Pre GE2025 Jaji Warioba: Tusipochukua hatua, uchaguzi mkuu utakuwa kama huu wa Serikali za Mitaa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Mzee wetu, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Jaji Joseph Sinde Warioba, Nampenda na kumkumbali sana sana,

Maelezo, maoni, tahadhari nk nk alizozitoa mzee wangu je Jukwaa alilotumia ni sahihi kiasi gani...
Mungu hutumia njia nyingi kufikisha ujumbe hata ndege wa porini hutumika kumwepusha mwanadamu asiliwe na simba, chui au nyoka. Hivyo Mzee Warioba yuko sahihi 100% mambo ya siri ndiyo yametufikisha kwenye ujinga na upumbavu huu tunaoishi nao.
 
Mzalendo halisi. Hawa ndio inabidi tuwape nchi. Wanauchungu na nchi sio wapigaji wa sasa.
 
Mzee wetu, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Jaji Joseph Sinde Warioba, Nampenda na kumkumbali sana sana,

Maelezo, maoni, tahadhari nk nk alizozitoa mzee wangu je Jukwaa alilotumia ni sahihi kiasi gani...
Mzee yuko sahihi. Tukumbuke, hata Mwl. Nyerere aliwahi kufanya hivyo kipindi fulani. Japo kwa nyadhifa zao kinchi ni tofauti, lakini siyo vibaya kama Mzee mstaafu kutoa maoni yako.
 
Una lalamikia kitu usicho kijuwa.

Hilo "...baraza la usalama wa taifa", wewe ulilisikia wapi na kujuwa kuwa wazee wastaafu wamo kwenye baraza la usalama wa taifa?

Wewe huoni mzee wa watu anahangaika hovyo; kwa sababu hata mahali pa kusemea asikilizwe hana?
Huyu hadi kalambishwa makofi na Bashite; halafu unadhani Samia anao muda na mzee kama huyu kumsikiliza?

Wewe sema tu kwamba ni bahati yake tu, kuwa hata hizo hadhara za kuitisha waandishi wa habari na kuzungumza bado anavumiliwa tu; wakiona anasababisha watu kuelewa anayo yazungumzia watamzima mara moja.

Sasa hivi wame mwacha tu, kwa kumpuuza.
 
Ukweli ndiyo huo.
 
Hatua zichukuliwa haraka kuweka utaratibu wa kuheshimu maamuzi ya wananchi kwenye sanduku la kura.
 
Akiwa Ikungi Singida Makamu mwenyekiti wa Chadema Mh Tundu Lisu alisema 2019 hayati Magufuli hakuuwa Mtu hata Mmoja alifutafuta uchaguzi tu

Leo Jaji Warioba anasema uchaguzi wa 2024 unafanana na ule wa 2019

Tunaendelea kukusanya maoni

Mlale unono 😀
 
Uchaguzi mkuu utakuwa mara 10000 ya balaaa ya serikali ya mtaa....
Tutegemeee maumivu zaidi

Ova
wapinzani washiriki kikamilifu wasisuse, kila alipo mgombea wa ccm na wa upinzani awepo ili tuone uchafuzi huo, wapinzani pia wajiandae kisaikolojia kukosa na kupata
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…