ITV siyo sahihi kutoa sauti ya Hotuba ya Tundu Lissu katika Mkutano wa ACT-Wazalendo

Ndo maana siku ya kuchaguliwa kwake waliweka mitambo yao kwapani, na habari yake kwenye taarifa haikuwa na kipaumbele lakini kesho yake walionekana Kisutu na video camera zao zile za kizamani za kuvuta miwaya na kwenye taarifa wakarusha habari ya mahakamani kama taarifa namba moja. Jana pia wakarusha habari ya msajili wa vyama vya siasa akiwaonya CHADEMA kama taarifa yao ya kipaumbele. Lakini hawakuthubutu kurusha taarifa ya wafungwa wakipandisha pendera za ccm Dodoma ila kwenye kikao cha ccm kutwa nzima tunapigiwa makelele. Wamejiondolea sifa ya kubalance taarifa zao kabisa.
 
Nilitaka nikupe mfano wa Lindi hivi majuzi ndo tungelinganisha vizuri ya Lissu na yaliyosemwa huko tuone nani hachungi vizuri ulimi.
 
Asipobadilika na kuchagua maneno, hotuba zake nyingi hasa kipindi cha kampeni hazitarushwa. Media law act 2016 inavibana vyombo vya habari kwenye issue za uchochezi.

Nani yuko tayari kulipishwa mafaini au kufungiwa kisa taarifa za mtu asiyeweza kuji control.
 
Nyie nyumbu tumewaambia sana humu mje na chadema tv mmekuwa na viburi. Nakumbuka nilianzisha uzi humu tukawapa umuhimu wa kuwa na tv yenu hasa kuelekea uchaguzi huu mkuu. Haya yote yalitabirika kwa mtu anayefahamu siasa za bongo. Tatizo kubwa hamjipangi mnafikiri kila kitu kitakuwa taken care of na umaarufu au harakati.

Pia mjifunze kuwadibiti wasemaji wenu. Siku hizi kuna sheria kali za habari na makosa ya mtandao. Hivyo nyie msiishie tu kusema wamekata matangazo yetu. Wenzenu wanazingatia maneno yatayorushwa kwenye vyombo vyao ambavyo vyenyewe ni vya kibiashara, si harakati. Na hili tulilitabiri mapema na kushauri mje na tv yenu ndiyo hivyo mkaleta matusi kibao.
 
Kama ndoto mnazo.
 
Hili tukio litakuwa endelevu. Jiandae kulizoea [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
nami nimeliona hili mkuu, nawashauri wafanye interviews nyingi na vyombo vya habari vya nje kama BBC, Aljazeera, CNN na wengine wengi wawaeleze mbinyo wa habari za wapinzani TZ...ushahidi tayari upo.
 
ITV wametia aibu kubwa

Eti Superbrand, Superbrand my foot
Wanaogopa kurusha maudhui halisi wanamzimia mzungumzaji sauti

Wamenibore kinyama hawa watu!
ITV sasa wako grp moja na TBCCM na Channel ten. Dio vituo vya kuangalia kwa sasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…