Jaji Werema: Dai la Katiba Mpya lisibezwe

Jaji Werema: Dai la Katiba Mpya lisibezwe

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Jana niliweka uzi hapa nikasema huenda Mama swuala la Katiba analiunga mkono ila inabidi atumie watu nje ya chama chake kuliibua kwasababu wenzake ndani ya chama hawalitaki.

Nikaongeza ni suala la muda tu makundi mengine yataibuka na kuunga mkono agenda ya Katiba Mpya.

Huyu keshaanza, wengine watafuata soon na Mama ataunga mkono hiyo agenda.

She is a silent killer.

Naamin CCM wanaitaka zaidi katiba mpya kuliko upinzani, kinachofanyika sasa ni kutafuta sababu ya kuibadilisha katiba ili hata wakifanya mafekeche yao waseme tu kuwa wao walikua hawatak nyinyi ndio mlioitaka.
 
JAJI FREDRICK WEREMA AZUNGUMZIA KATIBA PENDEKEZWA NA KUSISITIZA NI SUALA LA MUAFAKA NA INAWEZEKANA
Awamu ya tano madaraka ya urais yalitumika vibaya na hii ni mbaya haiwezekani wananchi wote waufyate mkia na hili ndiyo naona ni dai kubwa la wananchi kuwa taasisi ya urais na rais wadhibitiwe, hili mimi Fredrick Werema naliunga mkono.

TUMAINI UNIVERSITY DAR ES SALAAM COLLEGE.

"TUSIBEZE MJADALA WA KATIBA MPYA, TUANGALIE NI VITU GANI VIONGEZWE NA VIPUNGUZWE" - MWEREMA

4 Jul 2021
"TUSIBEZE MJADALA WA KATIBA MPYA, TUANGALIE NI VITU GANI VIONGEZWE NA VIPUNGUZWE" - MWEREMA Serikali ya wanafunzi chuo kikuu cha tumaini tawi la dar es salaam (Tudarco) imefanya kongamano la kubadilishana uzoefu kwa wanafunzi wanaosoma masomo ya sheria kwa kuwakutanisha wanafunzi hao na mawakili pamoja na wanasheria wasomi katika fani hiyo akiwemo mwanasheria mkuu mstaafu wa serikali ya tanzania jaji fredrick werema. Kupitia kongamano hilo, wanafunzi wameelezwa uhalisia na changamoto watakazo kutananazo katika mazingira ya kazi ambapo wamesisitizwa kutenda haki katika kazi zao. Aidha, kongamano hilo limetumika kujadili elimu ya sheria na jinsi inavyoweza kuathiri wanafunzi wanapokuwa vyuoni.

Ataja CV yake ndefu kutuelezea uzoefu na weledi wake ili akiwa anatoa hoja zake tujue ametumia angle zipi na kujijengea authority ya anachotueleza, hakika ni jambo zuri na sisi kama chombo makini cha JAMIIFORUMS, wanaJF tunampongeza Jaji Werema kwa hilo kutuweka sawa kuhusu weledi wake wa katiba na sheria.
Kutenganisha TANESCO

Jaji Werema kwa kirefu kabisa miaka 32 afanya kazi ya umma ktk sekta ya sheria serikalini, Wakili daraja 3 Iringa ,mkurugenzi katiba & sheria wizara ya sheria, Jaji Mahakama kuu kanda Iringa, mwanasheria mkuu serikali ya Muungano wa Tanzania, akiwa Nambia niliteuliwa na marais 14 kuwa Jaji wa SADC , niliacha ujaji wa SADC baada ya kuteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali Tanzania , baada ya kashfa ya ESCROW 2014 nilijiuzulu toka serikalini baada ya baraza la mawaziri kukosa mwelekeo na kumshauri Rais nijiuzulu, JK alikataa lakini nilimuelezea kwa hoja hatimaye akakubali nijiuzulu. Elimu : shule Kwiru, Songea Boys O LEVEL , PCB physics nilipata F, nikabadilisha kombi kwenda Kiingereza HGL , nimesoma UDSM, masters USA, pia kozi ktk nchi za ITALY , BOLIVIA AUSTRALIA CHUO CHA POLISI, MICROFINANCE , JAMAICA, ARGENTINA, UNITED KINGDOM , CHILE, URUGUAY
 
Na inashangaza kweli kwa mtu kama huyo kuyasema hayo anayoyasema.

