Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Team "maliyemu"?Hamjapona ugonjwa wenu wa kuangukaanguka?😜😜😜😜Watetezi wa wananchi kwa sasa ni team magu tu, wapinzani washalambishwa asali.😀😀
Hawaoni hata haja ya kuzungumzia mfumuko wa bei, mikopo isiyo na tija, safari na ziara za viongozi ndani na nje ya nchi. Wao ni kupongeza tu!
CCM haina jipya, inaishi kwa nguvu ya Dola na rushwa Wala Hilo siyo la kujiuliza.ccm haina tofauti na Ile ya 60yrs ago na sitegemei watafanya tofauti, middle class ya kitanzania acheni uoga wa kupigania unachokiamini na usitegemee upiganiwe
Huna lolote hizo push back zako so far zimezaa matunda gani?au unazifanyia nyuma ya keyboard kama unachofanya sasa?haitakusaidia,na kinachokufanya usifike kokote ni huko kupigania haki yako tu sasa subiri UONE huo ubinafsi wako utakufikisha wapi,mpaka mvi zitakuota unasema unapigania haki yako,kila mtu akisema anapigania hali yake patatosha?nini maana ya kuwa na viongozi??????tunapiga Kura ili iweje???????
Umetoa hoja kuntu wenye uelewa mdogo wameeanza kukuatack we binafsi badala ya hoja,itoshe kumsema nchi hii inavijana wengi wasiojitambua wao kutwa kupenda kuwa chawa
Siri kubwa: Siku zote anza taratibu na weka akiba ya maneno. Vinginevyo utashindwa kwenda juu!Ni kweli mkuu nalitambua hilo.
Lakini baada ya miaka takribani 6 ya bila mikutano, first gear ilikuwa crucial. Mwenyekiti alionekana kama hakujiandaa, ndio maana watu wanaulizana alilewa? Asali? Kutishwa? Nk
Ndo, sasa wananchi tunajiuliza ni bora hata wasingefanya mkutano kama hawana mawazo mbadala ya kuisadia nchi kujikwamua.
Hata cover la nje ya kitabu husadifu maudhui yaliyomo ndani. Vivyo hivyo, mkutano wa jana umeweka template ya mikutano ijayo.
Anyways!
Sophia Mjema kapata msaidizi ambaye ni Mbowe, mbowe sasa kawa Katibu Mwenezi msaidizi wa CCM Taifa. Mbowe jana kadhidirisha uchawa kwa Samia na hakuona ukubwa wa mkutano wa jana akaamua kutudharau akaja viwanjani kalewa chakali. Hakuna haja ya kuhudhuria mikutano ya Mbowe kama Chama mbadala wa CCM maana hakuna jipya utakalolisikia.Na, Robert Heriel
Jana agenda kuu ya mkutano ilikuwa kumshukuru na kumpongeza Rais, na ukimpongeza Rais tafsiri yake umeipongeza CCM. Ninaweza kusema Ulikuwa Mkutano wa CCM katika Vazi la CHADEMA. Na Hii ndio inaweza kutoa picha ni aina gani ya Siasa katika nchi hii tulizonazo.
Hakukuwa na sababu hata moja ya kumtaja Rais achilia mbali kumsifia kama kweli ule ungekuwa Mkutano wa CHADEMA.
Mwenyekiti Mbowe na viongozi wengine waliomsifia mwenyekiti wa CCM, Rais, Dr Samia Suluhu, wamefanya kosa kubwa kisiasa, kiushawishi.
Kimantiki, Kilichokuwa kinafanyika Jana ni kuushawishi umma wa watanzania waikubali CCM na kumuamini Rais Samia katika kuongoza Dola.
Sio ajabu Mbowe alizomewa, na walikuwa na haki ya kumzomea wafuasi wa Chadema. Jambo ambalo kama ingekuwa ni Mkutano wa CHADEMA lisingetokea.
Kama ungekuwa Mkutano wa Chadema, basi wazungumzaji wote waliopewa nafasi ya kusimama kuzungumza wangewashawishi watu kwa hoja namna CCM na Mwenyeketi wake walivyokosa sifa na vigezo vya kuongoza taifa hili.
Mkutano wa Jana Mwanza wa CCM, umejaribu kuonyesha watu wa nchi hii picha halisi ya wapinzani tulionao.
Hakuna anayetaka siasa za matusi, Mbowe kusema kuwa ati hatamtukana Mwenyekiti wa CCM, inashangaza, hakuna aliyemuambia amtukane. Wanachokataa ni Mbowe kuwa upande wa Samia, kuwa CCM. Tafsiri yake ni kuwa Wanachadema hawataki kuongozwa na MTU aliyeupande wa CCM.
Wanachadema wanaposema Mbowe analamba Asali, bila Shaka wanarejelea maana ya kuwa Mbowe yupo upande wa watawala wa CCM. Indirect way wanajaribu kusema Mbowe ni CCM. Na kama Mbowe yupo upande wa CCM automatically Mkutano wa Jana ulikuwa wa CCM.
Kulikuwa na hoja nyingi za msingi za kuzizungumzia,
1. Mbowe alipaswa aanzie alipoishia, kuwekwa ndani na baadaye kesi yake kufutwa. Ingawaje ni Jambo gumu [emoji3] lakini angeanzia hapo. Mfano Lissu yeye huanziaga pale alipopigwa Risasi. Wanasema ukitaka kumuua nyoka anzia miguuni.
