Jana ulikuwa ni mkutano wa CCM uliovalishwa vazi la CHADEMA

Watetezi wa wananchi kwa sasa ni team magu tu, wapinzani washalambishwa asali.😀😀
Hawaoni hata haja ya kuzungumzia mfumuko wa bei, mikopo isiyo na tija, safari na ziara za viongozi ndani na nje ya nchi. Wao ni kupongeza tu!

😂😂😂
 
Mtoa hoja jipiganie mwenyewe kwa hayo unayoyaamini uliyoyaandika humu, usijifanye shujaa kwa kujificha kwa ID fake hizi,Mh.Mbowe amekaa jela zaidi ya 150days bila ya kuwa na wapendwa wake, wewe ulifanya nini?maana muda wote ulikuwa na familia yako, Mh.Mbowe he done his bit sasa ni wakati wa ninyi middle class kujitokeza na kufanya mabadiliko ya kuisukuma nchi yetu mbele, it's craze mtu unatumia muda mwingi kumlaumu mtu mwingine eti akupiganie haki zako, uoga na uzuzu wa middle class ni cancer ndani ya nchi hii
Kwani yeye ndio wa kwanza kukaa jela?
Walikaa akina mandela et al, na bado walibaki na msimamo wao. Siasa za nchi hii ni against a person and not a system! Wao walimchukia mtu, hawakuchukia mfumo
 
Watetezi wa wananchi kwa sasa ni team magu tu, wapinzani washalambishwa asali.😀😀
Hawaoni hata haja ya kuzungumzia mfumuko wa bei, mikopo isiyo na tija, safari na ziara za viongozi ndani na nje ya nchi. Wao ni kupongeza tu!
Wewe umefanya juhudi gani to push back hayo uliyoyaorodhesha hapo juu?,jitokeze hadharani na pigana ,sio kujificha na hizi I'd fake halafu unajifanya shujaa, Mh.Mbowe kuwekwa ndani pale segerea, wewe hujawahi hata kuwekwa ndani kituo cha police cha kata, sasa unajifanya shujaa, pigana mwenyewe usitegemee watu wakupiganie
 
Mtoa hoja jipiganie mwenyewe kwa hayo unayoyaamini uliyoyaandika humu, usijifanye shujaa kwa kujificha kwa ID fake hizi,Mh.Mbowe amekaa jela zaidi ya 150days bila ya kuwa na wapendwa wake, wewe ulifanya nini?maana muda wote ulikuwa na familia yako, Mh.Mbowe he done his bit sasa ni wakati wa ninyi middle class kujitokeza na kufanya mabadiliko ya kuisukuma nchi yetu mbele, it's craze mtu unatumia muda mwingi kumlaumu mtu mwingine eti akupiganie haki zako, uoga na uzuzu wa middle class ni cancer ndani ya nchi hii

Mimi sijataka kupiganiwa na yeyote.
Nafikiri hata watanzania wengi hawajataka kupiganiwa, siku wakitaka kupiganiwa ndio mabadiliko yatakapotokea.

Kila MTU yupo kwaajili ya familia yake, na ukishakuwa Kwa ajili ya familia yako, automatically utakuwa KWAAJILI ya nchi yako
 
CHADEMA limebaki jina tu. Ila imechoka chakaliii.

Unapandisha jukwaani mianasiasa iliyokula IMESHIBA inaongea ikihema JUU JUU.

Sura zile zile kwa miaka 15 Sasa.

Stori zile zile.

Siasa zile zile.

Hakuna JIPYA.
 
Yani jana wamechemka hasa watu hawakuamini kama ni mbowe yule anaongea au mzimu wake

Hakika mwenyekiti kalambishwa asali si bure,sasa kama hautakuwa na nguvu ya kuisema CCM na mwenyekiti wake kuna upinzani hapo?

Mkutano wao wa jana umedhihirisha upinzani bongo hakuna wamejaa wachumia tumbo tu

Kazi ipo.
 
Fair enough, just shut up na hizi lawama kwa Mh. Mbowe it's totally unnecessary, pigana kwa familia yako, Mh.Mbowe hawezi kutupigania sisi wakati tumejificha chini ya uvungu wa vitanda vyetu, wewe umeshawahi hata kulala siku moja pale central police Dar kule shimoni?,tuache hizi lawama za kipuuzi, Mh.Mbowe amejaribu it's enough sasa na wengine nao waingize vichwa vyao
 
