PostGE2025 Jaji Warioba: Waliouawa Oktoba 29, 2025 ni wengi kuliko waliouawa kwenye Vita ya Kagera

PostGE2025 Jaji Warioba: Waliouawa Oktoba 29, 2025 ni wengi kuliko waliouawa kwenye Vita ya Kagera

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections
Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba “Waliouwawa tarehe 29 ni wengi kuliko waliouawa kwenye Vita ya Tanzania na Kagera"


Kwenye mahojiano na Jamhuri TV, Jaji Mstaafu Joseph Sinde Warioba amesema kuwa ukiangalia Vita ya Kagera, vijana wetu wengi waliuawa na adui. Hata hivyo, ukilinganisha na takwimu zinazozungumziwa sasa, idadi ya waliokufa ni kubwa zaidi kuliko ile ya vita. Tofauti ni kwamba, wakati ule tuliuawa na adui, lakini sasa tunajiua sisi wenyewe.

Ameongeza kwa kuhoji miongoni mwa polisi, hakuna hata mmoja ambaye ndugu yake ameuawa? Vivyo hivyo kwa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na viongozi—hakuna hata mmoja ambaye ndugu yake ameuawa?.

Kuhusu Jeshi, Jaji Warioba amesema kuwa bado msimamo wake ni kutolihusisha jeshi na siasa. Ameeleza kuwa msimamo huo aliueleza alipotoa kauli yake mwezi Desemba 2024, baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Baba kanyooka hakuna konakona....walidhani kupiga naye picha itabadil msimamo....big No
 
Wapuuzi wanasema tuko kwenye vita uchumi vya madini adimu na uranium kwa hiyo watu wachapwe risasi tu, Inasikitisha sana.
Mwigulu sijui anaona Watanzania hawana akili ?
Eti watu wanaweka picha za Darful Sudan...wakati zile picha hata ukiangalia mazingira ni hapa Tanzania...
Mwigulu nimekuja kujua hayupo timamu
 
Baba kanyooka hakuna konakona....walidhani kupiga naye picha itabadil msimamo....big No
Pozi la ile picha lilionyesha kuwa maongezi hayakwenda smoothly, mzee kagoma kupanda mtumbwi wa vibwengo. She is trying so hard to manipulate everyone on board lakini wale principled wanamkatalia.
Warioba back then alivyokuwa PM alitofautiana na Mzee Ruksa suala la Wahindi kuwa wanaingia hovyohovyo ikulu Magogoni wakatofautiana sana kwenye hilo mpaka akaachia ngazi.
 
Kwenye mahojiano na Jamhuri TV, Jaji Mstaafu Joseph Warioba amesema kwenye Vita ya Kagera, vijana wengi waliuawa na adui. Aidha, ukilinganisha na takwimu zinazozungumziwa sasa, idadi ya waliokufa ni kubwa zaidi kuliko ile ya vita. Tofauti ni kwamba, wakati ule tuliuawa na adui, lakini sasa tunajiua sisi wenyewe.


Ameongeza kwa kuhoji miongoni mwa polisi, hakuna hata mmoja ambaye ndugu yake ameuawa? Vivyo hivyo kwa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na viongozi—hakuna hata mmoja ambaye ndugu yake ameuawa?.

Kuhusu Jeshi, Jaji Warioba amesema kuwa bado msimamo wake ni kutolihusisha jeshi na siasa. Ameeleza kuwa msimamo huo aliueleza alipotoa kauli yake mwezi Desemba 2024, baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Ndiye mzee pekee tuliyebaki naye. All else ni chawa pro max!
 
Kipindi Cha vita vya kagera inakadiliwa vijana milioni mbili waliuawa.kwa maana vijana waliouawa MO29 wengi zaidi ya hao
 
Kwakweli nimefarijika sana. Wananchi walisubiri muda mrefu kiongozi wa kusema haya! Only Father Kitima ndio aligeuka kiongozi wa umma walau sasa Mzee Warioba amesema tunayotaka kusikia.
Huyu kiongozi wa nini kwa sasa? Hesabu aliipata wapi? Akibanwa athibitishwe ataweza?
 
Kwenye mahojiano na Jamhuri TV, Jaji Mstaafu Joseph Warioba amesema kwenye Vita ya Kagera, vijana wengi waliuawa na adui. Aidha, ukilinganisha na takwimu zinazozungumziwa sasa, idadi ya waliokufa ni kubwa zaidi kuliko ile ya vita. Tofauti ni kwamba, wakati ule tuliuawa na adui, lakini sasa tunajiua sisi wenyewe.


Ameongeza kwa kuhoji miongoni mwa polisi, hakuna hata mmoja ambaye ndugu yake ameuawa? Vivyo hivyo kwa vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na viongozi—hakuna hata mmoja ambaye ndugu yake ameuawa?.

Kuhusu Jeshi, Jaji Warioba amesema kuwa bado msimamo wake ni kutolihusisha jeshi na siasa. Ameeleza kuwa msimamo huo aliueleza alipotoa kauli yake mwezi Desemba 2024, baada ya uchaguzi wa serikali za mitaa.

Nimemsikiliza mzee, nimeangalia sura yake na anachoongea na kuona bila shaka yoyote kuwa, he's very genuine na kweli kuna shida kubwa huko serikalini....

Kwa kauli hii ya Jaji Joseph Warioba, amepingana na kuwazodoa rasmi kina Mwigulu Nchemba wanaotumia rasrimali nyingi za fedha kuzungukazunguka huku na huko kuhahaa na kulaghai watu kwa uongo huku wakificha tatizo halisi....

Bila Samia na genge lake la kihuni kukiri makosa yao waziwazi na kuomba msamaha/toba kwa Mungu na sisi wananchi, kila wanalofanya sasa watakuwa wanajilisha upepo tu, kimbunga cha malipo ya mauaji na dhuluma lazima kiwazoe...!
 
Kipindi Cha vita vya kagera inakadiliwa vijana milioni mbili waliuawa.kwa maana vijana waliouawa MO29 wengi zaidi ya hao
Mkuu, unajua millioni mbili ?
Rwanda walinyooshana vibaya sana...na walifika laki nane na kitu...
Ziwa Victoria Samaki wakivuliwa walikuwa na vidole vya binadamu..watu wakaogopa kuvua Samaki....
Maji ya Mto Kagera mpaka harufu ilibadilika...
 
Hii kaitoa baada ya kutoka ikulu, inaonekana amewagomea kununulika nadhani hapa asali waliyomuandalia labda watailamba wenyewe.

Samia anajaribu kukupa asali kwanza utetea genge lake. Amemwita Warioba akakataa kulamba asali. Akamtuma Mwigulu amwite Fr Kitima kumlambisha asali, Fr Kitima akakataa.

Baada ya hapo wakaanza kampeni chafu, kumchafua Fr Kitima na TEC. Wamepanga kumteka, kumtesa na kumuua. Ameshindwa kwenda kwenye msiba wa Mhagama kwa kuhofia maisha yake.

Mzee Warioba, aongeze ulinzi, kampeni chafu zitaanzishwa na mashehe wa kihuni na machawa wa genge la Samia, kabla ya kujaribu kumteka na kumuua.
 
Back
Top Bottom