Nawaasa sana mkae mbali na mpira hasa kama ni siku nyingi hamjacheza.
Jana baada ya kutoka job nilipofika nyumbani nilikuta wanangu wawili wa kiume wanacheza mpira pale nyumbani.
Sasa nikataka nijikumbushie umaridadi wangu kidogo, kuna style ile unaiunua mpira ukidunda ni kama unaupiga kwa nguvu (dochi) urudi sakafuni ili udunde kwa nguvu, ni kama ile ya Gabriel Batistuta.
Sasa ile mara ya kwanza nimejaribu nikaona mpira umedunda kidogo, ikabidi nitumie nguvu kubwa sana kuupiga ulipotua anga za chini, La haula!! niliukosa mpira kidole gumba kikagonga sakafu kwa nguvu sana.
Nilihisi kidole gumba kama kimeingia ndani hivi, Nilianza kusikia maumivu kwa mbali sana nikadhani yatapotea baada ya dakika chache.
Nikaenda kujipumzisha kitandani, hapo ndipo hali ilipokuwa mbaya zaidi, nilihisi mapigo yote ya moyo yamehamia kwenye kidole gumba na maumivu yalikuwa makali mno, mke wangu aliniletea barafu lakini wapi, nilitumia panadol lakini hamna kitu.
Wife akaniacha akaenda sebelni kuwapa kampani watoto basi huo mda ndio niliutumia kukubali tu nimeshindwa kuvumilia yani kwa yale maumivu nililia kama mtoto ndani ya blanketi, ahhh sio kwa maumivu yale, hata nilipoletewa chakula kitandani nilimwambia arudishe tu nikiwa nimeficha uso ndani ya blanketi, ilibidi usiku huo huo niwaombe waende duka la dawa kuninunulia dawa ya usingizi.
Cha kushukuru usingizi ulinipitia, nakuja kustuka ni saa 12 asubuhi na maumivu, kitu cha kwanza kufikiria ni kidole, nkajaribu kukikunja nikaweza japo kwa maumvu ya mbali sana, nilishukuru sana maana jana hata kukunja idole ilishindikana kabisa, yaani hata kukimnya tu ilikuwa ni maumivu.
Nawaasa sana mkae mbali na mpira hasa kama ni siku nyingi hamjacheza.