Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Baadhi ya Watanzania hawana shukraniChaguo la Mungu haliwezi kufeli...Mungu atamuongoza huyu mama na nchi itafika mbali.
Sukuma gang[emoji870][emoji870][emoji870][emoji870][emoji870]
Kiongozi wa Gengetena huyu ndiyo akae kimya kabisa
Yeye ndio ameshika remote, usitegemee ajikosowe mwenyewe.
Cartel is back.
[emoji849]Ukarimu wote anaompa ndo leo asimsifie kweli, hawa wote wezi tu na huyo mpuuzi angejua kitaani anavyochukiwa laiti angekaa kimya. Hakuna anayeomba kifo ila huyu dalali akifa nitamtolea Mungu sadaka nono sana
Dah!Cartel gang tena?Yeye ndio ameshika remote, usitegemee ajikosowe mwenyewe.
Cartel is back.
Rais mstaafu J. Kikwete akihojiwa amesema nchi inakwenda vizuri chini ya Samia na changamoto mbalimbali zinaondolewa ikiwemo uongezaji wa huduma za dharura kwenye sekta ya afya...
Watanzania kwa Unafiki tumepitiliziza. Haiwezekani Haiwezekani kila Rais tuseme anafanya vizuri wakati wanafanya things differently.Rais mstaafu J. Kikwete akihojiwa amesema nchi inakwenda vizuri chini ya Samia na changamoto mbalimbali zinaondolewa ikiwemo uongezaji wa huduma za dharura kwenye sekta ya afya...
Si mnasema Nchi inaongozwa na Majaliwa ? Mbona JF siku hizi kila mtu mtabiriIko hivi kama hamjagundua,
- Vasco ameshika remote
- Prince ndiye anamwelekeza Vasco buttons za kubonyeza
- Na picha ndiyo hiyo mnayoona
Wameshakuwa na wanakuja tena, wasukuma ni sawa na maji, usipoyanywa utayaoga, au utamwagilia bustaniWanamatatizo kweli ukabika umewatawala Nyerer ana wawjua ndio maana alikua na nadharia ya kua nihatari Msukuma. Muhaya . Mchaga na Mnyakiusa kua Raisi
The cartel is scrambling for the wealth amassing while commending futility at stake, Tanzania is doomed hurling into the darkest moment ever experienced since the time memorialRais mstaafu J. Kikwete akihojiwa amesema nchi inakwenda vizuri chini ya Samia na changamoto mbalimbali zinaondolewa ikiwemo uongezaji wa huduma za dharura kwenye sekta ya afya.
Kikwete amesisitiza Samia analeta matumaini kwa watanzania kwa manufaa ya leo na kesho.
My take. Hii inaweza kuwa ni njia ya kumsafisha Samia na madhaifu yanayoonekana kwenye utawala wake, amejitokeza kubadilisha upepo hasa baada ya uteuzi wa juzi wa mawaziri na lile jina moja linalojirudia kila awamu.
----
Rais mstaafu wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete leo amemsifia Rais Samia Suluhu Hassan na kusema anaendesha Nchi vizuri na kwamba changamoto hazikosekani, Dr. Kikwete ameyasema haya leo wakati walipotembelea eneo kutakakojengwa mradi wa jengo la matibabu ya dharura kwenye Hospitali ya Wilaya ya Chalinze iliyopo Msoga ukiwa ni mradi unaofadhiliwa na ABBOTT FUND ya Marekani kwa gharama ya Bilioni 1.2.
Rais Mstaafu Kikwete amesema haya
"Tuendelee kumuunga mkono Rais wetu, anayo dhamana kubwa... sio kazi rahisi... ina mawimbi mengi na pengine kwenye kazi ile unapata siku za furaha ni kidogo kuliko siku za maudhi lakini cha umuhimu ni wewe kuwa na moyo wa uvumilivu na ustahimilivu, mpaka sasa anaendesha Nchi vizuri changamoto hazikosekani, nilisema wakati mmoja kwamba Babu yangu alinisumulia kwamba Nchi haipoi kama ugali, ugali ukichelewa kuula unapoa wote".
"Nchi siku zote haiwi hivyo, hapa pakipoa mara kunaibuka hili mara lile lakini katika yote hayo mpaka sasa analiongoza Taifa vizuri, Uongozi atapata moyo zaidi akiona sisi ambao tupo pamoja nae tunaendelea kumuunga mkono kumuonesha kwamba tupo pamoja, ukiwa pamoja na wenzako unapata moyo wa kukabiliana na changamoto kubwa zilizopo ofisini".
Aidha, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amempongeza Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima kwa uongozi imara katika kuhakikisha Huduma za Matibabu ya Dharura zinashushwa ngazi ya Hospitali za Wilaya.
Dkt. Jakaya Kikwete ametoa pongezi hizo leo alipohudhuria hafla ya makabidhiano ya ramani katika eneo la ujenzi wa jengo la Huduma za Matibabu ya Dharura katika Hospitali ya Wilaya ya Chalinze- Msoga kwa Mkandarasi.
“Tulipokuwa na wazo la kujenga Hospitali yetu hii mpya tulizungumza na viongozi wa ABBOT pamoja na Dkt. Dorothy Gwajima wakati huo akiwa Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI, alisatusaidia sana” ameshukuru Mhe. Kikwete.
Hospitali ya Chalinze, Msoga inakuwa Hospitali ya kwanza ya Wilaya kuwa na Huduma za matibabu ya dharura nchini huku ikiwa kwenye eneo ambalo ni njia panda ya kuelekea Mikoa ya Kaskazini na Nyanda za Kati ya nchi na Nyanda za Juu Kusini eneo ambali halina huduma za dharura kuhudumia wagonjwa wenye uhitaji wa huduma za haraka hususani wale wanaopata ajali.