Pre GE2025 Jaji Warioba: Tusipochukua hatua, uchaguzi mkuu utakuwa kama huu wa Serikali za Mitaa

Pre GE2025 Jaji Warioba: Tusipochukua hatua, uchaguzi mkuu utakuwa kama huu wa Serikali za Mitaa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
mwendazake aliwatengenezea barabara na sasa wanafatisha tu...chadema muingie msituni tu ha ha ha 😁😆
 
Mkuu, una nini na huyu Mzee wetu?
..ni mstaafu kwenye chama kinachoharibu uchaguzi na mjumbe kwenye vikao muhim ya chama chake, ni mstaafu wa serikali inayotumia vibaya vyombo ya dola na anashiriki vikao kuongelea mambo ya nchi..ajabu HAJAWAHI kuita aliowaita leo ili atoe angalizo na msimamo wake tabla mambo hayajaharibika, kwa hiyo anasubiri uchaguzi uvurugwe, watu wafe..ndio aongee aliyosema leo, je watu waliouawa watarudi? Uchaguzi ulioharibiwa utarudiwa? Km sio unafiki ni nini hiki anachofanya???
 
  • Thanks
Reactions: UCD
Mzee Warioba anatumika kurejesha Imani ya akina Mbowe warudintena kwenye meza ya maridhiano, wapotezewe muda na Kisha warudi kwa wafuasi wao wawahamasishe kujiandikisha ili mwisho wa siku Dona kantriz waone Kuna demokrasia na watoke misaada. Lkn 2025 uchaguzi up utachafuliwa kama kawaida.
 
Jaji Warioba akiongea na waandishi wa habari leo Desemba 4 amesema haya

Ukiona mjadala wote uliofanywa tangu 2019 mpaka sasa, na imani iliyokuwapo kwamba uchaguzi wa mwaka huu (2024) hautofanana na ule wa mwaka 2019, lakini matokeo yake ni vilevile. Uchaguzi wa mwaka kesho (2025), kama hatutachukua hatua, utakuwa kama huu uliopita (Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 27, 2024).

Tume itakayosimamia uchaguzi wa mwaka kesho, ni ileile iliyosimamia uchaguzi wa mwaka 2020, maana sioni dalili pamoja na sheria kupitishwa kwamba kuwe na tume tofauti, sioni dalili kama tume hiyo itaanzishwa kabla ya uchaguzi, kwahiyo ni tume hiihii ndiyo itakayoendesha uchaguzi wa mwaka kesho.

Watakaosimamia ni walewale ambao wapo chini ya TAMISEMI, uongozi wa kisiasa ni uleule ndani ya TAMISEMI, hawakusikiliza yote yaliyosemwa katika kipindi chote wakarudia ya zamani, hata mwaka kesho watafanya vilevile, tutakuta watu wanaenguliwa wengi tu, tutakuta kura za bandia na mengineyo.
Huyu ana hasira na serikali kwa kuwa familia yake haijapewa nafasi
 
Pole poleee kilaa mmoja ataongea Kwa wakatii.....

Tafadhali tusikilizaneeee
FB_IMG_1733322947733.jpg
 
Akiwa Ikungi Singida Makamu mwenyekiti wa Chadema Mh Tundu Lisu alisema 2019 hayati Magufuli hakuuwa Mtu hata Mmoja alifutafuta uchaguzi tu

Leo Jaji Warioba anasema uchaguzi wa 2024 unafanana na ule wa 2019

Tunaendelea kukusanya maoni

Mlale unono 😀
Read more on comparison studies and analysis
 
Mbo
We punguani kichaa, hapa siyo mahali pako. Kwenye majalala huko ambako huwa unaokota mabaki ya vyakula, bakia huko huko. Hapa ni kwa wenye akili timamau pekee.
Mbona matusi kwani ukijibu kwa hoja kuna shida yoyote!!
 
Ndiyo kuna tofauti. Maana Jiwe aliiba uchaguzi tu, lkn huyu bibi katiba uchaguzi na kuuwa watu.
 
Ccm walivyo wapumbavu hawafatagi ushauri wa watu wa maana kama hawa
 
Huyu mzee katumwa kuongea haya, ili akina Mbowe warudi kwenye udanganyifu wa maridhiano.

Huyu mzee ana nafasi ya kuongea na wenye mamlaka ili kuwataka watende anayoyatamani na siyo kulalamika.
 
Mzee kaonya Serikali kutumia jeshi la Police kuisaidia CCM - kasema ni HATARI MNO kwa taifa.

Mwenye akili kasikia.
 
mzee kasema ukweli katika uhalisia uchaguzi sio wa haki
 
Back
Top Bottom