Jaji Werema: Dai la Katiba Mpya lisibezwe

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Jana niliweka uzi hapa nikasema huenda Mama swuala la Katiba analiunga mkono ila inabidi atumie watu nje ya chama chake kuliibua kwasababu wenzake ndani ya chama hawalitaki.

Nikaongeza ni suala la muda tu makundi mengine yataibuka na kuunga mkono agenda ya Katiba Mpya.

Huyu keshaanza, wengine watafuata soon na Mama ataunga mkono hiyo agenda.

She is a silent killer.

Your browser is not able to display this video.
 
Naamin CCM wanaitaka zaidi katiba mpya kuliko upinzani, kinachofanyika sasa ni kutafuta sababu ya kuibadilisha katiba ili hata wakifanya mafekeche yao waseme tu kuwa wao walikua hawatak nyinyi ndio mlioitaka.
 
JAJI FREDRICK WEREMA AZUNGUMZIA KATIBA PENDEKEZWA NA KUSISITIZA NI SUALA LA MUAFAKA NA INAWEZEKANA
Awamu ya tano madaraka ya urais yalitumika vibaya na hii ni mbaya haiwezekani wananchi wote waufyate mkia na hili ndiyo naona ni dai kubwa la wananchi kuwa taasisi ya urais na rais wadhibitiwe, hili mimi Fredrick Werema naliunga mkono.


Ataja CV yake ndefu kutuelezea uzoefu na weledi wake ili akiwa anatoa hoja zake tujue ametumia angle zipi na kujijengea authority ya anachotueleza, hakika ni jambo zuri na sisi kama chombo makini cha JAMIIFORUMS, wanaJF tunampongeza Jaji Werema kwa hilo kutuweka sawa kuhusu weledi wake wa katiba na sheria.
Kutenganisha TANESCO

 
Na inashangaza kweli kwa mtu kama huyo kuyasema hayo anayoyasema.

Ina maana wakati wanapokuwa ndani akili zao huwa zimenyofolewa?

Mfano halisi ni Babudi Kalamaganda, na yeye siku moja atatoka nje na kupiga mayowe:" Inatakiwa Kuwepo Katiba Mpya"

La ajabu hapo itakuwaumati utakaokuwa unashangilia mayowe hayo!
 
Wasomi na makundi yote mengine tujitokeze ili suala la katiba mpya lisiwe la kikundi fulani kama ambavyo CCM Lumumba wanataka kujimilikisha kwa niaba yetu sote Watanzania.
 
Toka maktaba : Nondo za Jaji Werema

21 February 2014

Dar es Salaam

Bunge la #Katiba 'haliwezi kuunda serikali moja'


Mwanasheria Mkuu Jaji Frederick Werema akumbushia kuwa hatuna masultani wala machifu.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amewataka wajumbe wa bunge maalum la katiba kutambua kuwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inawazuia wao kuunda mfumo wa serikali moja , kama inavyodaiwa na baadhi ya watu. Haiwezekani Serikali moja maana lazima serikali ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar lazima iwepo. Tundu Lissu na Zitto Kabwe nao watoa angalizo nyeti kabisa.

Jaji Werema amewasisitiza wajumbe wenzake, kutambua kuwa wanayo haki ya kuongeza kitu kwenye rasimu ya katiba, lakini hawana uwezo wa kuondoa chochote kwani rasimu hiyo imekusanya maoni ya wananchi.
Source : mwananchi digital
 
Angekuwa madarakani angesema hivyo?
 
Healer not killer

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
kimuingiacho mtu siyo najisi bali kimtokacho - Werema
 
"Lazima tujue kwanini watu wanadai Katiba Mpya.Tumepitia wakati mgumu sana katika miaka mitano iliyopita ambapo Madaraka makubwa ya Rais ya kufanya vitu bila kuhojiwa na bila kuwajibika yalionekana.Mimi Naona hoja katika hilo."Jaji Frederick Werema, AG Mstaafu

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…