2. Hoja ya Katiba Mpya, hii wameijadili lakini katika kiwango cha Chini.
3. Hoja ya Hali ngumu ya Maisha. Mkutano wa Jana ungepaswa utoe muhtasari wa jinsi serikali iliyopo madarakani ilivyoshindwa kuwapa unafuu Wananchi. Bei za bidhaa zipo juu. Wananchi wanataabika. Badala yake wanasifia CCM. Mpaka unajiuliza ulikuwa Mkutano wa chama cha upinzani kweli au Laa.
4. Hoja za Haki na Uhuru wa kujieleza.
Katika uwasilishaji wangejaribu kuwashawishi watu namna gani walivyofanikiwa kupigania hilo eneo. Hoja zao zijikite kuwa kila mafanikio na Maendeleo ya haki na Uhuru ndani ya nchi hii yamechangiwa Kwa kiasi kikubwa na Chadema.
Wangetakiwa wasema hata kuruhusiwa kwa mikutano ya kisiasa ni Kutokana na juhudi zao. Na watahakikisha kuwa Haki na Uhuru watavipigania Kwa gharama yoyote.
Hivi MTU akisema hivyo ametukana popote, amevunja sheria yoyote, jibu ni Hapana. Sasa unapomsifia hasimu wako kuwa bila yeye mikutano isingeruhusiwa unajaribu kuwaambia nini Wananchi?
Yaani ni sawasawa unaenda mtongoza Demu, alafu badala ujisifie wewe ATI unamsifia Mshindani wako. Unategemea Demu atakuonaje, si atakuona hamnazo!
5. Hoja ya UMOJA na USHIRIKIANO.
Katika Mkutano, Chadema ingeeleza kwa namna gani CCM ilivyoshindwa kuleta UMOJA na USHIRIKIANO ndani ya nchi. Kwa Hoja ZENYE mashiko na mifano dhahiri Wananchi wangeelewa.
Kisha iseme, Chadema Ipo kwaajili ya kuijenga nchi hii katika UMOJA na USHIRIKIANO. Sio kama CCM walivyofanya(unataja mifano).
Binafsi nimesikitishwa na chama ambacho ni kikubwa chenye miaka 30 Kwa Makusudi kabisa kikashindwa kuifanya siku ya Jana kuwa siku kweli ya uzinduzi. Badala yake wamezindua UCCM.
Kama tutaweka unafiki pembeni, nataka kusema, viongozi wa Chadema wamewaangusha wanachadema,
CCM inawazidije ujanja, Sasa si Bora hata msingefanya Mkutano kuliko kupoteza Muda na Pesa.
CCM wenzenu watapitia humohumo kwenye mapungufu yenu.
CCM ninavyowajua watakuja na kuwapaka Mavi mnuke,
Mimi ngoja nipumzike.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es
Siri kubwa: Siku zote anza taratibu na weka akiba ya maneno. Vinginevyo utashindwa kwenda juu!
Watu wanamsikiliza Kiongozi.
Atakachoongea Kiongozi Mkuu ndio kinasikilizwa.
Hao wengine hatuwazingatii sana
Mandela aliyeingia gerezani sio yule aliyetoka[emoji2]Kwani yeye ndio wa kwanza kukaa jela?
Walikaa akina mandela et al, na bado walibaki na msimamo wao. Siasa za nchi hii ni against a person and not a system! Wao walimchukia mtu, hawakuchukia mfumo
Kiongozi mkuu halisi wa sasa tunayesubiri kumsikiliza ni Tundu Lisu. Huyo Mbowe hata kabla ya mkutano wa jana tayari alishapoteza imani yetu.
Watetezi wa wananchi kwa sasa ni team magu tu, wapinzani washalambishwa asali.😀😀
Hawaoni hata haja ya kuzungumzia mfumuko wa bei, mikopo isiyo na tija, safari na ziara za viongozi ndani na nje ya nchi. Wao ni kupongeza tu!
😂😂🤣
Ingefaa astaafu Kwa heshima alafu awaachie kijiti wengine kama yeye keshaingia hofu, au utu uzima umemkabili,
Hizo ndio busara za siasa za Tanzania na hata Samia mwenyewe anaelewa nini maana ya “kusifiwa” na Mbowe. Mbowe asingekuwa na busara za kisiasa kwa hakika Magufuli angelisha mmaliza siku nyingi!Lakini kumsifia hasimu wako Mbele ya Mkeo na wanao Huko sio kuanza taratibu Mkuu.
Haikupaswa kivyovyote Chadema kuisifia CCM.
Hili limekuwa pendekezo langu la msingi, toka afanye blunder ya kumpokea Lowassa. Nashangaa hata uchaguzi uliopita aligombea uenyekiti tena. Hastahili kabisa kwa sasa nafasi hiyo.
Hili limekuwa pendekezo langu la msingi, toka afanye blunder ya kumpokea Lowassa. Nashangaa hata uchaguzi uliopita aligombea uenyekiti tena. Hastahili kabisa kwa sasa nafasi hiyo.
CHADEMA limebaki jina tu. Ila imechoka chakaliii.
Unapandisha jukwaani mianasiasa iliyokula IMESHIBA inaongea ikihema JUU JUU.
Sura zile zile kwa miaka 15 Sasa.
Stori zile zile.
Siasa zile zile.
Hakuna JIPYA.
Haikuwa Kete nzuri Kwa kweli, Lowasa ndiye aliyeimaliza chadema,