Januari Makamba adai uchaguzi wa 2020 ulitugawa, watu walifungwa, walinyang'anywa pesa, na waliharibiwa biashara zao

Wanatumia nguvu kubwa kupigana na marehem
 
Utamdhibiti na katiba inamruhusu!? Utawezaje!?
 
Wazuri hawafi sijui mtaalam wao kaona nini huko maana sahivi wanaropokaropoka tu
 
🀣🀣🀣
 
Kweli kabisa ili waonekane wanatenda haki , nchi hii Ina wanafiki wengi sana
Tunahitaji JPM mpya wa kuja kufundisha Adabu maana kwa Sasa tumepoteza dira
 
January jiuzulu maana uchaguzi wa 2020 haukuwa wa haki na wewe ulipita bila kupingwa sababu ya Hila za uchaguzi wa 2020
 
Uko sahih
 
Kwa kisukuma huwa tunasema alikuwa β€˜Anayabhula β€œ πŸ˜…πŸ˜…πŸ™
 
Naomba nisimuwekee maneno Makamba.

Maneno aliyoyazungumza ni tuhuma nzito kwa utawala wa Rais Magufuli.
HAKUNA WATU WATAOUNGUZWA NA MOTO MBAYA KAMA WANASIASA TENA HUSUSAN WANASIASA WA TANZANIA.
Hii habari ya kumbeza asiyekuwepo ili kulinda ugali wa aliyekuwepo ni mbaya sana.
Kama mtu angelikua anafufuka huyu Makamba angelizungumza mengine tofauti na haya.
 
Yaliyopita si ndwele tugange ya sasa na yajayo πŸ’

changamoto zilizopitia ziwe ni fursa ya kutupa ujasiri wa kujisahihisha, kujirekebisha na kujipanga vizuri kwa wakati ujao ili tufanye vizuri zaidi ...

kukata tamaa au kughadhabishwa na maoni na mitazamo ya wengine juu ya yalio pita si muhimu sana πŸ’
 
Kweli kabisa
Wazuri hawafi sijui mtaalam wao kaona nini huko maana sahivi wanaropokaropoka tu
apumzike kwa amani.

Kweli kabisa ili waonekane wanatenda haki , nchi hii Ina wanafiki wengi sana
Tunahitaji JPM mpya wa kuja kufundisha Adabu maana kwa Sasa tumepoteza dira
Mnadanganyana kwa sababu hamna utamaduni wa kuupenda wala kuuzoea ukweli.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…