Janet Yellen: Washington yatatokea madhara makubwa Marekani ikijitoa China

Micron ni kampuni ndogo sana mzee wangu. Walikuwa wanatengezea hard disk lakini wamepand kidogo siku hizi wanatengezea USB thumb drives na flash memory chips tu.
Yamekuwa hayo tena si mlisema mnaondoa makampuni yenu China mnaenda Thailand?

Mbona wameng'ang'ania China na wakati walipigwa ban 🤣🤣
 
Baada ya ziara za hao wafanyabiashara wakubwa kutoka Marekani

China itaanza kupokea wanasiasa kutoka Marekani, Blinken ataenda China mwezi huu
baadaye tena yule mama US treasury secretary Yellen naye ataenda China

Na wote agenda kuu ni economic cooperation. China is something else bro
 
Huyu kaja kuvuruga uhusiano uliojengwa na hao wenzake na kusababisha vurugu za sasa
Kati ya Xi na akina Trump na Biden nani wamevuruga uhusiano mzuri uliokuwepo kati ya China na Marekani

Kumbuka sikuzote chini ya utawala wa Trump na Biden Marekani ndio wamekuwa wa kwanza kuyafungia au kuyawekea vikwazo makampuni ya China

Na hayo makampuni yalikuwepo kipindi cha akina Clinton, Bush na Obama hatukuona yakifungiwa.
 
Hilo ni tatizo kwake kati ya ukuaji na ujenzi wa uchumi haya maneno mawili kwake yamekuwa changamoto
Ni changamoto sana. Shida inaanzia wapi unajua? Tayari mtu kama huyo ana mtazamo hasi kuelekea China, ni ngumu kuelewa mpaka aondoe hilo tatizo ndio ataanza kuelewa
 
Yamekuwa hayo tena si mlisema mnaondoa makampuni yenu China mnaenda Thailand?

Mbona wameng'ang'ania China na wakati walipigwa ban [emoji1787][emoji1787]

Vijana wa 2000’s hawawezi ijua historia ya China, wameshindwa Russia ndo wataweza China??. Micron wameamua kuwa wapole [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hata ukitembelea website za makampuni mengi ya China (China based companies& mfg industries) utakuta yalianzishwa zamani mengine tangu miaka ya 1950's hadi 1990's kabla hata West hawajaenda kuwekeza China
Mkuu uko sahihi sana hapa nina mifano michache ya viwanda na makampuni ya China yalikuwepo tangu zamani ila sisi tumeanza kuyafahamu miaka hii ya 2010's

YUTONG BUS kiwanda kilianzishwa tangu 1963

HUAWEI: 1987

SINOTRUK (HOWO): 1935

ZHONGTONG BUS: 1958

HISENSE: 1993

HAIER: 1984

ALIBABA: 1999

China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC): 1978
kampuni iliyojenga Kijazi Interchange, SGR Tabora hadi Kigoma

China Road and Bridge Corporation: 1979
Waliojenga SGR ya Kenya

Makampuni ni mengi huwezi kuyataja yote ila tukubali hawa jamaa Wachina walikuwa mbali hata kabla ya makampuni ya Ulaya na Marekani kuvutiwa kuwekeza kwao
 
Umeeleza vizuri sana.

TPP na Mzee wa kupambania mnaieleza vizuri sana China. Mko sahihi sana, nimekuwa China kwa miaka zaidi ya 15 nimejionea yote mnayoyasema.

China inayozungumziwa na mataifa ya Magharibi ni tofauti kabisa na China kwenyewe.

Tuna mengi ya kujifunza kutoka China si mtaalamu sana wa kuandika ila ningekmweza kuandika nyuzi za kujifunza kutoka china

Kwa wale wanaopinga china

The lesson to be learned from China's R&D is that progress requires long-term investment in human capital and physical capital and that making such investments or not making them can have major consequences for a nation's wellbeing.
 
