Jaji Elinaza Luvanda ajiondoa kuendesha kesi ya Mbowe na wenzake baada ya washtakiwa kudai hawana imani naye

Jaji Elinaza Luvanda ajiondoa kuendesha kesi ya Mbowe na wenzake baada ya washtakiwa kudai hawana imani naye

Baada ya Jaji Luvanda kutupa mapingamizi yote yaliyotolewa na Mawakili wanaomtetea Mbowe na wenzake, Mbowe amesimama na kumtaka Jaji Luvanda ajiondoe kuendesha kesi hiyo kwani ameonyesha upendeleo na taarifa zinasema ana maelekezo ya kupindisha sheria ili amfunge Mbowe na wenzake.

...... Jaji Luvanda amesema hati ya mashtaka ni batili amewashauri mawakili wa serikali wakaibadilishe, mawakili upande wa utetezi wamegoma wamemwambia kama hati ya mashtaka ni batili basi futa kesi Jaji akakataa ila amekubali kujiondoa kuendesha kesi.

UPDATE: Jaji Luvanda akubali
- Jaji Elinaza Luvanda aliyekuwa akisikiliza kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, amekubali kujiondoa katika kesi hiyo baada ya kushauriwa kufanya hivyo-MCL

View attachment 1926212
Aibu yake na aibu ya uzao wake,ipo siku kama si yeye wanawe watalipa. This is a promise.
 
Hii haimanishi judge anaingilia mwenendo wa kesi..na anatoa maelekezo nini cha kufanya..ili iweje..hiyo ni kazi ya judge??kwakuwaambia wakairekebishe inamaana anakubali imekosewa..and what does the law say hati inapokosewa..na ombi la kina kibatala lilikuwa ni nini kuhusiana na hati??
Mkuu uko sahihi ombi la kina Kibatala lilikuwa sio kuomba mawakili wa serikali wabadilishe hati bali kufuta kesi.
 
Binge dhaifu,serikali legelege Sasa litakuwa Jambo la hatari Sana Kama na mahakama itakuwa dhaifu. Uhuru wa mahakama huwa inatakiwa kulindwa na mahakama yenyewe Tena kwa wivu kabisa.
 
awasilishe mahakamani kama anao ushahidi juu ya hayo anayo mtuhumu nayo, sio kumchafua Jiji bila ushahidi.

kama hakuna ushahidi Jaji aendelee.

Kibatala anazidi kumchimbia shimo bila yeye kujielewa maskini Mbowe!!!

Hoja ya kitoto kweli hiyo eti unamkataa Jaji?!! tena unatoa tuhuma za kizushi na majungu ya kumchafua Jaji?

halafu hao mawakili wanamfundisha ujinga kama huo!!
Wenzio ujinga wanazificha kwa kunyamaza, tunaona mahakamani kila leo vibaka wanawakataa mahakimu na wanabadilishwa hiyo ni haki kisheria kumkataa jaji au hakimu ukiwa haurishishwi na uendeshaji wa kesi acha kulopoka
 
Jaji asikubali upuuuzi na ushenzi huu wa Mawakili wa Mbowe na Mbowe mwenyewe.

Huko ni kumtusi Jaji na Mahakama,

Mbowe na mawakili wake hawana sababu ya msingi zaidi ya kutaka kumyumbisha Jaji, tuhuma wanazo zitoa dhidi ya Jaji ni za kipuuuzi na hazina uthibitisho wowote zaidi ya kudhania na kuhisia tu, hakuna hoja hapo, kwa hiyo anamtaka Jaji ambaye ni RAFIKI YAKE ili asikilize kesi yake.

kwa hiyo imefikia sasa Mtuhumiwa kuchagua Jaji wa kusikiliza kesi yake aisee! hata marekani hakuna kitu kama hicho.

ninacho sema Jaji angeweza kujitoa kama tuhuma zinazo tolewa na Mbowe zina uthibitisho la sivyo Jaji aendelee tu kungurumisha kesi.......asikubali kubabaishwa na hoja za kipuuzi na za kuokoteza na zenye lengo la kuchelewesha haki kutendeka.
Jaji mwenyewe amekubali kuwa hoja zina mashiko halafu wewe unasema ni za kipuuzi? Zingekuwa za kipuuzi asingemtaka DPP akarebishe hati yake ya mashtaka kwa sababu iliyopo ni batili.

