ITV siyo sahihi kutoa sauti ya Hotuba ya Tundu Lissu katika Mkutano wa ACT-Wazalendo

ITV siyo sahihi kutoa sauti ya Hotuba ya Tundu Lissu katika Mkutano wa ACT-Wazalendo

Nimefuatilia mkutano wa ACT Live unaorushwa na ITV.

Tundu Lissu kapewa nafasi ya kuongea, kaongea kirefu, kisha akaanza kuzungumzia hali ya nchi ndani ya miaka mitano iliyopita, na nia na sababu ya kuiondoa CCM madarakani. ITV wakamzimia sauti.

Sasa najiuliza kama ITV inafanya kazi kwa maslahi ya CCM si ni bora mngejiunga kwa Humphrey Polepole naye alikuwa Live?

Hizi tabia za kipuuzi za vyombo vya habari nchini kufanya Censoring, wapinzani pindi wakiwa Live zinaudhi, na zinakatisha tamaa, na zinaonyesha kuwa hivi vyombo vya habari havijwezi.

Nimeona siku hizi ndo mchezo wa TV za online na hii ITV, yaani wapinzani wakianza kupoint out mapungufu ya serikali hii mnawazimia Sauti.

Hivi ITV na heshima zenu zote mmekuwa low kiasi hiki?

Wananchi wanakereka kwa upumbavu kama huu

Kama hamtaki kurusha Live matukio ya wapinzani basi acheni.

Leo ITV wamemzimia Sauti Tundu Lissu takriban dakika kumi na tano nzima.

Haya mambo ya ajabu sana
Ndo maana siku ya kuchaguliwa kwake waliweka mitambo yao kwapani, na habari yake kwenye taarifa haikuwa na kipaumbele lakini kesho yake walionekana Kisutu na video camera zao zile za kizamani za kuvuta miwaya na kwenye taarifa wakarusha habari ya mahakamani kama taarifa namba moja. Jana pia wakarusha habari ya msajili wa vyama vya siasa akiwaonya CHADEMA kama taarifa yao ya kipaumbele. Lakini hawakuthubutu kurusha taarifa ya wafungwa wakipandisha pendera za ccm Dodoma ila kwenye kikao cha ccm kutwa nzima tunapigiwa makelele. Wamejiondolea sifa ya kubalance taarifa zao kabisa.
 
Lisu ni mmoja wa Watu risk kwa TV ,ITV walishaponzwa na Chadema kuna siku mchungaji Msigwa walimrusha live akaanza kumporomoshea matusi Naibu Spika Tulia Ackson kitu ambacho Ni kinyume na maadili ya utangazaji wakalipishwa faini mamilioni na TCRA

Lisu hajiheshimu akianza kuropoka aweza ponza chombo Cha habari kikafungiwa ndio maana hata magazeti wanakwepa kaandika anayosema sababu yako kinyume na maadili ya uandishi wa habari .Ukiyaandika Ni at your own risk na hajali hata ufungiwe sawa na mikesi haji mahakamani anakutekezea likesi lako

Yuko so careless when it comes to public speaking .Akili yote huwa anaiacha nyumbani kwake kurusha live Ni kujitakia shida hujui Ni wapi atachomoka na dude lililo kinyume na maadili ya uandishi na kulirusha hewani
Nilitaka nikupe mfano wa Lindi hivi majuzi ndo tungelinganisha vizuri ya Lissu na yaliyosemwa huko tuone nani hachungi vizuri ulimi.
 
Asipobadilika na kuchagua maneno, hotuba zake nyingi hasa kipindi cha kampeni hazitarushwa. Media law act 2016 inavibana vyombo vya habari kwenye issue za uchochezi.

Nani yuko tayari kulipishwa mafaini au kufungiwa kisa taarifa za mtu asiyeweza kuji control.
 
Nyie nyumbu tumewaambia sana humu mje na chadema tv mmekuwa na viburi. Nakumbuka nilianzisha uzi humu tukawapa umuhimu wa kuwa na tv yenu hasa kuelekea uchaguzi huu mkuu. Haya yote yalitabirika kwa mtu anayefahamu siasa za bongo. Tatizo kubwa hamjipangi mnafikiri kila kitu kitakuwa taken care of na umaarufu au harakati.

Pia mjifunze kuwadibiti wasemaji wenu. Siku hizi kuna sheria kali za habari na makosa ya mtandao. Hivyo nyie msiishie tu kusema wamekata matangazo yetu. Wenzenu wanazingatia maneno yatayorushwa kwenye vyombo vyao ambavyo vyenyewe ni vya kibiashara, si harakati. Na hili tulilitabiri mapema na kushauri mje na tv yenu ndiyo hivyo mkaleta matusi kibao.
 
Achana na hivyo vyombo vya habari vya Tanzania ndugu. Wanadhani Magu anashinda uchaguZi wa mwaka huu. Wasichojua ni kwamba Tanzania inaenda kushangaza ulimwengu mwaka huu. Fundi Antipas Lissu anaenda kuwa raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka huu na wote waliomdhiaki wataenda kumwomba msamaha
Kama ndoto mnazo.
 
Hili tukio litakuwa endelevu. Jiandae kulizoea [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
nami nimeliona hili mkuu, nawashauri wafanye interviews nyingi na vyombo vya habari vya nje kama BBC, Aljazeera, CNN na wengine wengi wawaeleze mbinyo wa habari za wapinzani TZ...ushahidi tayari upo.
 
ITV wametia aibu kubwa

Eti Superbrand, Superbrand my foot
Wanaogopa kurusha maudhui halisi wanamzimia mzungumzaji sauti

Wamenibore kinyama hawa watu!
ITV sasa wako grp moja na TBCCM na Channel ten. Dio vituo vya kuangalia kwa sasa.
 
Back
Top Bottom