Wewe umefanya juhudi gani to push back hayo uliyoyaorodhesha hapo juu?,jitokeze hadharani na pigana ,sio kujificha na hizi I'd fake halafu unajifanya shujaa, Mh.Mbowe kuwekwa ndani pale segerea, wewe hujawahi hata kuwekwa ndani kituo cha police cha kata, sasa unajifanya shujaa, pigana mwenyewe usitegemee watu wakupiganie
Uko sahihi kabisa. Na maana yake ni kwamba hana sifa za kuwapigania wananchi anaowaaminisha kwamba atawaletea ukombozi. Musa wa nchi hii kwa kipindi hiki alikuwa JPM. Wao wakamuona adui. Sasa wamepoteza dira. 😀😀 na badoooo
 
Yani jana wamechemka hasa watu hawakuamini kama ni mbowe yule anaongea au mzimu wake

Hakika mwenyekiti kalambishwa asali si bure,sasa kama hautakuwa na nguvu ya kuisema CCM na mwenyekiti wake kuna upinzani hapo?

Mkutano wao wa jana umedhihirisha upinzani bongo hakuna wamejaa wachumia tumbo tu

Kazi ipo.
Wewe umeweka upinzani gani dhidi ya chama tawala?,nguvu za kuisema ccm itoke kwako sio kwa Mh.Mbowe, wewe unaogopa nini kufanya one man standing pale state house kupinga vitu ambavyo anaona hacienda Sawa hapa nchini?,woga uliokutawala ,sasa nyamaza mdomo wako kama huwezi kujipigania
 
Uko sahihi kabisa. Na maana yake ni kwamba hana sifa za kuwapigania wananchi anaowaaminisha kwamba atawaletea ukombozi. Musa wa nchi hii kwa kipindi hiki alikuwa JPM. Wao wakamuona adui. Sasa wamepoteza dira. 😀😀 na badoooo
Kwani wewe ndio msemaji wa hao wananchi?,wanaonwamini walikuwepo pale kumsikiliza, sasa kama unaona wewe u can do better anzisha chama chake na pigania hayo unayayaamini, but usitegemee mtu au watu wakupiganie
 
CHADEMA limebaki jina tu. Ila imechoka chakaliii.

Unapandisha jukwaani mianasiasa iliyokula IMESHIBA inaongea ikihema JUU JUU.

Sura zile zile kwa miaka 15 Sasa.

Stori zile zile.

Siasa zile zile.

Hakuna JIPYA.
ccm haina tofauti na Ile ya 60yrs ago na sitegemei watafanya tofauti, middle class ya kitanzania acheni uoga wa kupigania unachokiamini na usitegemee upiganiwe
 
Wewe umeweka upinzani gani dhidi ya chama tawala?,nguvu za kuisema ccm itoke kwako sio kwa Mh.Mbowe, wewe unaogopa nini kufanya one man standing pale state house kupinga vitu ambavyo anaona hacienda Sawa hapa nchini?,woga uliokutawala ,sasa nyamaza mdomo wako kama huwezi kujipigania

Wewe umeweka upinzani gani dhidi ya chama tawala?,nguvu za kuisema ccm itoke kwako sio kwa Mh.Mbowe, wewe unaogopa nini kufanya one man standing pale state house kupinga vitu ambavyo anaona hacienda Sawa hapa nchini?,woga uliokutawala ,sasa nyamaza mdomo wako kama huwezi kujipigania
Aliekwambia mimi ni mpinzani nani?tena mwambie mbowe hata huo uwenyekitii sasa basi maana hafai kuwa kiongozi wa upinzani na kwenda kusifia chama anachopinzana nacho,naona CHAWA wake umepanic hatari Ila habari ndio hiyo Jana kachemka na leo musoma hapati watu
 
Mimi sio chawa, mimi ni mtu ninayefanya push back 🔙 mwenyewe, sitegemei kupiganiwa haki yangu,CDM kupata watu au kutopata watu, time will tell ila wewe kuniambia hawatapata watu, ninakuweka kundi moja na Mwakipande
 
Kama amechoka kama usemavyo, kwa nini asipishe wengine wakiongoze chama?!
Usiweke maneno yako mdomoni mwangu, sijasema kama amechoka, la muhimu wewe mkuu nini kinakuogopesha kupigania haki zako?,mtoa hoja ametoa sababu nyingi tu kwenye uzi wake,sasa je yeye amefanya juhudi gani ndani ya nchi hii
 
JANA ULIKUWA NI MKUTANO WA CCM ULIOVALISHWA VAZI LA CHADEMA

Na, Robert Heriel

Jana agenda kuu ya mkutano ilikuwa kumshukuru na kumpongeza Rais, na ukimpongeza Rais tafsiri yake umeipongeza CCM. Ninaweza kusema Ulikuwa Mkutano wa CCM katika Vazi la CHADEMA. Na Hii ndio inaweza kutoa picha ni aina gani ya Siasa katika nchi hii tulizonazo.

