Baada ya Jaji Luvanda kutupa mapingamizi yote yaliyotolewa na Mawakili wanaomtetea Mbowe na wenzake, Mbowe amesimama na kumtaka Jaji Luvanda ajiondoe kuendesha kesi hiyo kwani ameonyesha upendeleo na taarifa zinasema ana maelekezo ya kupindisha sheria ili amfunge Mbowe na wenzake.
...... Jaji Luvanda amesema hati ya mashtaka ni batili amewashauri mawakili wa serikali wakaibadilishe, mawakili upande wa utetezi wamegoma wamemwambia kama hati ya mashtaka ni batili basi futa kesi Jaji akakataa ila amekubali kujiondoa kuendesha kesi.
UPDATE: Jaji Luvanda akubali
- Jaji Elinaza Luvanda aliyekuwa akisikiliza kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na wenzake, amekubali kujiondoa katika kesi hiyo baada ya kushauriwa kufanya hivyo-MCL
View attachment 1926212