Jaji Warioba: Dkt. Bashiru ajibiwe kwa hoja, hajafanya kosa lolote acheni kumshambulia

Hii ni point sn
 
Kwa mantiki yako hii maana yake hakuna mtu anayepaswa kutoa ushauri wowote juu ya uongozi katika Nchi hii.
Sababu tukisimamia misingi unayoamini hakuna msafi hata mmoja.
Hivyo tuache kulalamika kwa lolote,kuanzia mfumuko wa maisha,ufisadi n.k maana hakuna msafi

Sent from my CPH2219 using JamiiForums mobile app
 
Jibuni kwa hoja mnaambiwa

Ova
 
CCM ni kusanyiko la majangili tupu
 
JIBU HOJA, Bashiru wa enzi ya Magu alikuwa Mlevi!!!

Mlevi hujibiwa akiwa POMBE imekata, na Si wakati amelewa.

Bashiru huyu ndiye Bashiru halisi, Ajibiwe Kwa hoja.

..wako wanaosema tabia halisi ya mtu hujionyesha wakati ana madaraka au akiwa amelewa.
 

..nakubali Bashiru atetewe.

..lakini itapendeza kama Bashiru atawaomba radhi wale waliodhalilishwa na kuteswa wakati akiwa Katibu Mkuu wa Ccm.
 
Umri wa huyo Mzee, unaeza usiofikie pamoja na takataka ulizoandika hapa .jibuni hoja ya Bashiru Ali..
 
Kazi kaimaliza, kazi imebaki kwao ama wasuke ama wawe vipara. Yeye kamaliza na wananchi tumemwelewa Dr. Bashiru. Mwananume hang'ating'ati maneno, Bravo!!
 
Itakuwa amekusikia, na bila shaka atakumbuka anayotetea yeye mwenyewe juu ya uhuru wa watu kusema kama ulivyosema wewe hapa maneno yanayoonyesha kwamba mnayotetea nyinyi ni maslahi yenu binafsi na siyo maslahi ya nchi na wananchi wake.

Kazi yenu ni kazi ya kusifia tu, hata kisichofaa kusifiwa.
 
Yaani amekuwa kama kichaa, hakuna wa kumsikiliza siku hizi
Are you serious Kweli umefikiri Kabla ya kuandika comments zako mbili ? Napata wasi wasi kuwa hata wewe waweza kuwa Aina ya mbunge kibajaji au Good luck au Msukuma.

Kweli wewe unaweza kuwa think Tank ya Taifa na ukategemewa kuleta Matokeo chanya kwenye jamii! Kwamba unaona kwako ni Bora kusifiwa tu badala ya kujitazama!

Viongozi ambao ni pro government wanaolewa sifa zisizokua na maana na kukataa kujitazama na kusimamia maslahi ya wananchi hawatufai hata kidogo!
Integrity ya mzee Warioba katika Taifa hili haifai kubezwa hata kidogo uwe na heshima.
Hana njaa yoyote kama uliyokua nayo as he is enjoying retirement benefits kama pm mwingi yoyote! Ambazo wewe na ukoo wako hauwezi kuwa Nazo.

Kama unamchukia yeye personal let it be otherwiise jibu hoja zake na zile za Dr Bashiru.

Ogopa Taifa likiwa na wajinga wengi wanaweza kuchagua RAIS!
 
CCM ni chama cha kidemokrasia ndio maana watu wanatofautiana na mwisho wanaelewana.
Unatueleza hili leo kwa sababu yupo SSH!Nyakati zile saa hizi mngekua mnarushwa vichura huku mmevaa misuli mitupu.[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
"kuna wastaafu wanawashwawashwa"... Alsikika Kiongozi mmoja kutoka ktk kiti cha kuongozea malaika.
 
Ukitafakari kwa kina aina ya viongozi tulio nao ndio tunapojua dhahiri taifa kama taifa kufikia maendeleo halisi ni ngumu sana .

Kama wengi wa viongozi wetu wanatoa maoni yao juu ya maoni ya mtuwingine kwa namna tunavyo ona tukubali tu kwamba sisi wananchi wa taifa hili ni miongoni mwa wenye kupata hasara.

Mtu ametoa maoni ya kawaida kabisa kwa akili za walio wengi na mitazamo ya walio wengi lakini wanatokea madaktari wa falsafa ambao ndio hujulikana kama wasomi wa hali ya juu wanakosoa maoni ya mtu na si kwa maslahi ya taifa bali kwa kikundi chao na kiongozi wao!

Sisi kama wananchi wa kawaida tunaangalia kwa umakini mtanange huu, lakini kama tungejaliwa kujua hakuna wakati mzuri sisi wananchi tunaopata kama wakati wa kupiga kura.

Bahati mbaya sana hatutumii wakati huo kwa maslahi mapana ya taifa letu na sisi kwa ujumla , badala yake ni kulia kulalamika na kulaumu miaka na miaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…