Hakukuwa na sababu hata moja ya kumtaja Rais achilia mbali kumsifia kama kweli ule ungekuwa Mkutano wa CHADEMA.

Mwenyekiti Mbowe na viongozi wengine waliomsifia mwenyekiti wa CCM, Mhe. Rais, Dr Samia Suluhu , wamefanya kosa kubwa kisiasa, kiushawishi.
Kimantiki, Kilichokuwa kinafanyika Jana ni kuushawishi umma wa watanzania waikubali CCM na kumuamini Rais Samia katika kuongoza Dola.
Sio ajabu Mbowe alizomewa, na walikuwa na Haki ya kumzomea wafuasi wa Chadema,
Jambo ambalo kama ingekuwa ni Mkutano wa CHADEMA lisingetokea, kama ungekuwa Mkutano wa Chadema, basi wazungumzaji wote waliopewa nafasi ya kusimama kuzungumza wangewashawishi Watu Kwa hoja namna CCM na Mwenyeketi wake walivyokosa Sifa na vigezo vya kuongoza taifa hili.
Mkutano wa Jana Mwanza wa CCM, umejaribu kuonyesha Watu wa nchi hii picha halisi ya wapinzani tulionao.

Hakuna anayetaka Siasa za matusi, Mhe. Mbowe kusema kuwa ati hatamtukana Mwenyekiti wa CCM, inashangaza, hakuna aliyemuambia amtukane.
Wanachokataa ni Mbowe kuwa upande wa Samia, kuwa CCM.
Tafsiri yake ni kuwa Wanachadema hawataki kuongozwa na MTU aliyeupande wa CCM.

Wanachadema wanaposema Mbowe analamba Asali, bila Shaka wanarejelea maana ya kuwa Mbowe yupo upande wa Watawala wa CCM. Indirect way wanajaribu kusema Mbowe ni CCM.
Na kama Mbowe yupo upande wa CCM automatically Mkutano wa Jana ulikuwa wa CCM.

Kulikuwa na hoja nyingi za msingi za kuzizungumzia,
1. Mbowe alipaswa aanzie alipoishia, kuwekwa ndani na baadaye kesi yake kufutwa.
Ingawaje ni Jambo gumu 😀 lakini angeanzia hapo
Mfano Lisu yeye huanziaga pale alipopigwa Risasi. Wanasema ukitaka kumuua nyoka anzia miguuni.

2. Hoja Katiba Mpya, Hii wameijadili lakini katika kiwango cha Chini.

3. Hoja ya Hali ngumu ya Maisha.
Mkutano wa Jana ungepaswa utoe muhtasari wa jinsi serikali iliyopo madarakani ilivyoshindwa kuwapa unafuu Wananchi. Bei za bidhaa zipo juu. Wananchi wanataabika.
Badala yake wanasifia CCM.
Mpaka unajiuliza ulikuwa Mkutano wa chama cha upinzani kweli au Laa.

4. Hoja za Haki na Uhuru wa kujieleza.
Katika uwasilishaji wangejaribu kuwashawishi Watu namna gani walivyofanikiwa kupigania hilo eneo.
Hoja zao zijikite kuwa kila Mafanikio na Maendeleo ya haki na Uhuru ndani ya nchi hii yamechangiwa Kwa kiasi kikubwa na Chadema.
Wangetakiwa wasema hata kuruhusiwa kwa mikutano ya kisiasa ni Kutokana na juhudi zao.
Na watahakikisha kuwa Haki na Uhuru watavipigania Kwa gharama yoyote.
Hivi MTU akisema hivyo ametukana popote, amevunja sheria yoyote, jibu ni Hapana.
Sasa unapomsifia hasimu wako kuwa bila yeye mikutano isingeruhusiwa unajaribu kuwaambia nini Wananchi?

Yaani ni sawasawa unaenda mtongoza Demu, alafu badala ujisifie wewe ATI unamsifia Mshindani wako. Unategemea Demu atakuonaje, si atakuona hamnazo!

5. Hoja ya UMOJA na USHIRIKIANO.
Katika Mkutano, Chadema ingeeleza Kwa namna gani CCM ilivyoshindwa kuleta UMOJA na USHIRIKIANO ndani ya nchi. Kwa Hoja ZENYE mashiko na mifano dhahiri Wananchi wangeelewa.
Kisha iseme, Chadema Ipo kwaajili ya kuijenga nchi hii katika UMOJA na USHIRIKIANO. Sio kama CCM walivyofanya(unataja mifano).

