Unataka uwe unawasiliana naye ili umpole dadayako mume?huyu jamaa ni kweli tulimkabidhi dada yetu kifamilia, lakini baada ya miezi 6 kupita kuwasiliana adi tumpigie sisi, na sisi tumeamua hatutomtafuta akijisikia sawa tu, jengine bado hajamalizia mahari, kuhus maisha wanaishi vizuri na dada yetu ila sina uhakika 100%.nyie vijana acheni zadhau, tu nampigia tu dada yetu. yeye no.
Bas mwachenianasema ndo alivyo
Expert nakuunga mkono,huna mashemejiAkili za kimaskini hizi. Sema unadai mahari sasa gia ya kuingilia ndo tatizo.
Kwenye mahusiano mengi mashemeji wengi wanawaza kupiga hela tuu. issue za mahusiano ooh kupiga simu ni geresha tuu. kwani wao wanakatazwa kupiga simu? Mimi ndoa yangu ina zaidi ya miaka 15 kwa sasa ila nimeamua kuchinjia baharini mijinga jinga yote inayoitwa mashemeji. Nilioa, nikalipa mahari yote, nilihangaika baba yao alipoumwa hadi akafariki tukaenda tukazika. Miaka michache baadaye mama yao akaumwa nikahangaika naye hadi nikamchukua nikamleta kwangu kumuuguza kila kitu nikawa nagharimikia hadi bima nikamkatia. Hapo kuna mashemeji wakikwama kidogo wanampigia dada yao ananiambia kwa huruma nawasaidia.Baadaye mama akaforce kurudi kwao nikamrudisha. Tukaendelea kumuuguza hadi akafariki nilienda nikagharimikia almost nusu ya gharama zote za msiba. baada ya mwaka, mama yangu mzazi akafariki. Umbali wa mahali msiba wa mama yangu ulipotokea na kwa wakwe zangu nauli ni sh 5000. Lakini hakuna aliyekanyaga kwa kisingizio cha kukosa nauli, mashemeji zangu wana familia zao, mwingine anamiliki duka, mwingine mashine ya kusaga na mashamba kibao. Nikawapa taarifa kwamba sisi tumeandaa gari Costa kusafirisha mwili pamoja na abiria basi mwakilishi afike atasafiri na kurudi bure. Maana yake akisafiri hadi msiba ulipotokea gharama a kusafiri kwenda kwetu ni bure, takriban nauli ya kwenda na kurudi isingepungua 50k. bado hakuna aliyetokea. Yaani wao wameshindwa kuchangishana hata wamtume mmoja aje wawakilishe? Gari lililokodiwa lilienda na abiria pungufu, Nilienda msibani na mke wangu tuu. Wao haya kuja hawakuja, basi hata salamu za rambirambi hata wangechangishana wakatuma hata kwa M Pesa hata elf moja haikutumwa.
Baada ya miaka michache napigiwa na Bwashemeji ananiambia mbona sipigi simu wala siendi kuwatembelea? au kwa vile wazazi wamefariki wote sasa hata wao siwatembelei? Niliwaza cha kumjibu sikupata. Mimi ni wa muhimu kwao as far as nawapa chochote, ila kibao kikigeuka kwangu hawana muda.Basi kila mtu ashinde mechi zake
Yeahakiachika ndio utaelewa maana ya ''mind your business"
Tabia za ajabu sana eti kila siku kupigiana simu kama sina shida ya mhimu hata sipigi simu ya nini?huyu jamaa ni kweli tulimkabidhi dada yetu kifamilia, lakini baada ya miezi 6 kupita kuwasiliana adi tumpigie sisi, na sisi tumeamua hatutomtafuta akijisikia sawa tu, jengine bado hajamalizia mahari, kuhus maisha wanaishi vizuri na dada yetu ila sina uhakika 100%.nyie vijana acheni zadhau, tu nampigia tu dada yetu. yeye no.
Mimi afadhali baba mkwe naweza mpigia tukapiga story mbili tatu. Mama mkwe sina hata cha kuongea naeHivi unawapigia pigia ukweni ili iweje kama sio kutaka kupigwa vizinga
Mimi wakwe siwapigiagi tena sio kukwepa vizinga ila najikuta sina story za kupiga nao
Sasa awasiliane na nyinyi kuhusu kitu gani mwacheni dada yenu aenjoy na mumewehuyu jamaa ni kweli tulimkabidhi dada yetu kifamilia, lakini baada ya miezi 6 kupita kuwasiliana adi tumpigie sisi, na sisi tumeamua hatutomtafuta akijisikia sawa tu, jengine bado hajamalizia mahari, kuhus maisha wanaishi vizuri na dada yetu ila sina uhakika 100%.nyie vijana acheni zadhau, tu nampigia tu dada yetu. yeye no.
Kiuhalisia kuongea na wakwe ni kipaji sijui mnaongelea inshu gani maana kama ni salamu ni shikamoo marahaba imeisha iyoMimi afadhali baba mkwe naweza mipigia tukapiga story mbili tatu. Mama mkwe sina hata cha kuongea nae
Yani mimi huwa nakereka mtu anakupigia unadhani kuna jambo la maana eti anakusalimia upuuzi gani huu wewe huna kazi!Unavoonesha ulitaka uwe unaongea nae hovyo hovyo umzoee ili uhamie kwake watu si wajinga siku hizi kastukia mchongo kama una dada mwingine tafuta shemeji usuke upya mipango
Ukweni tunapiga simu kwa sababu maalumu sio nipige eti nilikuwa nawasalimia tu kesho kutwa nipige tena kuwasalimia tu na mawasiliano na dada yenu kama yapo tatizo liko wapi au na nyie mnaenjoy mkisikia sauti yake kwenye simuπ€π€π€
Tuko wengi mkuu π π πNilijua Niko peke yangu ππ
Majadiliano yangu Makuu ni sms
πππHatari yani... Watuvumilie tu aisee.yaani mpaka nimejistukia nikahisi mleta sledi ananisema...baba mkwe mara ya mwisho tumewasiliana mwaka juzi