Mzee wetu, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Jaji Joseph Sinde Warioba, Nampenda na kumkumbali sana sana,
Maelezo, maoni, tahadhari nk nk alizozitoa mzee wangu je Jukwaa alilotumia ni sahihi kiasi gani?
Je Mzee wangu kwani si member wa Baraza la usalama wa taifa?
Je kama ni member wa Baraza la usalama wa taifa wao kama wazee wastaafu waliolitumikia hili taifa kwa jasho damu na kwa nguvu zao zote na baadaye kutengeneza viongozi hata hawa wa sasa Wameshindwa je kukaa wao kwanza wastaafu wa hilo Baraza, kisha yale ambayo wanaona watawala hawako sawa wakutane ana kwa ana na Rais, Waziri mkuu, Mkurugenzi mkuu wa usalama wa taifa, CDF na IGP waambie ukweli na hali halisi anavyoona wao,
Je hii ya kutoka hadharani tena mstaafu mmoja tu rais na watu wake watafanyia kazi maneno ya mzee wetu?