Pre GE2025 Jaji Warioba: Tusipochukua hatua, uchaguzi mkuu utakuwa kama huu wa Serikali za Mitaa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Huyu mzee katumwa kuongea haya, ili akina Mbowe warudi kwenye udanganyifu wa maridhiano.

Huyu mzee ana nafasi ya kuongea na wenye mamlaka ili kuwataka watende anayoyatamani na siyo kulalamika.
Hamna mtu ataridi kwenye mazumgumzo yasiyo na tija.

Mazungumzo ambayo wapinzania wanaweza kurudi mezani labda yawe na nguvu ya kisheria.
 
Ameiongelea ile Kauli...
"Kula kwa urefu wa Kamba"...
😳😳
Mzee kajikoki huyu
 
Huyu mzee katumwa kuongea haya, ili akina Mbowe warudi kwenye udanganyifu wa maridhiano.

Huyu mzee ana nafasi ya kuongea na wenye mamlaka ili kuwataka watende anayoyatamani na siyo kulalamika.
Labda umemfahamu leo mzee Warioba
 
CCM sababu wamekosa mshipa wa aibu watasema mzee kaanza kukosa kumbukumbu - umri.
Ila kwa kweli JAJI kwa hoja zake zote kaliponya Taifa, Mzee yupo vizuri saana- ukiwa na wazee walau 50 tu wa namna hii katika nchi basi Serikali yako haiyumbi.
 
Msimamo wa kinafiki. Trust me anatumika.

Mbona alikuwa waziri mkuu na hakuibadili katiba hii mbovu? Kumbuka yeye ni mwanasheria, iweje atake mabadiliko akiwa nje ya ofisi?
Haujui mchango wake kwenye upatikanaji wa katiba mpya?
 
Nimeandika msg sasa hivi lakini imepotea. Inabidi niandike msg nyingine,kivingine.
Yaani Jaji Warioba ameongea kwa sababu wako kimya kuhusu swala.
Kwa hiyo anataka mjadala uendelee.
Ukimpinga,ndio anachotaka. Let us talk about this.
Lakini ukianza kutukama na kusema utamwita Makonda amshike shati( tena) that is disrespectful.
Hata hivyo mimi sikusikiliza Jaji Warioba amesema nini.
I am just vaguely aware kwamba analalamika kidogo kuhusu utendaji kazi wa TISS na Polisi katika Uchaguzi wa wiki iliyopita.
Polisi ni lazima watakuwa cautious.
Mtu katekwa,katekwa na nani.?
Labda katekwa na KMKM.
Kwa hiyo uchunguzi wa jambo lolote lazima uwe cautious.
 
Msimamo wa kinafiki. Trust me anatumika.

Mbona alikuwa waziri mkuu na hakuibadili katiba hii mbovu? Kumbuka yeye ni mwanasheria, iweje atake mabadiliko akiwa nje ya ofisi?
kama hajafanya hayo akiwa ofisini basi Hana haki ya kuyasemea hayo?
 
Angesema haya katika baraza la usalama wa taifa wewe ungesikia maoni yake? Ametumia haki yake ya kikatiba kutoa ,aoni yake. Anayeyapuuza ni kati ya wale wanaojali njaa zao kuliko taifa. Ila mataifa mengi ya ki Africa yamejikuta yakiingia katika machafuko kwa kupuuzia sauti kama hizi. Watu wengine wanamanung`uniko kuhusu chaguzi zetu.
 
Mzee wetu Joseph Butiku mwenyekiti wa kigonda cha Mwalimu Nyerere alipiga kelele sana kuhusu swala la Dp World kupewa Bandari yetu, na mimi nakafarijika kuona yupo upande wa wengi tuliokuwa haturidhii DPW kupewa,

je Samia alimsikiliza?
 
So hatakiwi kuongea? Ukute hana hata nafasi ya kupeleka mawazo Moja Kwa Moja sehemu huska ,

uchawa upo kwenye siasa Kwa maslahi binafsi sio rahisi kisikilizwa. Ametoa tahadhari juu ya kinachoendelea na amerejelea yaliyotokea Zanzibar.

Fair competition haikuwepo ni chuki tu inazidi kutengenezwa siku Hadi siku, na wengine wanafurahia Kwa sababu ni chama chao labda au Kwa sababu zao binafsi nyingine,

Si jambo la kufarahia hata kidogo. Mikakati pamoja na maelekezo ya kufanya dosari hizi inawezekana ilianza tokea wakati wa kuteua waandikishaji kisha kuteua wasimamizi wa uchaguzi.
Yakinyamaziwa haya mapema kunahatari zaidi huko mbeleni .
 
Msimamo wa kinafiki. Trust me anatumika.

Mbona alikuwa waziri mkuu na hakuibadili katiba hii mbovu? Kumbuka yeye ni mwanasheria, iweje atake mabadiliko akiwa nje ya ofisi?
Kila jambo Kwa wakati wake ndugu, kwani wewe huoni yanayoendelea?Hii kasumba ya kupuuzia watu wengine inatokea wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…