JamiiForums: Unaweza kuwa VERIFIED, fuata hatua hizi

Kama zipi, kuna mijadala huwezi kuchangia.
kwa maoni yangu
1.kila mtu atajiheshimu zaidi na atawaheshimu wenzake.

2. itapunguza ban kwa sababu kila mmoja ataepuka kutumia lugha zisizo faa.

3. tutafahamiana zaidi.

4. tutaaminiana zaidi ktk kupeana michongo/fursa.
n.k
kabla hujachangia mjadala wowote naamini kila mtu atajitafakari kwanza kama anaweza kuchangia kuliko ilivyo sasa kila mmoja anakurupuka tu!
sio lazima kila mjadala kila mtu achangie, unaweza ukafuatilia tu na ukapata faida na ikakusaidia sana.
 
Mkuu kwa maelezo ya hapo naona inawezekana wewe kuwa verified kwa jina hilo la Watu8

Reference kwa Bujibuji.
 
kwenye hiyo list ya verified users nimeona status za baadhi ya users bado ni za zamani na hazija badilishwa, mfano 'choma cha nkola MP' wakati ki uhalisia he/she is no longer MP...….., itakuwa ni busara kama ma users wenyewe hata JF ikawabadilisha hizo status, vile vile baadhi ya users walishaa RIP, sasa ni kwanini tusiwatoe kwenye list ya JF verified users??
 
Shida ukiwa verified inakuwa ni rahisi kwa JF kukufatilia, ikitokea siku umefungua ID mpya ukaandika visivyoeleweka wanakuunganishia ID unaumbuka bora nibaki hivi hivi kuliko kujitia kitanzi cha verification
 
Mtego mzuri huu wa Wasiojulikana kula damu za watu......
Waoga wa kuwa verified ni wale waliozea kutukana mitandaoni, matapeli,wezi na malaya.

Kwa mtu mzima anayejielewa ambaye anaichukulia Jamiiforums kwa heshima na staha. Ambaye siku zote ana michango chanya, mwenye kukubali kukosolewa na anayejua kuhandle mijadala kuwa verified ni nafuu zaidi kwake.

Vichaa,watu waoga,wasiojiamini,washamba wa mitandaoni and the like, kamwe hawawezi kufurahia kuwa verified.

Verified ipo kwa ajili ya watu makini pekee na smart kichwani kama Mzee Mwanakijiji Bujibuji Maxence Melo Mshana Jr
 
[emoji1752][emoji1545][emoji1752][emoji1752][emoji1548][emoji1548]

Sent from my Infinix X627 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…