Mimi ninakujibu kulingana na madai yako, yaani wewe unataka nikatae UKWELI kwakuwa aliyesema huo ukweli ni mtu fulani usiyempenda!!, haiwezekani, ukweli ni ukweli tu hata utoke kwa adui yako utabaki kuwa ukweli na mtu mwema ni yule anayepokea ukweli kutoka popote.
Kuhusu Qur'an kukopi hiyo sio kweli, kwani jambo moja likiandikwa na mtu mmoja na akaja mtu mwingine akaliandika je ni lazima huyo aliyekuja kuliandika baadaye atakuwa kalikopi kwa huyo wa kwanza??!!, chukua mfano hai Leibnitz na Newton ndio waanzilishi wa Culculus na wote bila kujuana waliandika kitu kimoja wakiwa mahali tofauti katika wakati mmoja, je nani alikopi kwa mwenzake??--- historia inasema hakuna aliyekopi kwa mwenzake, ni hivyo hivyo Allah yeye ni "ilmul ghaibi wa shahada", anajua mambo yaliyopita, ya sasa na ya baadaye iweje akopi kwa hao Sumerians kitu alichokifanya mwenyewe kabla hata hao Sumerians hajawaumba??!!, very hilarious.