Jaji Warioba: Miaka yote watu wanaelewa kujaza fomu, lakini 2020 ghafla hawajui. Siasa inataka kuingia kwenye Dini

Jaji Warioba: Miaka yote watu wanaelewa kujaza fomu, lakini 2020 ghafla hawajui. Siasa inataka kuingia kwenye Dini

Nchi ina wanasiasa wanafiki sana...
 
Nmefurahi kusikia Kinana anakiri kuwa Haki na Demokrasia havikuwepo, na ndio mwanzo mzuri kupata chaguzi zenye matakwa ya wananchi Ili kuleta viongozi wenye tija kwenye maendeleo yao
Uchaguzi mkuu 2015 Kinana alikuwa katibu mkuu ccm. Demokrasia na haki vilikuwepo wakati huo?!
 
Huko mahakamani si ndio wako akina jaji Tiganga? Au unadhani hao mahakama walikuwa hawajui nguvu ya lile kundi la watu wasiojulikana wa Magu?
Kama aliweza kumtoa CAG mpenda haki na anayechukia ufisadi kinyume cha sheria, basi wale majaji angewafuta dakika sifuri tu, and wahuni wake wangeanza kuwatukana kuwa siyo wazalendo/wapinga maendeleo
 
Mtu muovu sana alipita nchi hii..Diallo alisema ni miaka 5 iliyopita ni doa jeusi katika history ya nchi yetu
Chini ya utawala wa Hayati Magufuli, nchi ilikuwa kwenye laana kubwa. Ni kipindi ambacho haki za watu zilikanyagwa, na nchi ikafanywa kuwa jungle, ambapo fisi, mbweha na dubu waliwashambulia kondoo, bila ya kupatikana wa kuzuia uhalifu.
 
Chini ya utawala wa Hayati Magufuli, nchi ilikuwa kwenye laana kubwa. Ni kipindi ambacho haki za watu zilikanyagwa, na nchi ikafanywa kuwa jungle, ambapo fisi, mbweha na dubu waliwashambulia kondoo, bila ya kupatikana wa kuzuia uhalifu.
Sidhani kama hilo kosa litarudiwa tena, hawa watu wasiojua misingi ya vyama vyao ni hatari sana kuwapa madaraka makubwa! Naanza kumuelewa Mbowe now kwa nini bado anasita kuachia uenyekiti, kuna watu unaweza kuwaachia madaraka na wakavuruga mambo yote mliyoyajenga kama nchi/chama
 
Kwanini hawakuenda mahakamani?

Kubaki unalialia umeonewa wakati hakuna kesi hata moja mahakamani ya kupinga uchaguzi ni upuuzi na kupoteza muda.
Mahakama ipi kwa muijibu wa katiba ya JMT inauwezo wa kuchunguza shughuli za Tume ya Taifa ya Uchaguzi. Kesi unazozisikiaga ni kati ya mgombea dhidi ya mgombea mwenzie na si watendaji wa Tume.
 
Zaidi ya Nusu za kata nchi nzima CCM ilipita bila kupingwa sasa mahakamani unaenda kufungua kesi Gani wakati hata uchaguzi haukufanyika?

NEC watu walipeleka rufaa zilikaa zaidi ya wiki 2 mpaka 3 huku CCM ilishaanza kampeni ghafla unaambiwa rufaa Yako imefeli!!! Then what?? Hiyo kesi mpaka iishe si inabaki wiki moja kwenda uchaguzi!!!

Nmefurahi kusikia Kinana anakiri kuwa Haki na Demokrasia havikuwepo, na ndio mwanzo mzuri kupata chaguzi zenye matakwa ya wananchi Ili kuleta viongozi wenye tija kwenye maendeleo yao
Huyo Kinana hayo ameona hayakuwepo 2020 tu?

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
 
Anaonekana mlevi hata kwenye picha official ya kazini!!
Siku Mahera alipoteuliwa kuwa mkurugenzi Arusha then Nec nilishangaa sana maana tumepiga naye sana ulabu akiwa principal AIM TANZANIA, Tukiwa na totoz pembeni
 
Jaji Warioba akichangia kwenye mkutano wa TCD leo Dodoma, amenena haya

Miaka yote watu wanaelewa na wanajaza fomu vizuri lakini Mwaka 2020, ghafla watu hawajui kujaza fomu (wanaenguliwa). Hapa lazima kuna namna

Msitazame Wajumbe wa Tume pekee, angalieni Mfumo mzima wa Uchaguzi. Wizi wa kura unaanzia mbali. Unaanzia kwenye Kuandikisha wapiga kura, wakati wa kupiga kura na kutangaza matokeo

Siasa inataka kuingia kwenye dini, zamani viongozi tulikuwa tunakwenda kwenye vyumba vya ibada kama waumini, unasikiliza neno la Mungu. Siku hizi viongozi wakienda wanaombwa kutoa salamu za kisiasa, hii inaweza iingiza siasa katika dini tukapata matatizo

Vyama vingi vimekuwa kama makabila, vinaanza kugawa wananchi. Wananchi walikuwa kama jumuiya lakini siku hizi mambo mengi ya kijamii tunaingiza siasa, mfano msiba ni wa jamii lakini baadhi ya misiba unakuta sare za vyama,"

Katika vyama jumuiya zetu nazo zinakuwa kama za uhasama, badala ya kutuleta pamoja. Hali tuliyo nayo sasa utamaduni umetikiswa kidogo na tunapozungumzia maridhiano, nia yake kuturudisha kwenye utamaduni tuliokuwa nao


Viongozi wa kisiasa wangehubiri amani kama walivyofanya viongozi wa dini miaka michache iliyopita, nchi isingekuwa na malalamiko yanayolalamikiwa hivi sasa “kama wangetenda kama viongozi wa dini, nadhani matatizo haya tunayozungumza tusingekuwa nayo.


Mawazo ya Zitto yako kwenye kupiga kura tu. Kama kipofu haoni.
 
Back
Top Bottom