Jamaa yangu ananitesa kisa alinitafutia kazi, ni haki?

Jamaa yangu ananitesa kisa alinitafutia kazi, ni haki?

Wewe una tabia ya uchoyo na ubinafsi. Mtu mwenye busara angemsitiri jamaa yake na sio kuja kuandika uzi hapa. Wewe kama unashindwa ku-handle suala dogo kama hilo hata hiyo ajira unaweza ukaipoteza. Ninaungana na mwanauvinza kwamba uache kazi ili kumkomesha
Nimsitiri kwani yupo uchi? We unaona achokifanya ni sawa?
 
Wasalaam,
Nilikuwa down bad, Yani nimepigika kinoma, Yani apeche alolo, Yani mbombo ngafu, Yani moja haikai mbili haikai, Yani nmechina mweupe pee.
Kula ya mashaka, kulala kama ndege.

ila Kuna huyu jamaa angu tulisoma ote Olevel akaniconnect kwenye ajira inalipa fresh sio haba.


Sasa tatizo, imekuwa kama kero, Kila sku anajimwambafy kuwa bila yeye nsingetoboa anasema natakiwa niwe namshukuru Kila mshahara ukitoka.
Tukienda out Kila siku Mimi tu ndo anataka nimnunulie bia.
Wote tuna mshahara ila yeye anataka na shida zake Mimi nimtatulie.

Mimi naona imekuwa kama manyanyaso Sasa .... nifanyaje?
Umenikumbusha kuna habari moja ya mshua mmoja na Kigogo wa CCM.

Huyo mshua alikuwa mtumishi wa shirika moja kubwa la umma kwa muda mrefu, alikuwa anakaribia kupata kazi ya juu kabisa ya uteuzi wa rais katika shirika hilo, moja kati ya kazi nzuri kabisa Tanzania.

Alikuwa anajuana na kada mmoja mkubwa sana wa CCM. Sasa yule kada akamwambia mshua yule, hizi kazi kubwa huwezi kupata bila kupewa introduction kwa rais, kwa hivyo jiandae nikakupe introduction kwa rais. Ukiwa tayari nipigie simu nikuunganishie tuende Ikulu ukaongee na rais.

Yule mshua kwa heshima akakubali. Halafu akaipotezea kabisa ile issue.

Yuke kada mkubwa wa CCM akawa anasubiri kupigiwa simu, lakini akawa hasikii kitu. Yule mshua akaipotezea issue.

Mwishowe kabisa, rais akamteua yule mshua, bila ya yule mshua kupewa introduction kwa rais na kada wa CCM.

Siju moja miaka mingi baadaye, nikamuuliza yule mshua, kwa nini hukumpigia simu yule kada wa CCM ukapewe introduction kwa rais? Huoni kama ulikuwa unachezea shilingi chooni? Huoni kwamba ungeweza kukosa uteuzi kwa ajizi zako tu?

Yule mshua akaniambia, Kiranga, ningepelekwa kwa rais tu na yule kada wa CCM, basi miaka yote angejitapa kwamba yeye ndiye kanipatia ile kazi, na nisingeweza kufanya kazi yangu kwa uhuru. Najivunia sana ukweli kwamba rais ameniteua mwenyewe bila ya mimi kupelekwa kwake na mtu kupewa introduction.

Tatizo lako umepata kazi kwa connection ya mtu, na huyo mtu anajiona ana nguvu juu yako kwa sababu kakutafutia wewe hiyo kazi.
 
Umenikumbusha kuna habari moja ya mshua mmoja na Kigogo wa CCM.

Huyo mshua alikuw mtumishi wa shirika moja kubwa la umma kwa muda mrefu, alikuwa anakaribia kupata kazi ya juu kabisa ya uteuzi wa rais katika shirika hilo, moja kati ya kazi nzuri kabisa Tanzania.

Alikuwa anajuana na kada mmoja mkubwa sana wa CCM. Sasa yule kada akamwambia mshua yule, hizi kazi kubwa huwezi kupata bila kupewa introduction kwa rais, kwa hivyo jiandae nikakupe introduction kwa rais. Ukiwa tayari nipigie simu nikuunganishie tuende Ikulu ukaongee na rais.

Yule mshua kwa heshima akakubali. Halafu akaipotezea kabisa ile issue.

Yuke kada mkubwa wa CCM akawa anasubiri kupigiwa simu, lakini akawa hasikii kitu. Yule mshua akaipotezea issue.

Mwishowe kabisa, rais akamteua yuke mshua, bika ya yule mshua kupewa introduction kwa rais na kada wa CCM.

Siju moja miaka mingi baadaye, nikamuuliza yule mshua, kwa nini hukumpigia simu yule kada wa CCM ukapewe introduction kwa rais? Huoni kama ulikuwa unachezea shilingi chooni? Huoni kwamba ungeweza kukisa uteuzi kwa ajizi zako tu?

Yule mshua akaniambia, Kiranga, ningepelekwa kwa rais tu na yule kada wa CCM, basi miaka yote angejitapa kwamba yeye ndiye kanipatia ike kazi, na nisingeweza kufanya kazi yangu kwa uhuru. Najivunia sana ukweli kwamba rais ameniteua mwenyewe bila ya mimi kuoelekwa kwake na mtu kupewa introduction.

Tatizo lako umepata kazi kwa cinnection ya ntu, na huyo mtu anajiona ana nguvu juu yako kwa sababu kakutafutia wewe hiyo kazi.
Shida bro ya jamii yetu ni blabbing and blabbering isiyo faa.

Watu Wana taka watukuzwe na kukumbukwa kupita kiasi.
 
Back
Top Bottom