James Mbatia amtaka Majaliwa ajiuzulu Uwaziri Mkuu

Mbona mnamlazimisha sana wazee, mnataka mama abaki pekeake ili mumpelekeshe jinsi mnavyojiskia 😁😁😁!!?

Sasa kwa taarifa yenu atajiuzulu kisha atateuliwa upya acheni utoto!
Tumpelekeshe mama Samia kivipi?
Kwani Mama Samia hajitambui?
Unataka kusema Mama Samia anamuhitaji Majaliwa ili asipelekeshwe?
Huko ni kumdhalilisha wazi wazi Rais wetu, Mama Samia Suluhu.

Mama Samia kwa sasa ndio rais wa Tanzania wa awamu ya Sita. Lazima apewe nafasi ya kuunda serikali yake na kufanya kazi zake kwa uhuru na haki.

Majaliwa aliteuliwa kuwa waziri mkuu chini ya utawala wa awamu ya tano ulioongozwa na Magufuli. Magufuli hayupo tena madarakani, Majaliwa anawajibika kwa rais yupi?

Majaliwa anapaswa kujiuzuru ili kulinda heshima yake, kuilinda katiba na kulinda heshima ya taifa la Tanzania.

Majaliwa jiuzuru sasa.
 
Dikteta hajawahi kua na dhamira njema
 
Chezea ugali utaribu ni ule ule kama walivompa urais bana piga chini baraza maisha yaanze moja
 
Hahahahah

Baki na Mavi yako Nyumbani

Ntamiss sana Mtani wetu JPM
Hata Mimi mtani wangu namkubali saana. Ile roho, ujasiri, na uthubutu haumithiliki kirahisi.

Au nasema uongo ndugu zangu!

Mara Baki na Mavi yako. [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Huo ni uchochezi sasa

Mwanasheria nguli Dr Mwigullu Nchemba alishatoa ufafanuzi!
Siku hizi siyo mchumi first class! hata kama PM atagoma kujiuzulu bado rais anayo mamlaka ya kuvunja baraza la mawaziri, kufanya reshuffle na hata ku-suspend bunge na kurudi kwenye uchaguzi...
 
Wanasiasa wana maneno sana. Hawa wapinzani ni wepesi sana kuongea, ila wao huwa KAMWE hawatoi mifano au kutenda yale wanayoyahubiri. Mfano, ni uwajibikaji wa kidemokrasia, pale chama kinaposhindwa uchaguzi, basi kiongozi wa juu wa chama hicho kujiuzuru. Last year Jeremy corbyn alijiuzuru baada ya kubwagwa na boris. Huyu mbatia mbona yeye hajiuzuru kwa chama chake kuangushwa?
 
Siku moja moja huyu bwana huwa na points za ukweli. Haki kweri kuliko hata johnthebaptist na wenzake.

Kwa hakika angekuwa amemsaidia sana madam president.
 
Baadhi ya Mitz ni mijitu mijinga sn..... Kwao rais ni mungu wao yani
 
Katiba iko wazi kabisa, ni kwa wale wasioisoma au wale wanaoisoma kwa kupindishapindisha tu kwa ajili ya ajenda zao tu. Angalia, katiba yetu inasema hivi:





Angalia kifungu kidogo hicho cha (10) nilichowekea rangi, kuwa mtu atakayechukua madaraka ya urais ama kwa kurithi kutokana na kifungu kidogo cha (3) (yaani rais kuondolewa madarakani na baraza la mawaziri) hadi kifungu kidogo cha (5) (yaani rais akifariki), hana madaraka ya kuvunja Bunge au Baraza la mawaziri au kutengua teuzi za rais aliyekuwapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…