Mudawote
JF-Expert Member
- Jul 10, 2013
- 10,771
- 14,129
Leo Waziri wa Nishati, Januari Makamba amewajibu wanaohoji kuchelewa kwa Mradi wa Bwawa la Julius Nyerere JNHPP ni upuuzi tu na kama hawaamini majibu yake basi wamuue.
"Ukisema Bwawa litachelewa kwa sababu hii na hii wanasema muongo huyo, mshenzi huyo basi njooni mniue basi kama hamuamini, wote ni upuuzi tu" amesema Makamba
Chanzo: Wasafi Media
Kaka Makamba, kama unasoma hizi text elewa watanzania walikuwa na imani kubwa sana juu yako ila wewe mwenyewe uliiharibu na kuipunguza hiyo imani baada ya kuonekana unamkandia Dkt Magufuli. Pamoja na kuwa uliomba msamaha na Dkt Magufuli alikusamehe ila baada ya kifo chake ulionekana mwenye kufurahia kifo chake. Kosa lingine ulipoingia wizarani hapo kwenye nishati ulijinasibu kwa kusema serikali ya Dkt Magufuli chini ya uongozi wa wizara wa Dkt Kalemani TANESCO iliharibiwa, na kibaya zaidi ukasema eti kuna hujuma na ukaamua kuondoa top management yote. Hilo lilikuwa kosa kubwa sana ambalo wafanyakazi wa TANESCO mpaka leo umeonesha kwa kuwaambia unawaamini japo imani yao kwako haipo. Je ufanyeje? Nadhani jitahidi kukaa kimya, usipende kuongea ongea kwa sababu kila kauli yako adui zako wanaibeba na kuifanya ajenda. Kumbuka adui ulio nao ni wengi ukiacha na watanzania wanaokuchukia kwa sababu ya kumdharau Dkt Magufuli, kuna hawa wasaka urais, wanataka utu wako uchafuke ili ukose nafasi ya kuja kuwa Rais