PostGE2025 Jaji Chande: Tume imepokea ushahidi toka kwa Watu 63,603
Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Ndiyo ameanza kuisoma hiyo ripoti au bado yuko anaweweseka hajui pa kuanzia! Au ndiyo wanaendelea kutupanga ili tukubaliane mapema na upotoshi wao?
Kukubaliana nao wanajua kabisa hawawezi kutupanga. Hapo ni kutubaka tu,tukubali,tusikubali,wanapita na sisi. Wanajua WaTz bado sn kufikia kuwa Wakenya
 
Kwa sisi tuliojitokeza kuipa ushirikiano tume hiyo hatuna budi kujipongeza kama na mimi nisinge jitokeza, idadi ingekuwa ni watu 63,602, kutokana na mimi kujitokeza idadi imekuwa 63,603, huyo wa 63,603 ni mimi!.

Nipongezeni jameni.

P
We mzee ulitakiwa 29OCT ungekuwa front kama ulivyokuwa magomeni mwembechai.
 
Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Jaji Mohamed Chande Othman, amesema Tume hiyo imepokea ushahidi kutoka kwa Watanzania 63,603 kwa njia mbalimbali.

Amesema ushahidi huo umepatikana kupitia mahojiano ya ana kwa ana yaliyohusisha watu 1,323, mashahidi wa viapo (affidavit) watu 553, madodoso yenye maswali bila kutaja majina ya wahusika watu 4,891, pamoja na mikutano ya makundi 202.

Aidha, Jaji Chande amesema idadi kubwa ya ushahidi imepokelewa kupitia njia ya simu na ujumbe mfupi, ambapo watu 56,445 waliwasilisha taarifa zao kwa njia hiyo.


Soma:
Watupe ripoti yetu.. waiting is over
 
Mother is implicated, also a son. Sasa wanarekebisha ripoti.
Hii ripoti itatupa mwanga.. October 29 ilikua ni janga natumaini nione swala la KMKM huko .

Sasa tukipinga iyo report kwa hoja utaona watu kama akina msigwa wanajitokeza kuongea bullshit .. nawazaga jamaa anatuchukuliaje wa tz
 
Heshima aliyojijengea chande kuanzia tar 23 itakuwa imepotea kama profesa wa jalalani.
 
Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Jaji Mohamed Chande Othman, amesema Tume hiyo imepokea ushahidi kutoka kwa Watanzania 63,603 kwa njia mbalimbali.

Amesema ushahidi huo umepatikana kupitia mahojiano ya ana kwa ana yaliyohusisha watu 1,323, mashahidi wa viapo (affidavit) watu 553, madodoso yenye maswali bila kutaja majina ya wahusika watu 4,891, pamoja na mikutano ya makundi 202.

Aidha, Jaji Chande amesema idadi kubwa ya ushahidi imepokelewa kupitia njia ya simu na ujumbe mfupi, ambapo watu 56,445 waliwasilisha taarifa zao kwa njia hiyo.


Soma:
1776782870967-png.3576968
 

Attachments

  • 1776782870967.png
    1776782870967.png
    354.3 KB · Views: 33
Sometimes unakuwa kama mtoto kwa issues serious Pasko
Kama kujisema mimi ni mmoja wa hao waliojitokeza na kuipa ushirikiano tume ni utoto, then its ok, huu ni utoto, kwa vile kuna wengi walioitwa hawakujitokeza, na kuna wengi wameathirika, wamejinyamazia, sisi tuliojitokeza, tunastahili kupewa pongezi kwa kujitokeza.
P
 
Sasa hii Tume ya Chande sijui itakuja na aina ya majibu ya Tume ya Rwanda, Tume ya Afrika ya Kusini au Tume ya kukingia kifua utawala haramu wa CCM ya Samia ?
Tusubiri tuone kitakachosemwa, ila Ile kauli ya Lipumba kuhusu hii Tume inafikirisha.
 
Kwa sisi tuliojitokeza kuipa ushirikiano tume hiyo hatuna budi kujipongeza kama na mimi nisinge jitokeza, idadi ingekuwa ni watu 63,602, kutokana na mimi kujitokeza idadi imekuwa 63,603, huyo wa 63,603 ni mimi!.

