Jacqueline Mengi aendelea kudondokea pua rufaa, mahakama yaondoa maombi yake ya kutaka kuurudisha wosia

Kukosa elimu ni tatizo kubwa sana.Owa mwenye elimu alipaswa alione hili mapema kuwa wale wakubwa ndiyo majority shareholders na ndiyo watakuwa na maamuzi,hata angepata hiyo shares zote za Mzee Mengi kama alivyotaka,angewezaje kuwa na sauti kwa hayo Makampuni huku akiwa ni Minority? Elimu,elimu,elimu.Wazazi tusomeshe watoto wetu wa kike wasije kuwa vituko mbele ya safari
 
Sasa hapa kama sio sheria basi busara itumike kwa pande zote. Najua klyn hawezi kutoka patupu ila ugomvi wao ni ule wosia waachane nao waongee kidugu

Wanavyoendelea kujazana hasira baadae itashindikana hata kuyamaliza kindugu
 
Ingekuwa wewe ungekubali.
Ndugu zako wapewe chao mapema?hata Kama umechelewa kuja duniani?
 
Nimekuuliza ingekuwa wewe ungekubali ndugu zako wapewe chao mapema?hata Kama umechelewa kuja duniani?
 
Umejuaje hawana watoto
 
watoto wa mengi wamechangia Nini kwenye Mali za baba yao?
 
Story ya [mention]Asprin [/mention] watu hamjaelewa ni hivi mengi alikua na umiliki wa 100% ya mali yake kabla, , Mengi alipoachana na mke wake Mercy mgao ukawa hivi 25% zilienda kwa watoto wawili abdiel na rejina, kwahiyo mengi na mercy wakabaki na asilimia 75% ina maana Mengi akabaki na 37.5% na Mercy akabaki na 37.5% , Mercy mtalaka wa Mengi mama yao rejina akafa inamaana shares zake zikahamishiwa kwa watoto wake wawili abdiel na rejina wakawa jumla wana 62.5% ya mali yote kwahiyo majority share ni watoto wakubwa wawili, kwahiyo Mengi baada ya kufariki tunachukua ile 37.5% ya mzee Mengi tunaigawa mara 2 yaani 18.75% atapata jack na wanae na abdiel na rejina watapata 18.75% , kwahiyo asilimia 81.25% ni mali halali ya abdiel na rejina halafu ile 18.75 ndio jack na watoto wake wagawane hapo tunakamilisha 100% ya mali yote, kwahiyo alichofanya jack alitaka yeye apate shares nyingi kwa ujanja yaani apate 75% ya mali halafu rejina na abdiel wabaki na 25 % zao yeye bila kujua wachaga sio wajinga na hata hiyo 18.75 % lazima ataenda tena mahakamani kudai katengwa hapati chochote mtasikia tu atalambishwa hewa hadi achanganyikiwe mtaona.
 
Mkumbuke mzee mengi baada ya kustaafu ukurugenzi utendaji wa makampuni ya IPP na kubakia kama mwenyekiti wa makampuni hayo rejina na abdiel waliingia kama watendaji kwenye makampuni na biashara za familia hivo wanajua kila kitu na hiyo hufanyika na matajiri wengi wakubwa kama alivofanya Bakhresa yeye kwa sasa ni mwenyekiti watendaji ni vijana wake akina yusufu na wengine , au kama alivofanya marehemu Mzee ASAS akabaki mwenyekiti lakini watendaji wakabakia wanae akina Salim na faraja na ndugu zake kwahiyo watoto wakubwa wapo pale wanaelewa whatsgoing on
 
Mimi nimeelewa
Swali langu kwanini waligawiwa mapema wakati wazazi wao hawajafa?
Au nyie wenzangu 25% mnaona ndogo.?
Wamechangia Nini kwenye Mali za wazazi wao?mpaka wapewe hizo 25%.?
Haya Sasa mzee kaoa na watoto kazaa.unawatoa vipi kwenye hizo 25%?
yaani watoto wakubwa wachukue 63%.
Zibaki 37 bado hapo hapo wanataka wapate.
Hamuoni Kama mnawadhulumu hawa wengine?
 
Sidhan kama nyumba ya Moshi alipewa
 
Tumia huu ushauri kwa jack ili ashinde kesi, kwa kukusaidia jack ametumia hii point na haijamsaidia mahakamani yaan ameshindwa
 
Jackline anatafuta kifo tu kugombea Mali ambazo hausiki nazo na amezikuta.

Muhaya hawezi kuwazidi akili wachaga, anajidanganya tu.
Hivi kwa nini wasimtangulize tu?. Anakufa kifo cha kawaida tu kama mafua hivi.
Inatia hasira sana. Mtu amekuja tu katikati from no where. Tena alifanya mipango tu kisanii ya kuwa na mzee. Pili inaaminika moja kwa moja yeye ndie aliemtanguliza mzee.
 

Simple, tena wazo la watoto kupata 25% lilitoka kwa mzee Mengi kwa sababu watoto hao walikua kwenye uendeshaji wa makampuni hayo kitambo, hivo ili waendelee kushiriki ujenzi wa makampuni wakapata na mgao wao kabisa kwani kosa lilikua wapi hapo?
 
Umeandika vizuri sana, asiyeelewa anaendeshwa na ushabiki tu
 
kushindwa sio sababu kuwa Hana haki maana aliyetoa hukumu ni binadamu Kama wewe.
Tumia huu ushauri kwa jack ili ashinde kesi, kwa kukusaidia jack ametumia hii point na haijamsaidia mahakamani yaan ameshindwa
 
Sasa mbona mzee kagawa 37 zake zote kwa mapacha wake mnapinga?
Simple, tena wazo la watoto kupata 25% lilitoka kwa mzee Mengi kwa sababu watoto hao walikua kwenye uendeshaji wa makampuni hayo kitambo, hivo ili waendelee kushiriki ujenzi wa makampuni wakapata na mgao wao kabisa kwani kosa lilikua wapi hapo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…