Binafsi nimesikitishwa na chama ambacho ni kikubwa chenye miaka 30 Kwa Makusudi kabisa kikashindwa kuifanya siku ya Jana kuwa siku kweli ya uzinduzi.
Badala yake wamezindua UCCM.

Kama tutaweka unafiki pembeni, nataka kusema, viongozi wa Chadema wamewaangusha wanachadema,
CCM inawazidije ujanja,
Sasa si Bora hata msingefanya Mkutano kuliko kupoteza Muda na Pesa.

CCM wenzenu watapitia humohumo kwenye mapungufu yenu.

CCM ninavyowajua watakuja na kuwapaka Mavi mnuke,

Mimi ngoja nipumzike.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es
Mbowe ametumia busara kubwa angalau kupata mwanya wa kurudishwa kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa. Mbowe anaelewa vizuri uchanga wa demokrasia yetu na hangependa kuona CCM na dola yake wanapata mwanya wa kufanya ubabe wa kisiasa kama ilivyotokea siku zilizopita.

Kwa mwenye busara ataona hakukuwa na haja ya kuanza na gia kubwa. Ule ni mikutano wa ufunguzi tu sio sawa kumkosoa Mbowe kwa kutokuzungumzia kila kitu. Hata akitumia mikutano mitano ya kwanza hataweza kuzungumzia yote yapasayo, yapo mengi na kila mikutano una jambo lake na sio busara kurudia rudia yale yale kwenye mikutano ijayo.

Hakuna shida yoyote kumsifu mama angalau kwa kuridhia mikutano japo Mbowe anajua wazi kuwa ni haki kikatiba kufanya mikutano. Hiyo ni political tactic tunajua Mbowe atabadilisha gia angani pindi ndege itakapokuwa hewani. Hongera Mbowe kwa busara za hali ya juu za kisiasa!
 
Fair enough, just shut up na hizi lawama kwa Mh. Mbowe it's totally unnecessary, pigana kwa familia yako, Mh.Mbowe hawezi kutupigania sisi wakati tumejificha chini ya uvungu wa vitanda vyetu, wewe umeshawahi hata kulala siku moja pale central police Dar kule shimoni?,tuache hizi lawama za kipuuzi, Mh.Mbowe amejaribu it's enough sasa na wengine nao waingize vichwa vyao

Unaposema shut up unamaanisha nini?
 
Mbowe ametumia busara kubwa angalau kupata mwanya wa kurudishwa kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa. Mbowe anaelewa vizuri uchanga wa demokrasia yetu na hangependa kuona CCM na dola yake wanapata mwanya wa kufanya ubabe wa kisiasa kama ilivyotokea siku zilizopita.

Kwa mwenye busara ataona hakukuwa na haja ya kuanza na gia kubwa. Ule ni mikutano wa ufunguzi tu sio sawa kumkosoa Mbowe kwa kutokuzungumzia kila kitu. Hata akitumia mikutano mitano ya kwanza hataweza kuzungumzia yote yapasayo, yapo mengi na kila mikutano una jambo lake na sio busara kurudia rudia yale yale kwenye mikutano ijayo.

Hakuna shida yoyote kumsifu mama angalau kwa kuridhia mikutano japo Mbowe anajua wazi kuwa ni haki kikatiba kufanya mikutano. Hiyo ni political tactic tunajua Mbowe atabadilisha gia angani pindi ndege itakapokuwa hewani. Hongera Mbowe kwa busara za hali ya juu za kisiasa!
 
Mimi sio chawa, mimi ni mtu ninayefanya push back 🔙 mwenyewe, sitegemei kupiganiwa haki yangu,CDM kupata watu au kutopata watu, time will tell ila wewe kuniambia hawatapata watu, ninakuweka kundi moja na Mwakipande
Huna lolote hizo push back zako so far zimezaa matunda gani?au unazifanyia nyuma ya keyboard kama unachofanya sasa?haitakusaidia,na kinachokufanya usifike kokote ni huko kupigania haki yako tu sasa subiri UONE huo ubinafsi wako utakufikisha wapi,mpaka mvi zitakuota unasema unapigania haki yako,kila mtu akisema anapigania hali yake patatosha?nini maana ya kuwa na viongozi??????tunapiga Kura ili iweje???????
 
Basi sawa, lakini mleta hoja nadhani anayo hoja ya msingi.

Yesterday it was a "missed opportunity." Kila mmoja akikaa akatafakari moyoni analithibitisha hilo.
Kumbuka jana ilikuwa siku moja tu ya kwanza ya ufunguzi wa mikutano na kwamba zipo siku nyingi mno na mambo yote yataongelewa.
 
Back
Top Bottom