Januari Makamba atapita njia ya Hayati Lowassa katika safari yake ya kisiasa

Usimfananishe lowasa na vitu vya hovyo mkuu!!

Mi sipendi aina ya vijana kama yeye wanaofikiri urais ni haki Yao ya msingi kama maji ya kunywa Tena wanautaka Kwa mbeleko za baba zao kisiasa!!

Angalau Dr. Hussein Mwinyi namkubali sana hakuonyesha kama anautaka kabisa lakini akawa coz system ilimuandaa!!

Huyo hawezi kua Raise was nchi nature ishamkataa kabisa!!

Wakiondoka hai anaowategemea na ndoto za urais unaishia hapo hapo!!
 
Alipewa kuchagua wizara anayoipenda, jibu moja kwa moja likawa NISHATI. Samia akamzawadia na kumpa bajeti nzima ya NISHATI na ushehe. Sijui pesa kazipeleka wapi?

Wizara ya mambo ya nje haina pesa kama NISHATI. Mambo ya nje ni BENCHI. Huko kilio chake ni kizito.
Nafikiri ana hasira sana, kwani si Wizara aliyeipenda. Kimsingi Januari M nafasi ya Urais haiwezi. Ningemuomba alikubali hilo.
 
Moto Ni Mkali Na CCM Imepasuka Humo Humo Mbaya Zaidi Umemtaja Mmoja Ila Idadi Ni Kubwa Sana Wanaoutaka Urais Ukisema Tutasema Tanzania Itatikisika Mchana
 
Wagalatia/Walawi Mlisema Zamu Yao Sasa Ama Mmebadili Mnabaki Kobaz
 
Wanapofanana ni mwisho wa safari yao, na sio kwa akili au uwezo wa kutatua matatizo ya wananchi. Ile dhamira na shauku ya kuutaka Urais, hapo wanashabihiana.

Kwa mfano, Lowasa katuachia shule za KATA/ KUTWA ambazo ndio mombozi kwa walala hoi katikia kipengele cha Elimu. Kwa hili jina lake litaendelea kuishi kwa maisha yote ya kuwepo kwa mama Tanzania. Viatu kama hivi au mawazo kama haya ndio tatizo ambalo Januari M bado hajaonyesha popote pale.
 
Moto Ni Mkali Na CCM Imepasuka Humo Humo Mbaya Zaidi Umemtaja Mmoja Ila Idadi Ni Kubwa Sana Wanaoutaka Urais Ukisema Tutasema Tanzania Itatikisika Mchana
Idadi ni kubwa mno, lakini tofauti ni mbinu zinazotumika. Kuna ambao wanautaka lakini hawajaunda makundi na wala hawana mbinu chafu kufikia malengo yao. Hawa hatuna matatizo nao, na wajitokeze wengi tu.

Mbaya na kinachoniuma ni wale ambao wapotayari hata kutotoa huduma kwa wananchi wakidhani ndio njia pekee ya kumuangusha yule aliyewateua na anayetarajia kuwa mgombea. Mbinu hii inaniumiza mimi mwananchi wa kawaida na ndio maana napaza sauti.
Ni mara nyingi Rais amerudia kusema kuwa nimewachagua mkawahudumie watanzania, na si kujinadi katika uchaguzi ujao 2025.
 
Hawezi kuwa kama Lowasa, hana uwezo wa kuwa kama Lowasa na hawezi kuwa Lowasa kamwe....
 
Sema kifo cha Magufuli kimefanya ndoto za Urais kwa Makamba ziwe ngumu sana.
Hesabu Zimevurugika za wengi sana waliokuwa wanakinyemelea kiti ukizingatia 2025 tunaenda na Mama hadi 2030 wanachoka kabisa wanajikaza tu.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…