Jakaya Kikwete atabaki kuwa Baba wa Demokrasia bora Tanzania kupita Marais wote waliopita na wajao

Haya yanayoendelea sasa alisababisha yeye
Haya yanayoendelea sasa alisababisha yeye 2015 kwenye mchakato wa kumpata mgombea Urais ndani ya CCM. Mtu wake aliposhindwa akachomekea jinsia kwenye Mgombea Mwenza. Mungu alipoamua kesi ndiyo haya yanayoendelea sasa.
 
Sio kweli mfumo na nature ndio sababu
 
Hiyo ni ndani ccm, mm nazunguzia kwenye vyama vya upinzani
Haya majanga ya ombwe la Uongozi wa Nchi yetu yalianzia 2015. Pia aliharibu mchakato wa Katiba mpya 2014 pamoja na kutumika gharama kubwa kwa Kodi za Watanzania. Aliendekeza maslahi binafsi yake na familia yake.
 
Haya majanga ya ombwe la Uongozi wa Nchi yetu yalianzia 2015. Pia aliharibu mchakato wa Katiba mpya 2014 pamoja na kutumika gharama kubwa kwa Kodi za Watanzania. Aliendekeza maslahi binafsi yake na familia yake.
Huyu ndio kipindi chake, wabunge wa upinzani bungeni wafike zaidi ya 70,
 
Of course, alikuwa na uvumilivu kwa kiasi fulani, hata akikosolewa. Lakini hakuwa mfano wa demokrasia. Ilikuwa wakati wa utawala wake ambapo wanafunzi wa vyuo vikuu walipigwa mabomu kugoma na kufanya maandamano. Wapinzani wakiandamana walikuwa wakipigwa sana. Kuanzia wakati huo sijasikia tena vyuo vikuu vikitoa kauli kupinga mambo mbalimbali yanayokiuka haki za binadamu na utawala wa sheria. Sehemu nyingine vyuo vikuu vinatetea haki za watu na kwa kutumia usomi wao kuwa sauti ya jamii. Lakini hapa kwetu vimekuwa as if havipo kabisa! Kuna kitabu nilikuwa nakisoma kwamba Mwalimu Julius Nyerere alikuwa anakwenda kwenye mijadala Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Alithamini elimu na mchango wa wasomi, lakini baada yake sioni Rais mwingine aliyekuwa na utamaduni huo wa kuthamini wasomi - kukaa nao, kubalishana nao mawazo, na kuwasikiliza. Ilikuwa pia wakati wa Kikwete ilipofanyika 'operesheni tokomeza ujangili' na mambo yaliyofanyika wakati huo ilikuwa balaa, kwa mujibu wa taarifa ya Kamati ya Bunge iliyoundwa kuchunguza malalamiko yaliyotokana na hiyo operesheni. Nilikuwa na ripoti nzima ya Kamati ya Bunge. It was appalling! Ila wakati huo Bunge lilikuwa moto Moto kweli kweli chini ya Samuel Sitta.
 
Kikwete is just a nice guy. Kama mtu wà kawaida.
Ila kusema eti ana demokrasia blablah.. Hamna demokrasia pale. Ni janja janja tu. Jamaa ni mjanja, ni mtoto wa mjini. Lakini ni mtu poa.

Ila mtu anaekuja na majina yake mfukoni (majina ya wagombea urais 2015) na kusema wengine wamekatwa na kamati ya maadili, huyo sio mwanademokrasia.
Kifupi huwezi ukawa mwanademokrasia ndani ya CCM. Demokrasia ya kweli ikiwepo, CCM itaondoka madarakani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…