Jana ulikuwa ni mkutano wa CCM uliovalishwa vazi la CHADEMA

Watetezi wa wananchi kwa sasa ni team magu tu, wapinzani washalambishwa asali.πŸ˜€πŸ˜€
Hawaoni hata haja ya kuzungumzia mfumuko wa bei, mikopo isiyo na tija, safari na ziara za viongozi ndani na nje ya nchi. Wao ni kupongeza tu!

πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Kwani yeye ndio wa kwanza kukaa jela?
Walikaa akina mandela et al, na bado walibaki na msimamo wao. Siasa za nchi hii ni against a person and not a system! Wao walimchukia mtu, hawakuchukia mfumo
 
Watetezi wa wananchi kwa sasa ni team magu tu, wapinzani washalambishwa asali.πŸ˜€πŸ˜€
Hawaoni hata haja ya kuzungumzia mfumuko wa bei, mikopo isiyo na tija, safari na ziara za viongozi ndani na nje ya nchi. Wao ni kupongeza tu!
Wewe umefanya juhudi gani to push back hayo uliyoyaorodhesha hapo juu?,jitokeze hadharani na pigana ,sio kujificha na hizi I'd fake halafu unajifanya shujaa, Mh.Mbowe kuwekwa ndani pale segerea, wewe hujawahi hata kuwekwa ndani kituo cha police cha kata, sasa unajifanya shujaa, pigana mwenyewe usitegemee watu wakupiganie
 

Mimi sijataka kupiganiwa na yeyote.
Nafikiri hata watanzania wengi hawajataka kupiganiwa, siku wakitaka kupiganiwa ndio mabadiliko yatakapotokea.

Kila MTU yupo kwaajili ya familia yake, na ukishakuwa Kwa ajili ya familia yako, automatically utakuwa KWAAJILI ya nchi yako
 
CHADEMA limebaki jina tu. Ila imechoka chakaliii.

Unapandisha jukwaani mianasiasa iliyokula IMESHIBA inaongea ikihema JUU JUU.

Sura zile zile kwa miaka 15 Sasa.

Stori zile zile.

Siasa zile zile.

Hakuna JIPYA.
 
Yani jana wamechemka hasa watu hawakuamini kama ni mbowe yule anaongea au mzimu wake

Hakika mwenyekiti kalambishwa asali si bure,sasa kama hautakuwa na nguvu ya kuisema CCM na mwenyekiti wake kuna upinzani hapo?

Mkutano wao wa jana umedhihirisha upinzani bongo hakuna wamejaa wachumia tumbo tu

Kazi ipo.
 
Fair enough, just shut up na hizi lawama kwa Mh. Mbowe it's totally unnecessary, pigana kwa familia yako, Mh.Mbowe hawezi kutupigania sisi wakati tumejificha chini ya uvungu wa vitanda vyetu, wewe umeshawahi hata kulala siku moja pale central police Dar kule shimoni?,tuache hizi lawama za kipuuzi, Mh.Mbowe amejaribu it's enough sasa na wengine nao waingize vichwa vyao
 
Uko sahihi kabisa. Na maana yake ni kwamba hana sifa za kuwapigania wananchi anaowaaminisha kwamba atawaletea ukombozi. Musa wa nchi hii kwa kipindi hiki alikuwa JPM. Wao wakamuona adui. Sasa wamepoteza dira. πŸ˜€πŸ˜€ na badoooo
 
Wewe umeweka upinzani gani dhidi ya chama tawala?,nguvu za kuisema ccm itoke kwako sio kwa Mh.Mbowe, wewe unaogopa nini kufanya one man standing pale state house kupinga vitu ambavyo anaona hacienda Sawa hapa nchini?,woga uliokutawala ,sasa nyamaza mdomo wako kama huwezi kujipigania
 
Uko sahihi kabisa. Na maana yake ni kwamba hana sifa za kuwapigania wananchi anaowaaminisha kwamba atawaletea ukombozi. Musa wa nchi hii kwa kipindi hiki alikuwa JPM. Wao wakamuona adui. Sasa wamepoteza dira. πŸ˜€πŸ˜€ na badoooo
Kwani wewe ndio msemaji wa hao wananchi?,wanaonwamini walikuwepo pale kumsikiliza, sasa kama unaona wewe u can do better anzisha chama chake na pigania hayo unayayaamini, but usitegemee mtu au watu wakupiganie
 
CHADEMA limebaki jina tu. Ila imechoka chakaliii.