Na anajua kuwa hawezi kutenda haki ndio maana amejitoa. Kesi nzima ni aibu tupu. Wanalazimisha visivyo lazimika. DPP akatae kuendelea nayo na amuomba msamaha Mbowe.

Amandla...
 
Hakuna aibu yoyote hata kwenye sheria na miongozo ya kimahakama inasema hivyo endapo patakuwepo malalamiko yenye uzito hakimu au jaji anawajibika kujitathimini na kuchukua uamuzi wa kujiondoa kutunza heshima yake na yataasisi ya kutafsiri sheria. Matokeo ya kesi hiyo ni yaleyale tu hata akija mtu mwingine kuiendeleza
Kuna ushahidi au zile laki sita..MiCCM nonsense
 
Pole sana Mh Mbowe..

Ni vyema Mh Mbowe na team yake pamoja CDM ili suala mpambane zaidi kisheria kuliko kuleta siasa... tukijikita kwenye siasa tunaweza kusahau masuala muhimu ya kisheria na mwisho ukawa mbaya halafu bado tukaendeleza harakati za kisiasa za Free Mbowe....

Siasa ina mambo mengi, unaweza kuwekewa mtego na wewe ukajaa huku maadui zako wakiwa na malengo ya baadaye kukumaliza kwa wewe kuingia kwenye target yao bila kijua...mfano unaweza kuchokozwa baada ya watu kujua unahasira na wewe kupitia hasira zako ukaua kifupi utakuwa na kesi ya kuua...TUWE MAKINI....

Mambo mengine ni ujinga; kwa hiyo huko mahakaman wanapambama kisiasa?
 
Tulishasema tangu mapema kwamba hizi kesi za kutengeneza huwa zina mambo yake , kama binadamu wakati mwingine roho inakusuta .

Baada ya kuanikwa mitandaoni na Sauti Kubwa , hatimaye leo Jaji Luvanda amekubali kujitoa kwenye kesi ya Mbowe , baada ya kuombwa kufanya hivyo kutokana na kumstukia kwamba anatumika .

Huu ni ushindi wa kwanza .
Kumbe alikuwa kama KONDOO hajui aendako. Ametumika sana kuwakandamiza wanyonge kwa kiapo na mishahara yetu.
 
Tuhuma alizo zitoa Mbowe dhidi ya Jaji Luvanda sio tu zinamchafua yeye bali zinawachafua Majaji wote na Muhimili wa Mahakama.
Hivyo Mbowe na Mawikili wake walipaswa wathibitishe tuhuma hizo nzito.
Wewe ni mpumbavu. Swala la kutenda au kutotendwa kwa haki huwa ni hisia kwanza kisha sababu. Jaji anakiri hati ya mashaka ni batili. Lakini anataka jamhuri ibadilishe hati hiyo hiyo. Unajua kuwa hati haibadilishwi bali hufutwa tu?? Unajua kwanini watu huachiwa huru lakini wakishatoka eneo la mahakama hukamatwa tena na kushtakiwa kwa makosa mengine?? Kutaka hati batili ibadilishwe ndio hasa sababu inayomfanya Mbowe amkatae Jaji!! Sababu hiyo tu inatosha kisheria!! Na Jaji hataki kuifuta japo ni batili kwa sababu anajua akifanya hivo, mawakili wa utetezi watakataa Mbowe asishtakiwe kwa kosa lolote lililo katika hati hiyo batili!! Angeweza tu kuifuta kesi na kumwachia huru Mbowe na kisha Mbowe akakamatwa nje ya mahakama na kushtakiwa kwa hati nyingine tena!! Wewe kiazi huna uwezo wa kutambua haya, wewe ni shabiki maandazi!!

Kuhusu kumchafua mmoja na ukawa umechafua mahakama. Hiyo ni hoja ya layman. Hujawahi kusikia hukumu imetolewa na ikakatiwa rufaa na mrufani akashinda na kuwa huru? Kwanini unadhani hiyo sio alama kuwa mahakama si chombo cha haki?? Ni kwa sababu mahakama ni mfumo wa sheria unaochukua maamuzi kwa mizania ya watu binafsi!! Ni mizania hiyo hupingwa na kukatiwa rufaa, sio mahakama kama chombo/system. Na ni haki ya aliyehukumiwa kupinga mizania ya hakimu/jaji na ni maamuzi yake ndio uhojiwa, sio mfumo wa mahakama!! Ni sawa na kusema hili, kujitoa kwa Jaji Luvanda sio mwisho wa kesi hii wala sio mwanzo wa mfumo wa mahakama kujiondoa!!

