PostGE2025 Jaji Chande: Tume imepokea ushahidi toka kwa Watu 63,603
Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Yes. Huyu Pascal Mayalla atakuwa mmoja wa wale mashahidi wa kificho waliokuwa wakitoa ushahidi wakiwa tunduni kama njiwa🤣😂🤣
Duh...!, umejuaje?!, kumbe zile tundu za mashahidi wa kificho, hazisaidii kitu!, mtu umefichwa na bado watu wanawatambua mashahidi wa kificho!.
Sasa itakuweje?.
P
 
Sauti yako ilisikika ukiunguruma kutoka tunduni😂🤣😂
Duh...!, kwa vile witness protection ni haki ya shahidi, na sasa shahidi ambaye ni protected witness amejulikana, hivyo sasa, shahidi huyu aliyejulikana, anapaswa kufanyiwa name change na relocation to a third country, mimi nimechagua US!.

Mkisikia nimehamia US, msishangae!.
P
 
Report itakuwa kama mabandiko ya Lucas Msandambwa, waste of time and money 🤮
 
SEHEMU YA MPITO: SAUTI JUU YA TAIFA NA FUMBO LA KUPONYWA

Kabla ya kufunguka kwa hatua inayofuata, kulikuwa na jambo zito lililonijia—si kwa kelele, bali kwa uzito wa ndani usioepukika.

Maono haya hayakuwa ya mtu mmoja, wala ya mahali pa siri pekee. Yalikuwa juu ya taifa.

Nikaona juu ya Tanzania, kana kwamba anga limebeba kumbukumbu ambayo haijasemwa wazi kwa vinywa vya wengi, lakini imeandikwa katika kilio kisicho na sauti.

Kulikuwa na rejea ya tukio—tarehe iliyopita, lakini isiyoisha ndani ya roho za walioguswa nayo.
29/10/25.

Siku ambayo ardhi ilibeba damu, na ukimya ukafunika ukweli wake.

Lakini katika maono, siku hiyo haikuonekana kama mwisho—bali kama mbegu.

Mbegu ya kilio.

Imeandikwa:

“Damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.” (Mwanzo 4:10)

Na hapo ndipo nilipoanza kuona kwamba si kila tukio linaishia pale linapotokea. Mengine huanza kufanya kazi chini kwa chini, hadi wakati wa kujibu unapofika.

Katika picha iliyoonyeshwa, taifa lilionekana kama mjusi aliyekatika mkia—si kwa kushindwa, bali kwa kujilinda.

Sehemu inakatika ili mwili uendelee kuishi.

Lakini kilichokatika hakifi mara moja—kinatetemeka, kikitoa ishara kwa wanaotazama kwa makini.

Hivyo ndivyo ilivyoonekana.

Jaribio la kujitoa, kujisitiri, kujiponya kwa njia ya muda mfupi.

Lakini ndani yake kulikuwa na jambo jingine likianza.

Sio kwa kelele.

Sio kwa matangazo.

Bali kwa wale wanaoitwa ndani kwa ndani—wale wanaobeba mzigo wa taifa bila kutambulika.

Na hapo nikaonyeshwa muda:

Asubuhi.

Saa kumi na mbili kamili.

Mwanzo wa mwanga, lakini si mchana kamili.

Wakati ambao wachache huamka, na wengi bado wamelala.

Ndipo nilipoona kitu kikianza.

Sauti zisizo na vipaza sauti.

Maombi yasiyoandikwa.

Mioyo inayobeba mzigo bila kuonekana.

Na hapo ndipo neno lilikuja:

“Nimeyasikia.”

Kwa maana imeandikwa:

“Nimeona mateso ya watu wangu… nami nimesikia kilio chao… kwa maana nayajua maumivu yao.” (Kutoka 3:7)

Lakini pia:

“Kama watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekeza, na kuomba… ndipo nitasikia kutoka mbinguni, na kuisamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.” (2 Mambo ya Nyakati 7:14)

Hapa ndipo fumbo linakuwa gumu zaidi.

Kwa sababu si kila kilio huleta mabadiliko.

Lakini kuna kilio kinachofika.

Na kilichoonyeshwa si mwisho wa jambo, bali mwanzo wa mchakato.

Sio uponyaji wa ghafla.

Bali kazi ya polepole—kama mvua ya kwanza kabla ya mavuno.

Taifa halikuonyeshwa likianguka.

Lilionyeshwa likipitia.

Na kati ya kupita huko, kulikuwa na mgawanyiko wa wale wanaoona na wasioona.

Wapo watakaosema: hakuna kilichotokea.

Na wapo watakaojua: kitu kimeanza.

Kwa maana imeandikwa:

“Bwana hatatenda neno lo lote, asipowafunulia watumishi wake manabii siri yake.” (Amosi 3:7)

Lakini siri haifunuliwi kwa kelele.

Hufunuliwa kwa wale wanaosikiliza kati ya mistari.

Hivyo basi, si kila mtu ataelewa mwanzo huu.

Lakini wale walioonyeshwa, watajua kuwa:

Kilio kimefika.

Na kazi imeanza.

Polepole.

Kwa utaratibu usiotambulika kirahisi.

Mpaka pale ambapo matokeo yake yatakuwa wazi kuliko mwanzo wake.

Nitaendelea…


Karibu kwenye uzi huu wangu

 
Kwa sisi tuliojitokeza kuipa ushirikiano tume hiyo hatuna budi kujipongeza kama na mimi nisinge jitokeza, idadi ingekuwa ni watu 63,602, kutokana na mimi kujitokeza idadi imekuwa 63,603, huyo wa 63,603 ni mimi!.

