Sandinistas
JF-Expert Member
- Jul 5, 2013
- 2,612
- 1,776
Ndiyo maana huyo JPM hayupo nasi sasa hivi. Kila zama na kitabu chake. Zama za JPM hazikuwa zama za raia kulinda katiba ya nchi yao bali ya kila mmoja kunusuru uhai wake binafsi. Kwa msingi huo yule mwenye kumpa binadamu uhai na kumuondolewa anapohitaji kufanya hivyo aliachiwa hiyo hukumu. Naye bila kuwahi wala kuchelewa alihukumu kwa wakati wake. Hakika JPM alikuwa mwovu lakini alituaminisha kuwa angalau alikuwa na dhamira njema ya kulinda rasilmali za nchi dhidi ya waporaji. Tatizo lake kubwa: kiakili hakuwa mzima sana, roho mbaya, ushamba, ubinafsi uliopitiliza na alikuwa mbumbumbu wa siasa na uongozi. Kwa sababu hizo alijielekeza vibaya sana na kujikuta anapambana zaidi na raia wenzake kuliko kutoa uongozi. Kwa haya ya zama hizi, mkakati wa kipaumbele ni kupigania kwa nguvu zote utawala bora na utawala wa sheria.Kipindi cha utawala wa JPM alikuemo nchini? Kama ndiyo aache unafiki akae kimya kama alivyo ka kimya wakati jpm ana nagisi mihimili ya nchi, ka ni hapana hakuepo na muonea huruma hi nchi inatawaliwa na CCM sia sharia