Unapandisha jukwaani mianasiasa iliyokula IMESHIBA inaongea ikihema JUU JUU.

Sura zile zile kwa miaka 15 Sasa.

Stori zile zile.

Siasa zile zile.

Hakuna JIPYA.
ccm haina tofauti na Ile ya 60yrs ago na sitegemei watafanya tofauti, middle class ya kitanzania acheni uoga wa kupigania unachokiamini na usitegemee upiganiwe
 

Aliekwambia mimi ni mpinzani nani?tena mwambie mbowe hata huo uwenyekitii sasa basi maana hafai kuwa kiongozi wa upinzani na kwenda kusifia chama anachopinzana nacho,naona CHAWA wake umepanic hatari Ila habari ndio hiyo Jana kachemka na leo musoma hapati watu
 
Mimi sio chawa, mimi ni mtu ninayefanya push back πŸ”™ mwenyewe, sitegemei kupiganiwa haki yangu,CDM kupata watu au kutopata watu, time will tell ila wewe kuniambia hawatapata watu, ninakuweka kundi moja na Mwakipande
 
Kama amechoka kama usemavyo, kwa nini asipishe wengine wakiongoze chama?!
Usiweke maneno yako mdomoni mwangu, sijasema kama amechoka, la muhimu wewe mkuu nini kinakuogopesha kupigania haki zako?,mtoa hoja ametoa sababu nyingi tu kwenye uzi wake,sasa je yeye amefanya juhudi gani ndani ya nchi hii
 
Mbowe ametumia busara kubwa angalau kupata mwanya wa kurudishwa kwa mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa. Mbowe anaelewa vizuri uchanga wa demokrasia yetu na hangependa kuona CCM na dola yake wanapata mwanya wa kufanya ubabe wa kisiasa kama ilivyotokea siku zilizopita.

Kwa mwenye busara ataona hakukuwa na haja ya kuanza na gia kubwa. Ule ni mikutano wa ufunguzi tu sio sawa kumkosoa Mbowe kwa kutokuzungumzia kila kitu. Hata akitumia mikutano mitano ya kwanza hataweza kuzungumzia yote yapasayo, yapo mengi na kila mikutano una jambo lake na sio busara kurudia rudia yale yale kwenye mikutano ijayo.

Hakuna shida yoyote kumsifu mama angalau kwa kuridhia mikutano japo Mbowe anajua wazi kuwa ni haki kikatiba kufanya mikutano. Hiyo ni political tactic tunajua Mbowe atabadilisha gia angani pindi ndege itakapokuwa hewani. Hongera Mbowe kwa busara za hali ya juu za kisiasa!
 

Unaposema shut up unamaanisha nini?
 
 
Mimi sio chawa, mimi ni mtu ninayefanya push back πŸ”™ mwenyewe, sitegemei kupiganiwa haki yangu,CDM kupata watu au kutopata watu, time will tell ila wewe kuniambia hawatapata watu, ninakuweka kundi moja na Mwakipande
Huna lolote hizo push back zako so far zimezaa matunda gani?au unazifanyia nyuma ya keyboard kama unachofanya sasa?haitakusaidia,na kinachokufanya usifike kokote ni huko kupigania haki yako tu sasa subiri UONE huo ubinafsi wako utakufikisha wapi,mpaka mvi zitakuota unasema unapigania haki yako,kila mtu akisema anapigania hali yake patatosha?nini maana ya kuwa na viongozi??????tunapiga Kura ili iweje???????
 
Basi sawa, lakini mleta hoja nadhani anayo hoja ya msingi.

Yesterday it was a "missed opportunity." Kila mmoja akikaa akatafakari moyoni analithibitisha hilo.
Kumbuka jana ilikuwa siku moja tu ya kwanza ya ufunguzi wa mikutano na kwamba zipo siku nyingi mno na mambo yote yataongelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…