Umesema vyema
 
Sisi waafrika bado hatujajua tunaelekea wapi ,ndo kwanza tunatengeneza madawati ya wanafunzi wetu watoe ujinga na ujinga nao hautaki kuwatoka, unadai utaenda wapi na aakati ndo umefika
 
Win win siyo kwamba utishie usalama wa majirani zako halafu wote tushangilie; kila mara kunapokuwa na matatizo ya wakimbizi huwa hawakimbilii China au Urusi, wote hukimbilia europe, US, Canada na Australia. Win win siyo kwamba urushe bumuda lako ndani ya mipaka yangu wazi wazi kupiga picha halafu mimi nishangilie kuwa hiyo ni wini wini. Ni failure kubwa sana ya diplomacy ambayo haikuwa miaka ya tisni na elfu mbili. Waziri wa ulizni wa marekani anasema tukutane na waziri wa ulizni wa china tuongee ili kupunguza tension baina yetu, lakini waziri wa china anasema kwa kiburi kuwa hana interest; mambo ya kijinga sana hayo. Kama waziri wa ulinzi hana interest ya kuondoa Tension na marekani, unaona kuwa ni unafiki kwa viongozi wa China kuitisha mikutano na viongozi wa biashara wa marekani, ingawa wao hawakujibu rudely kuwa hawana interest lakini walihudhuria mikutano hiyo ingawa wengine bado wanaendelea kuhamisha biashara zao kutoka China kwenda nchi za jirani.


 
Usipokuwa na uwezo wa kupambanua mambo utaamini kila habari iliyo YouTube

Ukiongeza maarifa na uwezo wa kupambanua mambo utajua ipi ya kweli na ipi ni uongo
 
Usipokuwa na uwezo wa kupambanua mambo utaamini kila habari iliyo YouTube

Ukiongeza maarifa na uwezo wa kupambanua mambo utajua ipi ya kweli na ipi ni uongo
Nikukuambia ukweli wewe unaukataa. Sasa nadhani ukiwasikia hao wachina wenyewe ambao siyo wapiga propaganda nadhani utawaamnini kuliko mimi mmatumbi. Mwingine ni huyu mwanamke ambaye nilikuwa sijamaliza kumsikiliza



Unapodai China walikuwa ni viwanda tangu zamani na kufanya kuwa hiyo ndiyo criterion yako, unasahahu kuwa hata North Korea walikuwa na viwanda, Czechoslovakia (kabla ya kuvunjika) walikuwa na Viwanda, na hata Argentina walikuwa na viwanda tangu zamani lakini uchumi wao haujakuwa. Ukiangalia kwa nini utagundua kuwa hawajawahi kupata investments kutoka West. Ila ukiambiwa ukweli unashindwa kuumeza na kujaribu kuendeleza propaganda. Nchi za kiimra kama china na Urusi ni wazuri sana kwa propaganda kwa vile wanachuja sana habari na wewe ni victim wa hizo propaganda.
 
Tuanze sasa Tanzania kuangalia namna ya kuwa na nguvu za kiuchumi hata kwa hila maana kila tukijaribu kupata investors tunaishia kuparurana.

Wananchi sisi tunataka maendeleo na siyo mbambamba
 
Nchi za kiimra kama china na Urusi ni wazuri sana kwa propaganda kwa vile wanachuja sana habari na wewe ni victim wa hizo propaganda.
World Bank na IMF ndio huwa wanatoa takwimu za uchumi wa China ambazo zinatumika duniani. Kama na wao huwaamini basi sina la kukusaidia endelea na video zako za youtube
 
West wameanza hasa kuwekeza China miaka gani?
 
World Bank na IMF ndio huwa wanatoa takwimu za uchumi wa China ambazo zinatumika duniani. Kama na wao huwaamini basi sina la kukusaidia endelea na video zako za youtube
Hukumsikiliza vizuri yule Mbunge wa Hong Kong kwenye video aliyokuwa anaongea na mtangazaji Mhindi. Ameeleza vizuri jinsi jinsi ambavyo IMF na World Bank wanakuwa misled na serikali ya China kwa kupewa data feki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…