Jakaya Kikwete ungeachana tu na mambo ya siasa. Haitapendeza siku ukitutoka watu wafanye sherehe

Jakaya Kikwete ungeachana tu na mambo ya siasa. Haitapendeza siku ukitutoka watu wafanye sherehe

Umeifanyia mengi nchi hii
Mpaka unastaafu ulikuwa Rais bora kabisa
Uliwabeba wapinzani na kuimarisha demokrasia

Kujiataach na utawala huu watu wameanza kukuchukia
Nachelea kusema mazuri yote uliyofanya yanafutika
Itakuwa ni huzuni watu wakishetehekea siku ukitutoka.kumbuka una miaka 75 sasa.
THE FALL OF CCM 1995-2025.✍️📌
 
Watz bhana kwa kuwa emotional..

Kwa hiyo unadhani watu ambao wapo radhi mali za nchi zipigwe mnada au wachote mabilioni huku watu wakifariki hospitalini kwa kukosa dawa. Ndio watajali nyie mkishangilia vifo vyao kuliko wao kutengeneza dynasties na kuhakikisha hata wajukuu zao wataogelea kwenye mabilioni "generational wealth"...

Mnadhani watu wanajali sana nyie kuwapenda tofauti na kipindi cha kampeni. Amkeni ndotoni wakuu, watu mioyo ishakufa ganzi mbele ya maslahi
Imagine
 
Mwanasiasa yeyote haswa Hawa wa Africa Malengo yake ni kuwa kama JK So acha kujidanganya kuwa JK anaweza kukuelewa na kuku sikia never ever , Tatizo siasa za Africa sio rafiki kabisa Yaani sio kabisa ukitawala Halafu ukaja kuachia madaraka Basi kama hauto muandaa mtu wako kuja kukaa madarakani yule anayekuja kama atakuwa ni mtu wa visasi + chuki + wivu ana weza kuja kukupandikizia mikesi kukufilisi na kukufunga au kukunyonga kabisa

So that's why Unakuta Wana siasa wengi waafrica Wana tabiaa kama za Mzee uliyemtaja wanataka kubaki katika kumaintain power ili kulinda kile walicho kitafuta
 
Naunga mkono hoja

Kwangu mimi JK alikuwa rais mwenye nafuu sana, alijitahidi kuvumilia bunge huru, mahakama haukuchezewa kivile, vyombo vya habari lilikuwa na uhuru, matendo ya utekaji yalikuwa ni negligible, alijenga mabarabara mengi, shule nyingi za kata, udahili wa wanafunzi vyuo vikuu uliongezeka, ajira nyingi sana kila siku, internationally tulikuwa influential ktk siasa za Africa. Ofcourse na mapungufu yalikuwepo.

Lakini Pamoja na hayo sasa ni muda muafaka wa yeye kutambua kuwa Rais wa sasa hakubaliki, na yeye kudhani anaweza kumpigania rais huyu kumsaidia "angalau" aweze kuvuka muda wake salama anakuwa anajiharibia legacy yake mwenyewe, wananchi wanakuwa wanamchukia yeye pia.
Wananchi wangapi?. Wapiga kura wa TZ ni wengi sana na wamejiandikisha, idadi yao ni milioni 37.

Tukipewa uhai usishangae Samia akashinda ushindi wa kishindo kikubwa, Wenye akili timamu wanajua anafanya kitu gani, achana na hivyo vitoto vilivyoshangilia kifo cha Ndugai lipo kundi kubwa sana linasubiri siku ifike likapige kura kwa Samia.
 
Wananchi wangapi?. Wapiga kura wa TZ ni wengi sana na wamejiandikisha, idadi yao ni milioni 37.

Tukipewa uhai usishangae Samia akashinda ushindi wa kishindo kikubwa, Wenye akili timamu wanajua anafanya kitu gani, achana na hivyo vitoto vilivyoshangilia kifo cha Ndugai lipo kundi kubwa sana linasubiri siku ifike likapige kura kwa Samia.
Milioni 37 za mchongo
 
Kuzuia upinzani haikuwa sahihi. Na kuwahonga wapinzani haikuwa sahihi pia. Maendeleo tuliona kiasi kipindi cha Magu. Karudi Kikwete kwa mlango wa nyuma ni ufisadi tu kwa sasa.
Wapinzani walishanunuliwa na mfumo wa awamu ya nne.

Kama magu angeruhusu siasa kipindi chake, basi wale wapinzani woote walionunuliwa kipindi cha awamu ya nne wangetumika kumsumbua sana, na kwa kumsumbua huko, wangechelewesha plan zake za maendeleo.

Plan ikawa ni kupiga ban siasa, na kununua wanasiasa wa upinzani.

Binafsi sioni ubaya wa magu, aliamua kutumia nguvu, kuleta maendeleo ya kweli.

Alitakiwa pia kumfungulia mashtaka kiongozi wa awamu ya nne ili amsulubu na kumzuia asiwe threat kipindi chake, nadhani, alipoamua kutengeneza bunge lake ulikua ni mpango wa kubadilisha baadhi ya sheria ikiwa pamoja na kuruhusu viongozi kushtakiwa.

Kama magu angelikuwepo kipindi hiki, msoga angekua jela au angekua kila mara anahuzulia kesi zake mahakamani, maana mashtaka yale halisi yapo
 
Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni. JK wakati wa Urais wake alifanya mambo mengi mema, ya kuigwa, kukumbukwa na kuenziwa. Ni katika wakati wake tuliona viongozi wa vyama vya upinzani walizunguka kila siku Ikulu wakinywa juisi na kula mapocho pocho. Kulipotokea changamoto za kisiasa, alikaa na viongozi wa upinzani na kuzungumza nao mambo yakaenda.

Ni katika kipindi hicho Demokrasia nchini ilishamir. Uhuru wa vyombo vya habari ulikuwa mkubwa. Nikitaja kwa uchache. Siyo Malaika yapo pia kama binadamu hakufanya vya kutosha.

Baada ya JPM kufariki, tunasikia JK Kawa karibu sana na Rais aliyeko madarakani SSH. Si jambo baya maana mama alipata nafasi hiyo bila kutarajia, ni mipango ya Mungu. Japo Urais ni taasisi, kwenye mazingira hayo haikuwa kosa kwa Rais mstaafu kuwa karibu na mama kwa maana ya kumshauri na kumtia moyo. Urais si mchezo ukizingatia kuwa SSH alishtukizwa tu.

Hata kama Rais wetu SSH anashauriwa na Rais mstaafu JK, sidhani na siamini kama ushauri huo unaingia moja kwa moja kwenye utekelezaji bila kupitia kwenye vyombo husika. Siasa ni nzuri sana maana ni maisha ya leo na kesho. Lakini Siasa ni mbaya sana, inaweza kukujenga leo lakini ikakubomoa na kukufinyanga kesho.
 
Back
Top Bottom