ni bora mngejiunga kwa Humphrey Polepole naye alikuwa Live?

Hizi tabia za kipuuzi za vyombo vya habari nchini kufanya Censoring, wapinzani pindi wakiwa Live zinaudhi, na zinakatisha tamaa, na zinaonyesha kuwa hivi vyombo vya habari havijwezi.

Nimeona siku hizi ndo mchezo wa TV za online na hii ITV, yaani wapinzani wakianza kupoint out mapungufu ya serikali hii mnawazimia Sauti.

Hivi ITV na heshima zenu zote mmekuwa low kiasi hiki?

Wananchi wanakereka kwa upumbavu kama huu

Kama hamtaki kurusha Live matukio ya wapinzani basi acheni.

Leo ITV wamemzimia Sauti Tundu Lissu takriban dakika kumi na tano nzima.

Haya mambo ya ajabu sana
 
Kama mmefikia hapo basi hakika Ni wazi vyombo vya habari vimeminywa kwa kiwango Cha Lami.

Nadhani wengi mmejionea kilichotokea katika mkutano wa ACT katika ukumbi wa diamond jubilee pale ambapo Bw Tundu Lisu alipokuwa anahitimisha hotuba yake.

Jamaa ITV wameamua kutoa sauti na mwisho wa siku wametuachia manyoya.

Hakika kila rangi zitaonekana.

RIP Dr Reginald Mengi!
 
Achana na hivyo vyombo vya habari vya Tanzania ndugu. Wanadhani Magu anashinda uchaguZi wa mwaka huu. Wasichojua ni kwamba Tanzania inaenda kushangaza ulimwengu mwaka huu. Fundi Antipas Lissu anaenda kuwa raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka huu na wote waliomdhiaki wataenda kumwomba msamaha
 
Achana na hivyo vyombo vya habari vya Tanzania ndugu. Wanadhani Magu anashinda uchaguZi wa mwaka huu. Wasichojua ni kwamba Tanzania inaenda kushangaza ulimwengu mwaka huu. Fundi Antipas Lissu anaenda kuwa raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka huu na wote waliomdhiaki wataenda kumwomba msamaha
Inaumiza Sana watu wanahitaji kuona wanachokipenda halafu mambo yanakuwa tofauti.

Na ndio maana nchi za watu waliondelea kuminya Uhuru wa vyombo vya habari Ni Jambo moja sensitive Sana na Ni la hatari
 
Hawajui kwa udhalimu wa wazi wanaoufanya dhidi ya Lissu ndo mapenzi ya wananchi yanazidi kuongezeka kwake maradufu.

Mtu afunguliwe makesi, apigwe risasi, anyimwe matibabu then anarudi nyumbani vikao vya Chama chake hamuonyeshi, akialikwa kwenye vikao vya marafiki akiongea mnamzimia sauti.

Kwa kweli Enough is Enough nguvu ya umma lazima itamalaki mwaka huu. Waendelee kuongeza mapenzi kwa Lissu kwa udhalimu wao dhidi yake.

Wasichojua CCM na mawakala wao wakiwemo ITV na wengineo ni kuwa Mungu anambeba Lissu. Lissu haitaji kubebwa na wao.
 
Ndo maana nasema Membe ni Janja ya CCM kuumaliza upinzani tena kama walivyofanya kwa Lowasa ndo maana ACT mikutano yao hata Vyombo vya habari vinaoneshaa..!! Lakini Chadema hawawezi sababu watanyooshwa
 
Back
Top Bottom