Ina maana wakati wanapokuwa ndani akili zao huwa zimenyofolewa?

Mfano halisi ni Babudi Kalamaganda, na yeye siku moja atatoka nje na kupiga mayowe:" Inatakiwa Kuwepo Katiba Mpya"

La ajabu hapo itakuwaumati utakaokuwa unashangilia mayowe hayo!
 
Wasomi na makundi yote mengine tujitokeze ili suala la katiba mpya lisiwe la kikundi fulani kama ambavyo CCM Lumumba wanataka kujimilikisha kwa niaba yetu sote Watanzania.
 
Toka maktaba : Nondo za Jaji Werema

21 February 2014

Dar es Salaam

Bunge la #Katiba 'haliwezi kuunda serikali moja'

Mwanasheria Mkuu Jaji Frederick Werema akumbushia kuwa hatuna masultani wala machifu.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amewataka wajumbe wa bunge maalum la katiba kutambua kuwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inawazuia wao kuunda mfumo wa serikali moja , kama inavyodaiwa na baadhi ya watu. Haiwezekani Serikali moja maana lazima serikali ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar lazima iwepo. Tundu Lissu na Zitto Kabwe nao watoa angalizo nyeti kabisa.

Jaji Werema amewasisitiza wajumbe wenzake, kutambua kuwa wanayo haki ya kuongeza kitu kwenye rasimu ya katiba, lakini hawana uwezo wa kuondoa chochote kwani rasimu hiyo imekusanya maoni ya wananchi.
Source : mwananchi digital
 
Jana niliweka uzi hapa nikasema huenda Mama swuala la Katiba analiunga mkono ila inabidi atumie watu nje ya chama chake kuliibua kwasababu wenzake ndani ya chama hawalitaki.

Nikaongeza ni suala la muda tu makundi mengine yataibuka na kuunga mkono agenda ya Katiba Mpya.

Huyu keshaanza, wengine watafuata soon na Mama ataunga mkono hiyo agenda.

She is a silent killer.

Angekuwa madarakani angesema hivyo?
 
Healer not killer

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Toka maktaba : Nondo za Jaji Werema

21 February 2014

Dar es Salaam

Bunge la #Katiba 'haliwezi kuunda serikali moja'

Mwanasheria Mkuu Jaji Frederick Werema akumbushia kuwa hatuna masultani wala machifu.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amewataka wajumbe wa bunge maalum la katiba kutambua kuwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba inawazuia wao kuunda mfumo wa serikali moja , kama inavyodaiwa na baadhi ya watu. Haiwezekani Serikali moja maana lazima serikali ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar lazima iwepo. Tundu Lissu na Zitto Kabwe nao watoa angalizo nyeti kabisa.

Jaji Werema amewasisitiza wajumbe wenzake, kutambua kuwa wanayo haki ya kuongeza kitu kwenye rasimu ya katiba, lakini hawana uwezo wa kuondoa chochote kwani rasimu hiyo imekusanya maoni ya wananchi.
Source : mwananchi digital

kimuingiacho mtu siyo najisi bali kimtokacho - Werema
 
"Lazima tujue kwanini watu wanadai Katiba Mpya.Tumepitia wakati mgumu sana katika miaka mitano iliyopita ambapo Madaraka makubwa ya Rais ya kufanya vitu bila kuhojiwa na bila kuwajibika yalionekana.Mimi Naona hoja katika hilo."Jaji Frederick Werema, AG Mstaafu

Back
Top Bottom