PostGE2025 Jaji Chande: Tume imepokea ushahidi toka kwa Watu 63,603
Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Watanzania kwa sasa wanamjua adui yao.

Ni maajabu sana CHADEMA ambayo tunaambiwa ilikufa muda mrefu walikua wameifungia tangu June 10 , 2025 maana yake October 29 , 2025 ilikua na miezi 4 kifungoni haina ofisi, magari wala account za pesa sasa hicho chama kilifanikisha vipi hayo maandamano?

October 29 , mwenyekiti na makamu walikua gerezani kwa tuhuma za uongo.

Barabarani tuliona watu wenye bendera za Tanzania, maji , simu ,skafu na mabango hatukuona bendera hata moja ya CHADEMA.

CCM wanaishi kwenye denial ya miaka ya 60,70,80 ambapo Nyerere licha ya kufuta vyama vyote na kubaki mwenyewe na kufanya chaguzi za maigizo bado alikaribia kupinduliwa mara 7.

Sasa kama wao wanafikiri wanapendwa kwa kulazimisha waifute CHADEMA watatengeneza aina mpya ya upinzani ambao nadhani itakua ngumu kupambana nao zaidi .

Nasubirì kwa hamu nione Jaji Othman Chade akijipaka kinyesi ili kumsafisha muuaji.
 
Mimi hata sina wasiwasi na hilo genge la wastaafu wa CCM na kipeperushi chao cha udaku wanachoita ripoti.

Wao wafahamu fika wajinga waliisha Tanzania wataamua wachochee zaidi au wajitoe.
Hawa wajìnga kadiri wanavyojaribu kuzima huu moto ndiyo wanaukoleza, we waache wajichanganye tu.
 
Nafikiri report zote mbili anazo. Ila Ile nyepesi ndio utakuja public ngoja tusubiri tuone
 
Kama kujisema mimi ni mmoja wa hao waliojitokeza na kuipa ushirikiano tume ni utoto, then its ok, huu ni utoto, kwa vile kuna wengi walioitwa hawakujitokeza, na kuna wengi wameathirika, wamejinyamazia, sisi tuliojitokeza, tunastahili kupewa pongezi kwa kujitokeza.
P
Kwanini ambaye hakwenda wamuona hayupo sawa na wewe uliyeenda waona upo sawa, ilihali ilikuwa jambo la hiyari.

Hiyari ni usawa, either uwende au usiende wote mko sawa na mnahitaji pongezi vilevile
 
Kumbe wanachunguza chanzo na sio nani alihusika kumwaga ubongo?

Tutegemee Sababu lukuki nyingine zikitoka kwa akina mwashambwa?
Mkuu, siku muuaji Samuya anawapa go ahaed hilo genge la wastaafu wa CCM aliwapa na maeneo ya kuchunguza kabisa.

Ni sawa wewe upo kwako unapotoa maelekezo kwa watoto wafanye kitu fulani unakua unajua tayari na hutegemei wataenda kinyume na maelekezo hayo.
 

Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Jaji Mohamed Chande Othman, amesema Tume hiyo imepokea ushahidi kutoka kwa Watanzania 63,603 kwa njia mbalimbali.

Amesema ushahidi huo umepatikana kupitia mahojiano ya ana kwa ana yaliyohusisha watu 1,323, mashahidi wa viapo (affidavit) watu 553, madodoso yenye maswali bila kutaja majina ya wahusika watu 4,891, pamoja na mikutano ya makundi 202.

Aidha, Jaji Chande amesema idadi kubwa ya ushahidi imepokelewa kupitia njia ya simu na ujumbe mfupi, ambapo watu 56,445 waliwasilisha taarifa zao kwa njia hiyo.


Soma:
Ripoti comprehensive kama hii inaandaliwa kwa muda mfupi hivi? Lengo la kuhoji watu wengi na kutumia njia za ajabu kuwafikia, lilikuwa ni kuandaa mazingira ya kuficha ukweli na hatimaye kuchakachua ripoti nzima. Nchi hii ina mambo ya ajabu sana.
 
Kwa sisi tuliojitokeza kuipa ushirikiano tume hiyo hatuna budi kujipongeza kama na mimi nisinge jitokeza, idadi ingekuwa ni watu 63,602, kutokana na mimi kujitokeza idadi imekuwa 63,603, huyo wa 63,603 ni mimi!.

Nipongezeni jameni.

P
Asante kwa kutuwakilisha vema mwanaJF. Na sisi JF ni kama tumetoa maoni kupitia kwako mzee Pascal Mayalla
 

Mwenyekiti wa Tume ya Uchunguzi wa matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea wakati na baada ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 29, 2025, Jaji Mohamed Chande Othman, amesema Tume hiyo imepokea ushahidi kutoka kwa Watanzania 63,603 kwa njia mbalimbali.

Amesema ushahidi huo umepatikana kupitia mahojiano ya ana kwa ana yaliyohusisha watu 1,323, mashahidi wa viapo (affidavit) watu 553, madodoso yenye maswali bila kutaja majina ya wahusika watu 4,891, pamoja na mikutano ya makundi 202.