Mmezoea kufanya uovu dhidi ya watu wasiokuwa na ufahamu wa haki zao au wasiokuwa na nguvu kifedha kuweka wajuzi wa sheria ili kujiokoa na adhabu zenu. Mwimba ngombe wa laki 4 anafungwa miaka 6 "ili iwe fundisho" halafu mnakutana na "don" aliyepoteza mabilioni ya serikali akipewa kifungo cha miaka miwili au kulipa faini ya milioni 8!! Kwa mwendo huu mtajikuta hata wale washtakiwa watatu wa mwanzo nao wanaokoka kupitia Mbowe bila kujua kama walitenda makosa yanayowahusu au la!

Binafsi ninataka haki itendeke na kujiondoa kwa Jaji sio kiashiria cha haki kutendeka wala kutotendeka!!
 
Kwani kesi inaendeleaje huko wakuu tuambiane kinachojiri kuhusu hii kesi
 
Nitoe tu maoni binafsi na mapendekezo kuhusiana na mifano na mienendo ya kesi mbali mbali ambazo nimewahi kusikiliza na kuhudhuria, mara nyingi mtuhumiwa huwa anajisikia vizuri kama yeye anasikilizwa na anatendewa kwa mujibu wa sheria. Mahakama ni muhimili pekee ambao unaheshima yake na imani yake, wananchi huiamini mahakama na kuipa heshima kadri na wakati unao faa, Mhakama si muhimili wa kuelekezwa na haitakaa itokee kwa sababu wanasimamia vifungu vya sheria mbalimbali na kutoa maamuzi kwa mujibu huo.

Sijafurahia kwa leo kusikia mtuhumiwa kumkataa jaji sijui Mkuu wao anajisikiaje, kwa kusikia kitu kama hiki maana linampa ukweli kwamba imani imepotea kwa kesi hiyo sasa hapa tunahitaji kuwapa imani wananchi kuhusu muhimili huo, hii lazima iwe kauli ya mkuu wa majaji hapa nchini. Lakini bado nafasi ipo ya kutosha kwa jaji ajaye kujua na kuelewa kwa kipi na kwanini walikataa kuendelea na kesi hiyo na jaji huyo na kujitahidi sana makosa kama haya yasijirudie maana yakijirudia tu basi wananchi wakipoteza imani basi watatafuta njia nyingine ya kusaidiwa ili wapewe haki yao.
 
Baada ya Jaji Luvanda kutupa mapingamizi yote yaliyotolewa na Mawakili wanaomtetea Mbowe na wenzake, Mbowe amesimama na kumtaka Jaji Luvanda ajiondoe kuendesha kesi hiyo kwani ameonyesha upendeleo na taarifa zinasema ana maelekezo ya kupindisha sheria ili amfunge Mbowe na wenzake.

Jaji Luvanda amesema hati ya mashtaka ni batili amewashauri Mawakili wa serikali wakaibadilishe, Mawakili upande wa utetezi wamegoma wamemwambia kama hati ya mashtaka ni batili basi futa kesi Jaji akakataa ila amekubali kujiondoa kuendesha kesi.

UPDATE: Jaji Luvanda akubali
Jaji Elinaza Luvanda aliyekuwa anaisikiliza kesi ya Uhujumu Uchumi nyenye mashtaka 6 yakiwemo ya ugaidi, amejitoa kusikiliza kesi hiyo, sababu ya kujitoa kwake, ni kutokana na mshtakiwa wa nne katika kesi hiyo, Mhe. Freeman Mbowe na wenzake kuwa hawana imani na Jaji huyo.

Pia soma > Mahakama ya Uhujumu Uchumi: Mvutano mkali kesi ya Mbowe na wenzake. Hatma ya kesi kujulikana Septemba 6
Mambo haya kwenye tasnia ya sheria ni ya kawaida sana wala hakuna la ajabu hapa! Huo ndio weledi unaotakiwa hasa hasa huko Mahakamani. Hongera sana Jaji Luvanda.
 
Back
Top Bottom