Jana nimeenda club kwa mara ya kwanza, nimetoka nduki baada ya kuuziwa maji 4000/=

Jana nimeenda club kwa mara ya kwanza, nimetoka nduki baada ya kuuziwa maji 4000/=

Sehemu kama hizo kama wewe ji kabwela inatakiwa unaenda ukiwa full yaani umekuka na kushiba then unaenda kuburudika ata ukinunua maji ya 4000 sio mbaya unakunywa mpaka ahsubuhi.

Kuna siku nilikua malaika beach nikaambiwa wine yq 12000 wao wanauza 45k nikasema hii nikawa nafanya kazi ya kuwachenga wahudumu huku naendelea kula burudani saafi.
Hahaha
 
Pole xana, pia hongera kwa kukubali fedheha na aibu ili usave 4000 yako kuliko kupoteza ela yako ili tu ufiche aibu then badae kuanza kuijutia...kwa maisha ya mtanzania wa hali ya chini kununua maji kwa 4000 ni ukichaa wakati hiyo ela unapata chapati 10 na kikombe cha chai kwa mama lishe, pia hao uliowakuta huko sio wote wanaishi maisha yao halisi wengi tu wanafake maisha so wasikutishe sana!
Wa hali ya chini anaenda club kufanya nn? Si aende dukani kwa mangi?
 
Usiige maisha wala kutaka kujilinganisha na mtu mwingine.....Maisha ni Siri kubwa kuhusu swala la kupata hela Kila mtu ana mbinu zake za kupata hela ni ngumu Sana kuuziwa silaha zote za mtu(Mbinu za kupata hela)

Pambana , pambana,pambana
Kuna mchina aligoma kuniuzia saa ya nakshi kwenye ndege. Nikadhani amenidhalilisha....nilipofika Mtaa wa Congo, Dar es Salaam nikamuelewa yule Dada wa Kichina kwenye ndege!!!!
 
Naomba udadavue vizuri yaani ulikuwa huna hela au ....?
Dolali nilikuwa nayo Tena wakati huo naitwa "Kelele"....sema nilikuwa nimeangukia kwenye trick za marketing officers wa saa za nakshi, yule Dada wa kichina ndiye aliniokoa. Yaani nilitaka kununua muhogo uliochemshiwa Manzese kwa Bi-Nyau na kufungwa kwenye karatasi zenye Nembo ya KFC kwa bei ya nyumba ya Ufukweni Zanzibar.

Wakati mwingine, binafsi na hisi ni ulimbukeni wangu kununua kitu kwa bei ya juu wakati najua kitu hicho hicho naweza kukipata sehemu nyingine kwa bei ya chini.
 
Kiukweli watu huko duniani Wana pesa aisee, imebidi nijitafakari upya nimekuja kufanya nini duniani kwa sababu kwa mambo niliyoyaona jana usiku nilirudi nyumbani kwa huzuni kubwa Sana, aibu na maumivu.

Nilikua zangu road nikasema Wacha niende rock city mall nikashangae maghorofa, nikajikuta nimeingia CASK bar maana nilisikia Fid q atakuepo kwa sababu Mimi ni mdau wa hip-hop nikaona acha nijisogeze nikasikie Ngoma kama bongo hiphop, I'm professional n.k.

Kufika nikakuta kwanza parking magari yamejaa yaani watoto ni wakali sijawahi ona, size zote zipo, class A, wachafu, wazuri yaani ni wewe tu, mluga luga nikasema Leo lazima niopoe nilikua na 50,000/= mfukoni nikasema Leo watanikoma sitakosa mtoto hata wa 20,000/=
Nikanyooka mpaka counter nipate hata wine chupa ndogo Ile ya imagi nizuge nayo huku nikiendelea kuangalia mrembo yupi atanifaa nichomoke nae, huku kitaa hiyo wine Wanauza 3500/= Sasa yule counter hakunisikia vizuri akaleta chupa ya maji akanambia 4000/= chupa ndogo nikamuuliza shingapi? huku nimepigwa na butwaa kusikia hiyo bei ya maji, Pembeni yangu walikua wamekaa mademu wamechafua meza vibaya wamejaza windohek, hennesy n.k yaani waliokua pale counter hakuna aliekua mnyonge, kipindi naleta mshangao nikamwambia yule anaehudumia counter anirudishie hela yangu maana siwezi nunua maji Mls 700 kwa 4000/= wakati hata bombani yapo, kipindi naondoka nikasikia vicheko kutoka kwa wadada na washikaji waliokua counter.

Nikaona huku nimekosea njia nimeingia kwenye Chaka la matajiri, hata sikumsubiri fid q aje nikatoka Moja kwa Moja mpaka nje huku niliona kama Kila mtu ananicheka kwa fedhea, nikaondoka kinyonge nikatembea kwa mguu mpaka coner ya bwiru kinyonge huyoo nikaingia gheto kulala huku moyoni nikiwa na masononeko.


View attachment 2859139
View attachment 2859140


Hila wadau tuambiane ukweli mnapata pesa wapi za kuspend kiroho mbaya hivyo? Hamna majukumu? Au mna pesa nyingi Sana mnatafuta sehemu ya kuzitumia?
Seen.
 
Back
Top Bottom