Tunkamanini
JF-Expert Member
- Jul 18, 2014
- 377
- 93
- Thread starter
-
- #61
Kuwa wa kwanza kufika ofisini na kuwa wa mwisho kuondoka. Bila kujali zile null proseque alizokuwa anazipiga kifisadi, kesi za kigaidi bila evidence ya kutosha na kipindi chake kutowahi kushinda kesi hata moja chini ya wanasheria wake....
Hii ni hati inayotolewa na DPP yenye nguvu ya kumwondolea mashitaka mtuhumiwa.Fungua hiyo maneno kwa urefu wake
Hii ni hati inayotolewa na DPP yenye nguvu ya kumwondolea mashitaka mtuhumiwa.
Wakati wa DPP Feleshi hati za aina hii zilitolewa kwa watuhumiwa hasa wa mauaji ikiwamo ile ya mtuhumiwa wa mauaji ya Bilionea wa Arusha Erasto Msuya aitwaye Joseph Damas(Chusa).Pamoja na watuhumiwa wengine kumtaja kama mhusika mkuu lakini DPP alimfutia mashitaka kwa kasi ya ajabu..
Dr. Feleshi kila siku ukitoa jmosi ambapo huingia saa mbili na kutoka saa kumi na mbili na jpili ambapo huingia saa nne na kutoka saa kumi na mbili, huingia ofisini saa kumi na moja alfajiri na kutoka saa tatu usiku, huo uhuni na ulevi labda ni wa kimtazamo huu, jamaa alivyo lazima ujiulize mala mbili mbili umwingieje kumuhonga.
Kuwa wa kwanza kufika ofisini na kuwa wa mwisho kuondoka. Bila kujali zile null proseque alizokuwa anazipiga kifisadi, kesi za kigaidi bila evidence ya kutosha na kipindi chake kutowahi kushinda kesi hata moja chini ya wanasheria wake....
Ha ha ha Kama ikulu inavyotisha kwa ulinzi mzito... Rais anavyoogopwa kusogelewa kwa ulinzi Mkali alonao bado wahuni wanamchezea na kuchezea ikulu yetu atakuwa yeye unayedai anakesha ofisini?
Ha ha ha we jamaa inaonesha uwezo wako Wa kufikiri mdogo Sana MTU kukaa ofisini muda mrefu ndo alama ya uadilifu??
Huwa unalala nae huko kwake? Jamaa hamna kitu pale sema kwa Tanzania ilivyo sitashangaa akiteuliwa maana hata uko ikulu kuna vilaza wengi wasiojua hata proof read ya one page mpaka wanatuambia rais ameanza kazi tarehe 8/12/2010 badala ya 2014
Nlisema kama jambo hulijui uliza, unadhani utashinda vipi kesi kama hauna ushahidi wa kutosha? nimetolea mfano kesi moja ya UDA ambayo humu mliipigia sana kelele, Dr Hossea hakutaka Feleshi amjumuishe Kisena kwenye kesi kama mtuhumiwa na badala yake alitaka atumike kama shahidi wakati ushahidi ulikuwa wazi kwamba Kisena and Co walihusika kijinai.
Dr Hossea akahujumu ushahidi ili kumuokoa Kisena na Riz1 hivyo kesi kukosa ushahidi na kupelekea Dr Feleshi kuiondoa mahakamani, nilishangaa sana watu wakimlaumu Feleshi kwa hili badala ya kumpongeza, hamumjui Feleshi msimjaji.
Kwa hiyo unataka kuaminisha kuwa wote waliofanya uchunguzi mpaka kesi ikaenda mahakamani walikosea? kwa nini DPP aliruhusu mshtakiwa akaenda mahakamani? Huyu mfanyabiashara 'crook' ana maslahi gani kwa umma?Unadhani anafanya hivyo kwa kukurupuka tu? ni lazima uamuzi wake ubase kwenye ushahidi na pia maslahi ya umma, kama DCI kawasilisha kwa DPP ushahidi wa kumsafisha mtuhumiwa unadhani DPP atafanya nini zaidi ya kuiondoa kesi? DPP sio chombo chunguzi kumbuka.
Duuuh we jamaa usitake watu tuseme mengi hapa...
Kisena na Riz 1 wanalilindwa na nani Kati ya Hosea na Feleshi??
Unajua vizuri kisa na sababu ya Feleshi kupewa u DPP?
Duh ha ha we chenga hasa Kati ya Hosea na Feleshi yupi ana uhusiano binafsi na huyo kisena na Riz 1?
Unafahamu nani aliyesababisha Feleshi kuzawadiwa ujaji?
Kwa hiyo unataka kuaminisha kuwa wote waliofanya uchunguzi mpaka kesi ikaenda mahakamani walikosea? kwa nini DPP aliruhusu mshtakiwa akaenda mahakamani? Huyu mfanyabiashara 'crook' ana maslahi gani kwa umma?
Siwezi argue na mpu.mbavu kama wewe, nimekuona hata kule kwa Werema ukidai unamfahamu vizuri sana kwamba kazaliwa 1951, we jamaa sioni hata dhima ya mabandiko yako hapa ya kishenzi, muulize Hosea ushaidi wa UDA uko wapi ndo uje ulaumu Feleshi kuiondoa kesi mahakamani.
Huwezi fanya kazi za umma wakati huo huo ukawa mfanya biashara, hiyo pia ni moja ya mambo yanayomtofautisha Feleshi na hao wengine wote.
Matusi na jazba vyanini mkuu wangu??
Mbona mi nipo kawaida tu nachangia bila povu vipi mwenzangu?
Sasa ya Werema yamekujaje? Halafu nakushauri tu informations nyingi za kwenye hiyo website ni inaccurate kabisa....
Na pili kwa Tanzania enzi za kina werema hakukuwa na vyeti vya kuzaliwa so watumishi wengi walifoji miaka ili watumike kwa muda mrefu...
Usihamishe mjadala turudi kwa Feleshi...
Nimekuuliza Feleshi na Hosea nani anamahusiano binafsi na huyo Tapeli Kisena na Riz one?
Kila MTU anajua the whole system ilivyokuwa na kigugumizi juu ya umiliki Wa UDA Leo unaleta utetezi Wa hovyo?
Feleshi asingefika hapo alipo bila kuwa na uhusiano Wa karibu na kina JK....
Vipi kesi za akina Rwakatare ilikuaje zikafika kortini bila ushahidi Wa kina?
Huyu Tunkamanini ndiye Dr Eliezer Feleshi mwenyewe anajipigia debe ili ateuliwe kuwa AG. Angalia posts zake zote utaona kuwa Ana habari za ndani kabisa ambazo anapaswa kuwa nazo mhusika tu na si mtu mwingine, halafu anapokutana na arguments za wachangiaji wengine wanaokosoa au kutoa mapugufu ya Feleshi basi anatoa povu kwa jazba. Hii ni aibu kwa mtumishi wa umma kwenye ngazi aliyofikia kutumia fake ID ya mitandao ya jamii kujipa sifa ambazo hana ili kumshawishi Raisi amteue. Aibu acha hizo Dr Eliezer Feleshi.