NAMBA MOJA AJAYE NCHINI
JF-Expert Member
- Oct 29, 2019
- 9,863
- 20,806
Usimfananishe lowasa na vitu vya hovyo mkuu!!Sio siri kuwa shauku ya mh Januari Makamba kuutaka urais ni kubwa sana pengine zaidi ya ile shauku ya mh Lowasa. Lakini kwa bahati mbaya mapito yake hayatatofautina na yale ya Mh Lowasa.
Atajitahidi sana, atakusanya watu, atakuwa kwenye makundi pendwa na hata nyakati nyingine atafika katika 5 bora, lakini kamwe hatachaguliwa kuwa mgombea Urais kupitia CCM.
Hata akifanya kama Lowassa, kuhamia upinzani nako atachaguliwa kuwa mgombea wa Urais lakini safari itaishia kama ile ya Mh Lowasa.
Mi sipendi aina ya vijana kama yeye wanaofikiri urais ni haki Yao ya msingi kama maji ya kunywa Tena wanautaka Kwa mbeleko za baba zao kisiasa!!
Angalau Dr. Hussein Mwinyi namkubali sana hakuonyesha kama anautaka kabisa lakini akawa coz system ilimuandaa!!
Huyo hawezi kua Raise was nchi nature ishamkataa kabisa!!
Wakiondoka hai anaowategemea na ndoto za urais unaishia hapo hapo!!