Aidha, Jaji Chande amesema idadi kubwa ya ushahidi imepokelewa kupitia njia ya simu na ujumbe mfupi, ambapo watu 56,445 waliwasilisha taarifa zao kwa njia hiyo.


Soma:
Kwa hizo hadidu za rejea, ni wazi hii tume imekula kodi ya wananchi bure. Hii itabaki kuwa hadithi kama hadithi nyingine za Abunuasi.

Hadidu ambazo hazitaji Idadi ya waliouliwa, wahusika wa mauaji, ni wapi ilipo miili ya wapendwa wetu na adhabu kwa wauaji na waliochoma miili ya marehemu kwenye tanuru la sementi, ni zaidi ya kichekesho.
 
Pretoria, RSA
Tume ya Ukweli na Maridhiano (TRC) Africa ya Kusini

Tume ya Ukweli na Maridhiano (TRC) nchini Afrika Kusini, iliyoanzishwa mwaka 1995 na kuongozwa na Askofu Mkuu Desmond Tutu, ilitumoa mbinu ya haki ya kurejesha uadilifu kama mahakama, kushughulikia ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu uliofanywa kati ya 1960 na 1994. Kwa kuachana na mbinu ya jadi ya kulipiza kisasi ya kesi za Nuremberg ya Ujerumani dhidi ya vigogo wa utawala wa Hitler, TRC ililenga kusema ukweli, ushuhuda wa umma, na msamaha wa masharti ili kukuza maridhiano ya kitaifa.

Mbinu hiyo iliundwa kwa kuzingatia kamati kuu tatu, zikifanya kazi kupitia michakato ifuatayo:

1. Muundo na Kamati
  • Kamati ya Ukiukaji wa Haki za Kibinadamu: Ilichunguza ukiukwaji kama vile mateso, mauaji, kutoweka, na utekaji nyara uliofanywa na serikali ya ubaguzi wa rangi na harakati za ukombozi.
  • Kamati ya Msamaha: Ilizingatia maombi ya msamaha kutoka kwa watu binafsi waliofanya uhalifu uliochochewa kisiasa, mradi watoe taarifa kamili ya matendo yao.
  • Kamati ya Fidia na Urekebishaji: Ililenga kurejesha heshima ya waathiriwa na kutunga mapendekezo ya ukarabati na fidia.

2. Vipengele Vikuu vya Mbinu
  • Vikao Vinavyolenga Waathiriwa: Tume ililenga ushuhuda wa waathiriwa, ikipokea zaidi ya kauli 22,000 na kufanya vikao vya hadhara ambapo waathiriwa wangeweza kushiriki uzoefu wao.
  • Msamaha wa Ukweli: Wahalifu wanaweza kuomba msamaha, kwa "njia ya tatu" kati ya mashtaka na msamaha wa kitaifa, kwa kutumia ufichuzi ili kupata kinga dhidi ya mashtaka ya kiraia na jinai.
  • Uwazi wa Umma: TRC ilifanya mikutano ya hadhara kote nchini—mara nyingi katika makanisa ya ndani na kumbi za miji—iliyorushwa kwenye televisheni ili kurahisisha uelewa wa kitaifa na utambuzi wa umma wa yaliyopita.
  • Haki ya Marejesho na Ubuntu: Mchakato huo uliathiriwa sana na dhana ya Kiafrika ya Ubuntu , ambayo inalenga kurejesha maelewano, kutambua muunganiko, na kukuza upatanisho badala ya kulipiza kisasi.
  • Ukweli Mwingi: Mbinu hiyo ililenga kuanzisha aina nne za ukweli: ukweli/uchunguzi wa kisayansi (ushahidi), hadithi binafsi/masimulizi (uzoefu), mazungumzo ya kijamii (mazungumzo ya jamii), na uponyaji/urejeshaji (malipo).

Takwimu Muhimu na Matokeo
  • Kuchukua Taarifa: Zaidi ya taarifa 21,000 zilishughulikiwa kutoka kwa waathiriwa wa ukiukwaji wa haki za binadamu.
  • Mchakato wa Msamaha: Zaidi ya maombi 7,000 ya msamaha yalipokelewa, huku zaidi ya msamaha 1,500 ukitolewa.
  • Ripoti ya Mwisho: Tume ilichapisha ripoti ya vitabu vingi, ikiandika kuhusu unyanyasaji wa enzi ya ubaguzi wa rangi, ambayo iliwasilishwa kwa Rais Nelson Mandela.
Ingawa TRC ilisifiwa kama mfumo bunifu wa kujenga amani, ilikabiliwa na ukosoaji kwa kuzingatia kwake ukiukwaji mkubwa, ukiondoa athari za kimfumo za ubaguzi wa rangi, na kwa utekelezaji wa polepole wa fidia
Hii tume ya Chande kama isingekuwa ya mchongo ilipaswa kufanya kazi kama hii ya TRC.
 
Back
Top Bottom