Jamaa alieoa dada yangu mgumu kuwasiliana na sisi ndugu wa mkewe

Jamaa alieoa dada yangu mgumu kuwasiliana na sisi ndugu wa mkewe

huyu jamaa ni kweli tulimkabidhi dada yetu kifamilia, lakini baada ya miezi 6 kupita kuwasiliana adi tumpigie sisi, na sisi tumeamua hatutomtafuta akijisikia sawa tu, jengine bado hajamalizia mahari, kuhus maisha wanaishi vizuri na dada yetu ila sina uhakika 100%.nyie vijana acheni zadhau, tu nampigia tu dada yetu. yeye no.
Unataka uwe unawasiliana naye ili umpole dadayako mume?
 
Akili za kimaskini hizi. Sema unadai mahari sasa gia ya kuingilia ndo tatizo.
Kwenye mahusiano mengi mashemeji wengi wanawaza kupiga hela tuu. issue za mahusiano ooh kupiga simu ni geresha tuu. kwani wao wanakatazwa kupiga simu? Mimi ndoa yangu ina zaidi ya miaka 15 kwa sasa ila nimeamua kuchinjia baharini mijinga jinga yote inayoitwa mashemeji. Nilioa, nikalipa mahari yote, nilihangaika baba yao alipoumwa hadi akafariki tukaenda tukazika. Miaka michache baadaye mama yao akaumwa nikahangaika naye hadi nikamchukua nikamleta kwangu kumuuguza kila kitu nikawa nagharimikia hadi bima nikamkatia. Hapo kuna mashemeji wakikwama kidogo wanampigia dada yao ananiambia kwa huruma nawasaidia.Baadaye mama akaforce kurudi kwao nikamrudisha. Tukaendelea kumuuguza hadi akafariki nilienda nikagharimikia almost nusu ya gharama zote za msiba. baada ya mwaka, mama yangu mzazi akafariki. Umbali wa mahali msiba wa mama yangu ulipotokea na kwa wakwe zangu nauli ni sh 5000. Lakini hakuna aliyekanyaga kwa kisingizio cha kukosa nauli, mashemeji zangu wana familia zao, mwingine anamiliki duka, mwingine mashine ya kusaga na mashamba kibao. Nikawapa taarifa kwamba sisi tumeandaa gari Costa kusafirisha mwili pamoja na abiria basi mwakilishi afike atasafiri na kurudi bure. Maana yake akisafiri hadi msiba ulipotokea gharama a kusafiri kwenda kwetu ni bure, takriban nauli ya kwenda na kurudi isingepungua 50k. bado hakuna aliyetokea. Yaani wao wameshindwa kuchangishana hata wamtume mmoja aje wawakilishe? Gari lililokodiwa lilienda na abiria pungufu, Nilienda msibani na mke wangu tuu. Wao haya kuja hawakuja, basi hata salamu za rambirambi hata wangechangishana wakatuma hata kwa M Pesa hata elf moja haikutumwa.

Baada ya miaka michache napigiwa na Bwashemeji ananiambia mbona sipigi simu wala siendi kuwatembelea? au kwa vile wazazi wamefariki wote sasa hata wao siwatembelei? Niliwaza cha kumjibu sikupata. Mimi ni wa muhimu kwao as far as nawapa chochote, ila kibao kikigeuka kwangu hawana muda.Basi kila mtu ashinde mechi zake
Expert nakuunga mkono,huna mashemeji
 
huyu jamaa ni kweli tulimkabidhi dada yetu kifamilia, lakini baada ya miezi 6 kupita kuwasiliana adi tumpigie sisi, na sisi tumeamua hatutomtafuta akijisikia sawa tu, jengine bado hajamalizia mahari, kuhus maisha wanaishi vizuri na dada yetu ila sina uhakika 100%.nyie vijana acheni zadhau, tu nampigia tu dada yetu. yeye no.
Tabia za ajabu sana eti kila siku kupigiana simu kama sina shida ya mhimu hata sipigi simu ya nini?
 
Hivi unawapigia pigia ukweni ili iweje kama sio kutaka kupigwa vizinga

Mimi wakwe siwapigiagi tena sio kukwepa vizinga ila najikuta sina story za kupiga nao
Mimi afadhali baba mkwe naweza mpigia tukapiga story mbili tatu. Mama mkwe sina hata cha kuongea nae
 
huyu jamaa ni kweli tulimkabidhi dada yetu kifamilia, lakini baada ya miezi 6 kupita kuwasiliana adi tumpigie sisi, na sisi tumeamua hatutomtafuta akijisikia sawa tu, jengine bado hajamalizia mahari, kuhus maisha wanaishi vizuri na dada yetu ila sina uhakika 100%.nyie vijana acheni zadhau, tu nampigia tu dada yetu. yeye no.
Sasa awasiliane na nyinyi kuhusu kitu gani mwacheni dada yenu aenjoy na mumewe
 
Kah! awapigie ili iweje sasa? kama kuna shida atapata taarifa kwa Dada yenu
 
Mahari atamalizia, kwani angemaliza ndio msingetaka awatafute?
 
Mimi afadhali baba mkwe naweza mipigia tukapiga story mbili tatu. Mama mkwe sina hata cha kuongea nae
Kiuhalisia kuongea na wakwe ni kipaji sijui mnaongelea inshu gani maana kama ni salamu ni shikamoo marahaba imeisha iyo
 
Ndiyo huyohuyo dada Yako ambaye mumewe hajaja kujitambulisha na hajamtolea mahari au huyu ni mwingine Tena?🤔
 
Anayemuelewa shemeji yako ni dad's ako aliyeolewa. We hata ukijitahidi kumsoma huwezi kumuelewa.
 
Unavoonesha ulitaka uwe unaongea nae hovyo hovyo umzoee ili uhamie kwake watu si wajinga siku hizi kastukia mchongo kama una dada mwingine tafuta shemeji usuke upya mipango

Ukweni tunapiga simu kwa sababu maalumu sio nipige eti nilikuwa nawasalimia tu kesho kutwa nipige tena kuwasalimia tu na mawasiliano na dada yenu kama yapo tatizo liko wapi au na nyie mnaenjoy mkisikia sauti yake kwenye simu🤔🤔🤔
Yani mimi huwa nakereka mtu anakupigia unadhani kuna jambo la maana eti anakusalimia upuuzi gani huu wewe huna kazi!
 
Kwa hiyo mmekaa mkajadiliana kwanini shemeji yenu hajamalizia mahari ya dada, sio!

Daaah! Umasikini ukichanganyika na uvivu ni kitu kibaya sana.

Huwa napiga simu ukweni mara chache chache sana kwa baba mkwe. Vinginevyo kuwe Kuna tatizo
 
Back
Top Bottom