We nae kama zuzu vile, ngoja nikueleweshe kama mtoto wa miaka mi3, Mengi, Mercy, Abdiel & Regina walikua wanamiliki kampuni ya familia kwa pamoja kila mtu na shares zake ila Mercy na Mengi ni mke na mume, na wao kwa sababu ya ndoa na kwa sababu wao ndio waanzilishi basi lazima shares zao ziwe kubwa, hivyo wao wakachukua 75%, then Abdiel akawa anamiliki 12.5 na Regina 12.5, na hii ni kwa sababu ya mchango wao katika kuanzisha na kuendeleza kampuni hio, ila sababu ni familia, wakaziunganisha zote pamoja kama familia moja na maisha yakaendelea (wanaojua mambo ya mgawanyo wa hisa za makampuni zinavokua waneelewa).
Baada ya kutoelewana kati ya wanandoa wawili(Mengi na Mercy), ikabidi watengane na kuamua kugawanya shares zao, yani kila mtu amiliki kivyake, isiwe tena ya pamoja ambayo ilikua ni 75% for two, sasa wakati wa kutengana, sababu kampuni ina 100% shares za umiliki wa pamoja , ikabidi kwanza kabla ya kugawanywa, kila alie na hisa zake arejeshewe hisa zake ili zibaki za hawa wawili kisha wagawane.
Hivyo Abdiel na Regina wakaondoa shares zao kwanza ambazo Abdiel 12.5 na Regina 12.5 na ukiziunganisha ni 25% walizokua wanamiliki, sio urith ni mali yao binafsi (kama wewe unaponunua nguo zako hapo nyumbani kwenu, siku mzee wako na mama wakiachana, wakati wa ugawaji nguo, za kwako utaziondoa sababu haziwahusu), na ndipo hapo inabaki 75%, ambayo wagawane sasa hao walogombana waachane kwa amani kila mtu abebe chake.
Hivyo wakagawiwa kisheria, sio maamuzi binafsi, mahakama na wanasheria walihusika, hivyo wakagawana hiyo 75% ambayo kila mmoja alipata 37.5%, hivyo Mengi alipata 37.5% na Mercy 37.5%.
Baada ya hapo sasa, Mercy ambae ni mama wa wale watoto walioondoa share zao, akaamua kuwarithisha share zake zote watoto wake wawili, kumbuka kampuni inaendelea, huo ni ugawanywaji tu wa shares ama kwa kiswahili tuite kugawiana uhalali wa umiliki wa kampuni kisheria, hivyo watoto wakaziunganisha shares za mama yao 35.5% na za kwao 25%, zikawa 65%, hivyo watoto ndio wakawa wamiliki number moja wa makampuni wakiwa na share kubwa kuliko baba yao.
Uhusiano kifamilia ukaendelea, na mzee alipoona hawezi tena, akawaachia watoto wake wamuendeshee kampuni na kulinda shares zake, hivyo wao wakaingia mazima kwenye kuendesha shughuli za kampuni hadi baba yao alipopatwa na umauti.
Hivyo kisheria ni haki yao kama watoto kurithi pia 37.5% ya mali za baba yao, ambapo kila mmoja angepata 18.75%. Lakini ikatokea kwamba baba yao alikua na watoto wengine wawili ambao alipata akiwa na mama mwingine, hivyo mgao wa hiyo 37.5% ya baba, itagawiwa kwa watu wa 5, ambao ni watoto wa mke mkubwa walietengana wawili, watoto wawili wa mke mdogo na mke mdogo wa marehemu. Hivyo kila mmoja atapata 7.5%, (inaweza isiwe sawa sababu mke mdogo anaweza akaambulia maybe 3-5% sababu ya muda alioishi na huyo bwana, ila watoto watagawiwa sawia wote wanne na mke mdogo atapewa % zake japo ni ndogo tu.
Sasa cha ajabu kikaja kwenye ule wosia, ambao bila sababu za msingi (tuassume ni kweli marehemu aliuandika yeye), matehemu akaacha kugawa hizi mali zake kwa watoto wake wawili, tena ambao kwa facts kabisa ni wao walioshiriki kikamilifu hadi baba yao kupata mali zote, ni wao wamekua bega kwa bega na baba yao, ni wao wamekua na baba yao for years, ni wao wanajua siri zote za baba yao, alafu anammilikisha mali zote mke mdogo, ambae mahusiano yao yamekubwa na utata mpaka kifo chake, then amerithishwa kiiiiiiiiiiila kitu, tena akipata shida basi arithi ndugu wa mke mdogo.
Kisheria, kama marehemu aliwaondoa watu halali katika urithi wake, ni lazima aandike sababu ya kueleweka kwa nini watu hao hawarithishi chochote, la sivyo wosia unakua batili, na mahakama itautupilia mbali, na kugawa kwa taratibu za kisheria za mirathi za nchi husika.
Nadhani umeelewa. Kinachomuumiza jacky ni kua atapata % ndogo tu, tena atalua kama mtu baki kwenye makampuni ya mzee, na watoto wake pia watakua na shares kidogo sana, tofauti na wale wengine, ila ni haki yao. Angefaa tangu mwanzo akae na familia waamue mambo kifamilia, wala wasingemtupa, pengine angejishusha hata wangeweza kuwapa wadogo zao % zote za baba yao, ama wakaziunganisha pamoja kama watoto, wakaendelea kula maisha, ndio hivyo mtaka vyote kwa pupa, hukosa vyote kwa mkupuo.