Nipongezeni jameni.

P
Upongezwe kwa unafiki wako au upongezwe kwa kipi?

Unawezaje kuchunguza matukio ya wezi kwa kuita wezi wachunguze wizi?
 
Naona kabisa Chadema ikienda kuangushiwa jumba bovu. Maana kinazungumzwa kikubwa ni ni chanzo cha vurugu, sioni suala la.watu waliouliwa nje ya maeneo ya vurugu na majeruhi wazima waliohitaji matibabu wakitupwa mochwari na pia maiti za maelfu ya watu hazikukabidhiwa kwa mazishi likitajwa.
 
Wajinga waliisha huyo Chande asifikiri anaweza kudanganya watu na hicho kipeperushi cha udaku wanachokileta kwa watanzania.

Kwa akili zao mbovu zilezile za kudanganya watu Samuya alipigiwa kura milioni 32 kwa uchaguzi ulioshindwa kufanyika ndio akili hizo hizo wanatumia kufanya manipulation ya namba za kusanyiko hilo la wastaafu wa CCM wakijiita tume ya uchunguzi.

Nyie zungukeni lakini mjue fika watu hawajazika ndugu zao zaidi ya kuzika viatu,picha na nguo ilhali waliona ndugu zao mnawauwa kwa risasi.

Mbegu mlizopanda mavuno yakifika wakati wake watu wasije kuanza kuulizana imekuaje .

Kuna watu miaka 5-10 mbele wao na familia zao wataomba hifadhi nchi za ng'ambo bila kutarajia kwa kuhofia usalama wao.
 
Naona kabisa Chadema ikienda kuangushiwa jumba bovu. Maana kinazungumzwa kikubwa ni ni chanzo cha vurugu, sioni suala la.watu waliouliwa nje ya maeneo ya vurugu na majeruhi wazima waliohitaji matibabu wakitupwa mochwari na pia maiti za maelfu ya watu hazikukabidhiwa kwa mazishi likitajwa.
Watanzania kwa sasa wanamjua adui yao.

Ni maajabu sana CHADEMA ambayo tunaambiwa ilikufa muda mrefu walikua wameifungia tangu June 10 , 2025 maana yake October 29 , 2025 ilikua na miezi 4 kifungoni haina ofisi, magari wala account za pesa sasa hicho chama kilifanikisha vipi hayo maandamano?

October 29 , mwenyekiti na makamu walikua gerezani kwa tuhuma za uongo.

Barabarani tuliona watu wenye bendera za Tanzania, maji , simu ,skafu na mabango hatukuona bendera hata moja ya CHADEMA.

CCM wanaishi kwenye denial ya miaka ya 60,70,80 ambapo Nyerere licha ya kufuta vyama vyote na kubaki mwenyewe na kufanya chaguzi za maigizo bado alikaribia kupinduliwa mara 7.

Sasa kama wao wanafikiri wanapendwa kwa kulazimisha waifute CHADEMA watatengeneza aina mpya ya upinzani ambao nadhani itakua ngumu kupambana nao zaidi .
 
20 April 2026

RASMI RIPOTI YA UCHUNGUZI MATUKIO YA OKTOBA 29 NA HAKI ZA BINADAMU YA 2025 IMETOLEWA NA LHRC​


View: https://m.youtube.com/watch?v=NmXwlYB3LJw
Kituo cha Sheria na haki za binadamu ( LHRC ) kwakushirikiana na shirika la Zanzibar Fighting Against Youth Challenges Organization ( ZAFAYCO ) Kimezindua rasmi ripoti ya Haki za Binadamu Tanzania ya mwaka 2025 ambapo ripoti inatoa taswira Pana ya matukio na masuala yanayoathiri haki za kiraia na kisiasa pamoja na haki za kiuchumi kijamii na kiutamaduni na vilevile imeibua changamoto za kimuundo zinazoendelea kuathiri utekelezaji wa haki za binadamu sambamba na kuangazia masuala mapya yanayojitokeza katika uwanja wa haki za binadamu nchini.
 
Back
Top Bottom