Jamvi la wanawake: Ni kazi gani za nyumbani anapaswa kufanya mwanaume / mume akitoka kazini?

Jamvi la wanawake: Ni kazi gani za nyumbani anapaswa kufanya mwanaume / mume akitoka kazini?

Mfanye yote lakini hata siku moja msije mkadhani kuwa mnaweza kuwa sawa na waume zenu. Radical feminism ni mpango wa shetani kuangamiza taasisi takatifu ya ndoa kama ilivyoasisiwa na Mungu mwenyewe - na washirika wake wakuu ni hawa homosexuality, timu kataa ndoa n.k. Zote ni kampeni za shetani kuisambaratisha taasisi ya ndoa ambayo kimsingi ndiyo hutupa familia bora na imara. Na bila familia bora na imara huwezi kuwa na jamii imara na bora. Ni anguko kuu!

Fanyeni yote lakini simameni katika zamu yenu kama wasaidizi wetu, wake zetu, wapendwa wetu na mama watoto wetu; nasi tusimame katika zamu yetu kama vichwa vya familia, walinzi, providers na makuhani wa familia zetu. Huo ndiyo mpango wa Mungu; na mengine yote ni madogo na yanazungumzika! 🙏🏿
Rudi kwenye mada, mshauri huyu binti/mke kwenye hayo mambo mawili aliyouliza.
 
Serious huu ndio muda wa kuogeshana mama, unanunua shower jeri mpya ijumaa wife hajui

Unamwita bafuni unamuogesha huko mnakulana huko.

Wakija kina junior hapo kichwa kinawaza deals na mipango ya site mpya+ Ada
Kama kweli unafanyaga haya, basi huwa unasusiwa mbususu sana mpaka uchoke
 
Kivumbi na jasho🔥🔥🔥
Ukijiona bado hupo tayari kwa majukumu na kazi za familia basi Bora ukae single,upambane na kukufanyia Kazi za nyumbani Kwa ajili yako mwenyewe.

Ukiona bado una ubinafsi wa kuhesabiana majukumu basi ujue wewe bado upo kundi la kuendelea kuwa mwenyewe kwanza.


Sema huyo kaka naye mvivu hakiyanani
Yaani mtu hagusi Kazi hata Moja!amekaa tu !hajisikii vibaya kukaa tu mwenzie anafanya kazi zote na wakati wamefika wote wakiwa wamechoka!

Kweli ndoa ni shughuli pevu
Binti mwenye ndoa yake changa kaja kulalamika kikaoni kwamba mumewe hafanyi shughuli yoyote wakirudi nyumbani japo wote wanafanya kazi na wanatoka asubuhi kwenda kazini na kurudi jioni.

Wanaishi nje kidogo ya mji ila wana usafiri, hivyo huwa wanapitiana baada ya kazi na kurudi nyumbani pamoja. Mke analalamika kuwa anachoka kufanya shughuli zote za nyumbani peke yake kwasababu wakirudi nyumbani mume anaenda kuangalia TV au kujilaza mpaka muda wa chakula.

Wenye uzoefu; msaidieni kumshauri:
  1. Ni namna gani aanzishe mazungumzo na kuwasilisha hii kero yake kwa busara na heshima.

  2. Ni kazi zipi wanaume wanapaswa kufanya au wanaweza kusaidiana nyumbani baada ya kutoka kazini.


PS:
Walikubaliana wasiwe na msichana wa kazi kusave pesa na kwa sababu nyumba waliyopanga haina chumba cha ziada.
 
Anatakiwa akapumzishe akili grozar iliyoko karibu kwa kupata bia bariiid huku akivuta hisia jinsi ya kuja kula chakula cha usiku
Kwahiyo we Shing hata kuweka sahani mezani hutaki na ukirudi kutoka kunywa bia zako huyo mkeo bado awe na nguvu za kukususia mbususu. Ndiyo maana mnalalamika wanawake hawana hamu na tendo, wanakua wamechoka jamani 🤣 🤣 🤣
 
Kwahiyo we Shing hata kuweka sahani mezani hutaki na ukirudi kutoka kunywa bia zako huyo mkeo bado awe na nguvu za kukususia mbususu. Ndiyo maana mnalalamika wanawake hawana hamu na tendo, wanakua wamechoka jamani 🤣 🤣 🤣
Swali lako linaonesha una element za ufeminist... Kwani hukujifunza kwa mama?😁
 
Rudi kwenye mada, mshauri huyu binti/mke kwenye hayo mambo mawili aliyouliza.
Jibu kuu limo humo humo (kama ukishughulisha ubongo japo kidogo).....

Asimame katika zamu yake kama mke mwema na mume wake naye asimame katika zamu yake kama mume mwema kama Mungu Alivyokusudia. Mengine yote ni madogo na yanazungumzika.

Mimi na Mama E, kwa mfano, huwa tunapika pamoja. Nakata vitunguu na nyanya wakati yeye anachambua mchele huku tunapiga umbea na kupanga mipango yetu. Wakati mwingine namwandalia maji ya kukoga...you know the small things. It is always about the small things!

Nasisitiza tena: kila mmoja akisimama katika zamu yake, mengine yote ni nyongeza tu. Palipo na upendo wa kweli, heshima na kuaminiana hakuna kinachoshindikana!
 
Back
Top Bottom