Jamani mpeni Tundu Lissu PHD ya heshima jinsi alivyomwelezea vizuri Mwalimu Nyerere huko Uganda

Sasa ndio anajifanya anamuheshimu Nyerere wakati alishasema Mwalimu alizoea kuishi kwa uongo na udanganyifu? Sitoshangaa siku akianza kumsifia Magufuli ha ha ha😎
Ulimsikiliza na kumuelewa au nyie ndio walewale?
Kuhusu kumsifu Magufuli kwani hujasikia? Amemsifu sana na mara nyingi amemtetea hasa kuhusu rasilimali za nchi. Lissu ni mkweli sana, huwa hamsingizii uongo binadamu mwingine na nikuambie jambo? Ayasemayo yote kuhusu Hangaya hakuna analodanganya.
 
Mwenye macho haambiwi tazama na mwenye masikio haambiwa sikia lakini pia Chema chajiuza na Kibaya chajitembeza!
 
Zitafute hotuba alizokuwa anatoa kwenye Bunge la Katiba kumhusu Nyerere na alivyokuwa akimtuna na kumdhalilisha ndio utajua kwamba Lisu dishi limeyumba na hajui anasimamia wapi. Kwa ufupi ni kigeugeu na mfuata upepo.
 
Ona huyu anataka sisi tutafute kitu kisichokuwepo. Wewe unayesema alimtukana ndio utafute hizo clips kama ushahidi wa maelezo yako. Lissu ni mkweli
 
Ona huyu anataka sisi tutafute kitu kisichokuwepo. Wewe unayesema alimtukana ndio utafute hizo clips kama ushahidi wa maelezo yako. Lissu ni mkweli
Hansad za bunge zipo. Lisu ni ndumilakuwili flani anaebadilika kulingana na fursa.
 
Hiyo shahada ni ya Marais wa Kiafrika tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…