Ramesses II
JF-Expert Member
- Sep 29, 2013
- 3,710
- 5,054
Ndio maana mataifa makubwa kama US huwa wanaidharau hii United Nations na mpaka kutishia kuacha kuchangia...
Sasa Kikwete masikini ya Mungu eti anatumwa aka negotiate na Taliban kurejesha watoto wa kike shule akiwa kama mwenyekiti wa Global Partnership for Education.
Mtu atakaepata mkanda wa mazungumzo ya Kikwete na Taliban atauza filamu ya comedy kali kuliko zote Afrika kama wasipom-behead mkutanoni.
Lakini lengo pana zaidi la GPE ni kupeleka fursa ya elimu bora kwa kila mtoto mnyonge duniani.
Huku nyumbani the Kikwetes of the third world wamefanya nini japo kujaribu kumpa mtoto mnyonge elimu wanayopata watoto wao binafsi? (Kumbuka hotuba ya JK kwenye mazishi ya JPM alivyoeleza bila aibu jinsi watoto wake wanavyosoma shule za academy).
Wanachaguliwa na UN kwa vigezo gani watu hawa hawa waliofeli katika mambo hayo hayo ya kuwapa nafuu wanyonge?
Acha kuwa mtumwa wa fikra. Pia kuwa mzalendo. Kwani Kikwete anaenda kupigana mieleka na Taliban au wanafanya mazungumzo? Pia Afganistan ni miongoni mwa nchi maskini duniani. Bado ipo third World country. Kwa maisha wanayoishi bora Tanzania mara 1000.
Mimi nina imani Mhe. Jakaya Kikwete analimaliza hilo jambo tena kiulaini kabisa.