Nipongezeni jameni.

P
Hongera P.
 
Kwa mfano tuliona video huyu kijana anatembea barabarani wakati waandamana wengine wamejificha kwenye vibanda wanarekodi, alipigwa bunduki ya mgongo akafa palepale.
Sasa hii tume si ya ******* tu hii
 
1777107207043.png

Jicho la Saidi Micahel kuhusu kauli ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan baada ya kupokea Ripoti ya matukio ya Oktoba 29. chanzo.DW Kiswahili
 
Ripoti inasisitiza bila huruma kuwa hitimisho lake halikutokana na mawazo au tuhuma, bali ushahidi wa moja kwa moja kutoka kwa wale waliohusika. Metrics za ushiriki mkubwa zilimsaidia Tume kuthibitisha uratibu na actualisation ya machafuko kwa uwazi kamili. #MaridhianoYaTaifa
#TumeYaUchunguziReport
Ripoti Ya Tume
IMG-20260429-WA0128.jpg
 
NJIA STAHIKI ZILIZOTUMIKA KUZUIA NA KUTULIZA MACHAFUKO NA VURUGU za 29 OKTOBA 2025 📌

Watu wamekuwa wanapayuka sana na kuongea mambo mengi kuwa ilitumika nguvu kupita kiasi kutuliza vurugu zile. Swali ni hivi watu wanapochoma moto vituo vya mafuta,vituo vya mabasi,magari ya watu binafsi na serikali huwa kiwango cha kutuliza na kuthibiti nguvu huwa kikoje?

Tume ya Jaji Chande imetafiti jambo hili kwa kina na kwa kuzingatia tishio lililokuwepo na hatari iliyoletwa na wahuni waliokuwa wamefadhiliwa kuchoma moto nchi na kuangusha serikali na na tume ya Jaji Chande imesema yafuatayo kwenye mambo waliyoyagundua na kuyachunguza;

💡Serikali ilichukua hatua mbalimbali ili kuimarisha hali ya usalama na kuwezesha kurejesha utulivu kwa mujibu wa wajibu wake wa Kikatiba (Ibara ya 30 na 31)
💡 Jeshi la Polisi nchini kwa kuzingatia Kanuni za Jumla za Jeshi la Polisi - PGO Na. 274 (8) zinazoeleza hatua za matumizi ya nguvu ambazo ni;

1. Uwepo wa Askari katika eneo husika wakiwa wamevaa sare kama ishara ya kwanza kuonesha kuwa wapo kwa ajili ya kutekeleza jukumu la usalama (presence),
2. (Ilani – Amri ya Maneno) Kutoa maelekezo ya maneno, mf. Tawanyikeni,
3. Udhibiti wa kawaida,
4. Udhibiti Mkali,
5. Nguvu isiyo ya kuua, na
6. Nguvu ya kuua au kujeruhi.

🚨Tume ya Jaji Chande iligundua kuwa licha ya hatua za awali (1-4) hapo juu kuchukuliwa na jeshi la polisi bado vurugu ziliendelea kwa taswira ya vurugu za kupangwa, kuratibiwa na kufadhiliwa

🚨 Vurugu hizi zilipangwa na kufadhiliwa na tume iligundua kuwa moja ya viashiria vya vurugu za kupangwa ni pale ambapo vurugu kuanza kwa wakati mmoja katika maeneo mbalimbali ya nchi, kufunga barabara kabla ya vurugu na kuharibu mali za watu au taasisi zilizokuwa zimelengwa, mathalani vituo vya mafuta, vituo vya Polisi, miundombinu ya Serikali, majengo ya CCM, majengo ya Mahakama, na nyumba za watu binafsi

🚨Tume iligundua kuwa wafanya vurugu na machafuko yale walihusika na matumizi ya silaha za moto (mabomu ya kutengeneza) dhidi ya Jeshi la Polisi

🚨Tume ilibaini yakuwa wafanya vurugu hawa walisababisha majeruhi na vifo kwa wananchi na Polisi, uharibifu wa mali za Umma na binafsi.

🚨Hali hiyo, ilisababisha Jeshi la Polisi kutumia nguvu zaidi kwa lengo la kurejesha utulivu na usalama wa watu na mali zao katika baadhi ya maeneo yaliyokua na ukinzani mkubwa.

#MaridhianoYaTaifa
#TumeYaUchunguziR
IMG-20260429-WA0130.jpg
eport
Ripoti Ya Tume
 
Swali ni hivi watu wanapochoma moto vituo vya mafuta,vituo vya mabasi,magari ya watu binafsi na serikali huwa kiwango cha kutuliza na kuthibiti nguvu huwa kikoje?
You must be sick in the head! Watoto na watu waliouawa majumbani mwao walikuwa wanachoma kitu gani?
 
Nimeandika points zangu nyingiiii nzuriii nikaamua nifute tu.

Sawa mleta mada. Hakukuwa na tatizo lolote kutuliza fujo kwa kuuwa watu wote wale
 
Lazima uwe shetani kuona kuwa watu kuuawa majumbani mwao, wengine wakiwa wanaangalia mpira, wengine wakiwa wanacheza Pool, wengine kuamrishwa walale chini wakalala, wametii, na bado wakauawa. Kuona mauaji yale yalikuwa halali, kwanza ni lazima uwe umebeba roho ya shetani, na mwisho ni lazima uwe na uwendawazimu wa aiana fulani.
Yeyote mwenye akili timamu, na mwenye Roho wa Mungu, anajua kuwa kilichofanyika ulikuwa ni uharamia na ushetani wa hali ya pekee.
 
Back
Top Bottom