Jamaa yangu ananitesa kisa alinitafutia kazi, ni haki?

Nimsitiri kwani yupo uchi? We unaona achokifanya ni sawa?
 
Umenikumbusha kuna habari moja ya mshua mmoja na Kigogo wa CCM.

Huyo mshua alikuwa mtumishi wa shirika moja kubwa la umma kwa muda mrefu, alikuwa anakaribia kupata kazi ya juu kabisa ya uteuzi wa rais katika shirika hilo, moja kati ya kazi nzuri kabisa Tanzania.

Alikuwa anajuana na kada mmoja mkubwa sana wa CCM. Sasa yule kada akamwambia mshua yule, hizi kazi kubwa huwezi kupata bila kupewa introduction kwa rais, kwa hivyo jiandae nikakupe introduction kwa rais. Ukiwa tayari nipigie simu nikuunganishie tuende Ikulu ukaongee na rais.

Yule mshua kwa heshima akakubali. Halafu akaipotezea kabisa ile issue.

Yuke kada mkubwa wa CCM akawa anasubiri kupigiwa simu, lakini akawa hasikii kitu. Yule mshua akaipotezea issue.

Mwishowe kabisa, rais akamteua yule mshua, bila ya yule mshua kupewa introduction kwa rais na kada wa CCM.

Siju moja miaka mingi baadaye, nikamuuliza yule mshua, kwa nini hukumpigia simu yule kada wa CCM ukapewe introduction kwa rais? Huoni kama ulikuwa unachezea shilingi chooni? Huoni kwamba ungeweza kukosa uteuzi kwa ajizi zako tu?

Yule mshua akaniambia, Kiranga, ningepelekwa kwa rais tu na yule kada wa CCM, basi miaka yote angejitapa kwamba yeye ndiye kanipatia ile kazi, na nisingeweza kufanya kazi yangu kwa uhuru. Najivunia sana ukweli kwamba rais ameniteua mwenyewe bila ya mimi kupelekwa kwake na mtu kupewa introduction.

Tatizo lako umepata kazi kwa connection ya mtu, na huyo mtu anajiona ana nguvu juu yako kwa sababu kakutafutia wewe hiyo kazi.
 
Shida bro ya jamii yetu ni blabbing and blabbering isiyo faa.

Watu Wana taka watukuzwe na kukumbukwa kupita kiasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…